NENO LA LEO (JANUARI 04, 2021): HAPA NDIPO WAAJIRIWA WANAKOSEA KATIKA MIRADI YAO.
Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni wakati mwingine tena tumepata kibali cha kuwa hai. Kitu pekee ambacho tuna deni kutokana na uhai huu ni jinsi tutakavyotumia siku hii ya leo kukamilisha majukumu yaliyopo mbele yetu. Wajibu uliopo mbele yetu ni kuhakikisha tunatumia siku hii kutoa thamani kwa jamii inayotunguka na viumbe vyote kwa ujumla.
Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya kupata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, tafadhali JIUNGE SASA.
Katika neno la tafakari ya leo tutaona jinsi ambavyo waajiriwa wengi wamekuwa wakipoteza hela nyingi katika uanzishaji na uendeshaji miradi. Kwa waajiriwa inafahamika kabisa kuwa asilimia kubwa mishahara yao haiwezi kutosheleza mahitaji yote ya msingi. Ili wawe salama kifedha wengi wamekuwa wakianzisha miradi mbalimbali kama sehemu ya kujiongezea kipato. Hata hivyo, kwa wengi miradi hii imekuwa sehemu ya kupoteza fedha zaidi kutokana na sababu zifuatazo:-
Kweli #1: Usimamizi mbovu. Waajiriwa wengi kutokana na kubanwa na majukumu yao ya kazi ambapo kuna nyakati wanalazimika kisafiri nje ya sehemu miradi yao ilipo wanajikuta miradi ilishaharibika kuliko ilivyotarajiwa. Mfano, kawaida kwa Waajiriwa kujihusisha kwenye miradi ya kilimo na ufugaji. Miradi hii yote ufanikiwe kupata faida inahitaji usimamizi wa karibu was mhusika. Siyo miradi ya kutegemea kupewa taarifa za mtu aliyepo kwenye mradi na ukaamini taarifa hizo. Hali ni tofauti kwa Waajiriwa kwa kuwa wengi wao wanaendesha miradi ya kilimo na ufugaji kwa rimoti. Matokeo yake inapofikia wakati wa mavuno wanajikuta wamepoteza hela nyingi kuliko ilivyotarajiwa.
Kweli #2: Hakuna taarifa za maandishi za mradi husika. Hela inayoingia na hela inayotoka hakuna taarifa zake sahihi. Wengi wanaendelea kuweka hela kwenye miradi husika kutoka katika vyanzo vingine bila kuandika sehemu yoyote. Matokeo yake kuna miradi mingi ambayo inaendeshwa kwa hasara hila kwa kuwa hakuna maandishi wengi wanahisi kuwa miradi hiyo inazalisha faida.
Kweli #3: Kutumia ushauri ambao haujafanyiwa uchunguzi. Wengi wanakurupuka katika uanzishaji wa miradi kwa maana hili neno sahihi ambalo nawezakutumia ili nieleweke kwa urahisi. Waajiriwa wengi wanaanzisha miradi yao kwa kutumia taarifa za kusikia au ushauri wa juu juu. Mtu akisikia kilimo cha tikiti kinalipa ghafla anakimbilia kulima tikiti, akisikia kuna faida katika ufugaji kuku ghafla nae anakimbilia huko au akisikia nyumba za kupanga zinalipa ghafla nae anazama. Kwa ujumla Waajiriwa wengi wanaanzisha miradi yao kwa kuigaina.
Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza baadhi ya mapungufu yaliyopo katika uanzishaji na uendeshaji wa miradi kwa Waajiriwa. Kweli hizo tatu nilizoeleza hapo juu zinaweza kuwa zinamgusa yeyote kati yetu hivyo ni suala la kutazama upya kama mradi wako unazalisha faida au unaedelea kuwa sehemu ya kupoteza fedha zako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: 1. Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾
https://fikrazakitajiri.blogspot.com/2020/01/orodha-ya-vitabu-nilivyosoma-katika.html?m=1.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
onclick='window.open(