NENO LA LEO (JANUARI 19, 2021): JE WAJUA KUWA PESA HAINUNUI FURAHA?

Habari ya asubuhi mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza jitihada zinazolenga kukamilisha ushindi katika siku hii ya leo. Ni siku nyingine tunapata nafasi ya kuwa bora zaidi kuliko ilivyokuwa jana kupitia kwenye thamani tunayotoa katika majukumu yetu ya siku ya leo.

 Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA

Katika jamii tunayoishi, tumeshuhudia asilimia kubwa ya watu ambao mara nyingi huwa wanachanganya uhusiano uliopo kati ya pesa na furaha halisi katika maisha. Katika neno la tafakari ya leo nataka nikukumbushe kuwa kadri unavyoweka malengo ya kuboresha maisha yako hasa katika sekta ya uchumi huna budi kufahamu kuwa kamwe pesa haiwezi kununua furaha.

Wote ni mashahidi kuwa pesa kidogo zinaweza kukufanya uwe na maisha ya huzuni hasa pale mahitaji ya pesa yanapozidi uwezo wako wa kifedha. Kwa tafsiri hii ni wazi kwamba pesa ndogo inaweza kukusababishia uwe na msongo wa mawazo au maisha ya huzuni. Hata hivyo, pamoja na kwamba pesa ndogo inaweza kukusababishia msongo wa mawazo; wote ni mashahidi kuwa wapo matajiri wengi ambao wanaishi maisha ya huzuni pamoja na kwamba wana pesa nyingi kwa ajili ya kukidhi kila hitaji la maisha yao.

Kwa tafsiri hii tunajifunza kuwa unaweza kuwa na pesa nyingi lakini maisha yako yakawa na msongo wa mawazo au huzuni ya moyo kuliko hata masikini. Kumbe, tunachojifunza kwa ujumla wake ni kwamba masikini au tajiri wote wanaweza kuwa na maisha ya furaha au huzuni bila kujali kiwango cha pesa wanachomiliki. Baada ya kugundua uhusiano uliopo kati ya fedha na furaha unatakiwa ufahamu kwamba furaha ya kweli inaanzia ndani mwako pasipo kujali kipato ulichonacho. Hii ni kutokana na ukweli kwamba sio pesa au vitu unavyomiliki vitakufanya uwe na furaha bali furaha unaitengeneza mwenyewe.

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa hatima ya maisha yako ipo mikononi mwako, na ndivyo ilivyo na kwenye maisha yenye furaha. Kila aina ya maisha unayotamani kuwa nayo katika uhai wako ni lazima uyatengeneze ndani mwako (nafsi na roho yako). Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(