HII NDIYO NJIA SAHIHI YA KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA MAHITAJI YA PESA

NENO LA LEO (JANUARI 14, 2021): HII NDIYO NJIA SAHIHI YA KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA MAHITAJI YA PESA

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambapo tumepewa kibali cha kuwa hai. Kibali hiki in cha kuwa na uwezo wa kuvuta pumzi ya hewa safi na kutoa hewa chafu na katika kufanya hivyo tunapata nguvu ya kutafuta ridhiki kupitia majukumu yetu ya kila siku. Kila unapovuta hewa safi (Oxyjeni) na kutoa hewa chafu (Carbondiode) unatakiwa kutambua kuwa unazalisha nguvu kupitia mmeng'enyo wa chakula na nguvu hizo zinatakiwa   kutumika kwa faida.

Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA

Mwanadamu ni kiumbe ambacho kinategemea uwepo wa pesa kwa ajili ya kukamilisha mahitaji ya msingi. Toka pesa ilipogunduliwa katika historia ya maendeleo ya Mwanadamu imekuwa ni nyenzo muhimu ya upatikanaji wa mahitaji ya msingi kwa mtu mmoja mmoja, familia na hata taifa. Hata hivyo, katika maendeleo ya Mwanadamu kadri umri kuongezeka ndivyo mahitaji ya pesa yanavyoongezeka. Hali iko hivyo pia kwa familia na hata taifa. Mara zote ukuaji wa mtu, familia au taifa huwa unaambatana na ongezeko la mahitaji ya pesa.

Tutakubaliana kuwa katika kipindi cha utoto mahitaji ya pesa huwa ni kidogo sawa na ilivyo kwa familia changa ya watu wawili. Hila kadri umri unavyozidi kuongezeka au kadri familia inavyozidi kupanuka ndivyo na mahitaji ya pesa yanaongezeka. Katika jamii zetu tumezoea kuona mwezi Januari na Julai katika kila mwaka inakuwa ni miongoni mwa miezi ambayo huwa inahusisha mahitaji makubwa ya pesa kwa mtu mmoja mmoja au familia. Hali hii inatokana na ukweli kwamba miezi hii inahusisha ulipaji ada za wanafunzi pamoja kodi za pango la nyumba. Hata hivyo, mwezi Januari unakuwa na mwezi wenye vilio vikubwa vya upungufu wa pesa kwa kuwa wengi wanakuwa na matumizi makubwa nje ya bajeti katika sherehe za mwisho wa mwaka.

Je ni ipi tiba halisi ya kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya pesa? Katika jamii, watu wengi huwa wanatumia mbinu ya kubana matumizi kama tiba ya kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya pesa. Hata hivyo, mbinu hii huwa haimpi mhusika Uhuru wa kufurahia maisha kutokana na jinsi anavyojibana katika mfumo mpya wa maisha. Matokeo ya mbinu hiyo ni kuongezeka kwa msongo wa mawazo kadri mahitaji ya pesa yanavyoongezeka.

Kumbe, tiba halisi ya kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya pesa siyo kupunguza matumizi bali ni kuongeza mifereji mipya ya mapato. Wengi katika jamii wanaendelea kuteseka kwa kuwa wanaishi kwa kutegemea chanzo kimoja cha pesa bila kugundua kuwa chanzo hicho kinaelemewa kutokana na ongezeko la mahitaji ya pesa. Kama ni mshahara, ukweli ni kwamba kasi ya ongezeko la mahitaji ya pesa haiwezi kuendena na kasi ya ongezeko la mshahara toka kwa mwajiri wako. Hata kwenye biashara, tunashuhudia biashara nyingi zinakufa kutokana na kuzidiwa mahitaji ya pesa yanayowakabili wamiliki wa biashara hizo. Tafsiri yake ni kwamba kasi ya ongezeko la mahitaji ya pesa inakuwa kubwa ikilinganishwa na faida inayotengenezwa kwenye biashara.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza ni kawaida mahitaji ya pesa kuongezeka kadri umri unavyoongezeka. Baada ya kutoka kwenye maisha ya utegemezi wa wazazi, mahitaji ya pesa yanaongezeka kwa kasi sana ikiwa hakuna mkakati wa kuongeza vyanzo vipya vya mapato. Badala ya kupunguza matumizi kwa kujibana kama mbinu ya kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya pesa unatakiwa kuongeza mifereji ya kipato ili kuendana na ukuaji wa mahitaji ya pesa. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(