NENO LA LEO (JANUARI 25, 2021): JE UNAYAFAHAMU HAYA KUHUSU MALEZI YA MWANAO?
Habari ya leo rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia
ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku ya kwanza ya juma ambayo ni matarajio yangu kuwa
umeianza siku kwa kutekeleza yale ambayo yanakupa muunganiko wa matokeo kila
siku. Furaha ya mwanadamu inapatikana pale ambapo anajivunia mafanikio ambayo
ni zao la kazi halali kupitia majukumu yake ya kila siku. Hakikisha katika siku
hii ya leo umetumia kazi yako kueongeza kilele cha furaha yako katika maisha ya
kila siku.
Katika
Makala maalumu ya leo nitakushirikisha vitu muhimu unavyotakiwa kuzingatia
ikiwa wewe ni mzazi au mlezi au unategemea kuwa na majukumu hayo katika kipindi
cha uhai wako hapa Duniani. Kwanza kabisa kama mzazi/mlezi unatakiwa kutambua
kuwa tupo kwenye kipindi cha mapinduzi ya teknolojia ya habari. Kipindi hiki kinakutaka
mzazi/mlezi uwe macho kuliko vipindi vilivyotangulia kutokana na ukweli kwamba
Dunia yote imefunuliwa kwenye macho ya Watoto wako. Ikiwa utashindwa kutimiza
wajibu wako, Dunia itawafundisha wanao tabia ambazo zitakusonenesha katika kipindi
chote cha uhai wako.
Ni katika kipindi hiki cha mapinduzi ya teknolojia ya habari mzazi/mlezi unatakiwa kufahamu kuwa mtoto anahitaji kufundishwa kujifunza vitu vingi zaidi ya kile alichosomea. Hivyo, ukiwa mzazi/mlezi unatakiwa kufahamu kuwa wewe ni walimu namba moja kwa mwanao. Mzazi/mlezi unapaswa kutambua kuwa elimu inayotolewa haijitoshelezi kwa ajili ya kufanikisha maisha ya mwanao. Hivyo, mtoto anahitaji kufundishwa misingi muhimu ya maisha ya mafanikio ikiwa ni pamoja na elimu ya fedha ambayo haifundishwi kwenye mitaala ya shule zetu.
Je mtoto anapotezea wapi uwezo/akili ya kuzaliwa? Watoto wote wanazaliwa wakiwa tajiri na akili nyingi. Kadri mtoto anavyozidi kukua ndivyo anapoteza uwezo wake na akili ikilinganishwa na enzi za kuzaliwa kwake. Mara Watoto wengi wanapoteza uwezo wao kutokana na mazingira wanayokulia. Mazingira hayo yanahusisha kauli wanazoambaiwa na wazazi/walezi, walimu, ndugu na jamii inayowazunguka.
Je mzazi/mlezi unalinda vipi uwezo wa mwanao katika kufikiri na kununi? Katika ukuaji mtoto anatakiwa afundishwe umuhimu wa kufahamu kuwa katika maisha hakuna jibu sahihi. Jibu la HAPANA au NDIYO yote ni majibu sahihi ikitegemewa na namna muhusika anavyosimama kutetea jibu lake. Hii ni elimu ambayo mtoto ataipata kwa wazazi pekee kwani elimu ya sasa inalenga kwenye kutambua watoto wanaoweza kutoa majibu sahihi na kuwafanya wengine waonekana hawana uwezo.
Mtoto anahitaji kufundishwa kwa vitendo. Elimu ya sasa inajikita zaidi kwenye nadharia kuliko vitendo, elimu hii imepelekea kuzalisha vijana wengi ambao darasani wanafaulu kwa viwango vya hali ya juu japo katika maisha mafanikio yao ni ya kawaida. Hii ni kutokana na ukweli kwamba elimu ya sasa inazalisha watu ambao wanaweza kuelezea kwa kina mbinu mbalimbali kwa nadharia wakati hawajawahi kutumia mbinu husika katika maisha yao. Wajibu wako kama mzazi/mlezi ni kumfandisha mwanao kupitia shughuli unazofanya. Kama unamiliki biashara hakikisha wanao wanajua misingi ya kusimamia na kuendesha biashara husika.
Je mzazi/mlezi unamuandaaje mwanao kwenye elimu isiyokuwa na mwisho? Mtoto anatakiwa kutambua kuwa elimu ya kweli inaanzia pale
anapomaliza masomo yake. Mtoto anahitaji kuandaliwa kwa ajili ya kuendelea
kujifunza katika kipindi chote cha maisha yake. Hii ni kutokana na ukweli
kwamba watoto wengi wanapomaliza masomo yao wanaona kuwa ndo mwisho wa kujifunza.
Hali hii imepelekea jamii kuendelea kuwa na watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri
na kungamua mambo kwa kuwa nadhari walizosoma shuleni hazi nafasi katika maisha
ya kila siku.
Mwisho,
katika neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa tupo jinsi tulivyo kutokana na
athari ya malezi na makuzi tuliyopewa kutoka kwa wazazi/walezi. Hata hivyo, kwa
sasa tumekabidhiwa jukumu la kuhakikisha tunawalea Watoto wetu katika misingi
ambayo itawafanya wajivunie kuwa na wazazi/walezi bora katika kipindi chote cha
uhai wao. Yapo mengi ambayo tumeyakosa kutoka kwa wazazi/walezi wetu hila sasa
wajibu wetu ni kuhakikisha Watoto wetu wanapata kile ambacho tulikosa. Zaidi ya
yote tuna wajibu wa kuwalinda Watoto wet una makucha ya Dunia. Kumbuka, mbegu
ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii
niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika
Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya
pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka
kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu
inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
BORN
TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano:
0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua
pepe: fikrazakitajiri@gmail.com