HUYU NIDYE MPINZANI WAKO HALISI KATIKA KUISHI MALENGO YA 2021.

NENO LA LEO (JANUARI 3, 2021): HUYU NIDYE MPINZANI WAKO HALISI KATIKA KUISHI MALENGO YA 2021.

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni nyingine ambapo tunabahatika kuongeza siku za uhai wetu katika safari ya maisha yetu hapa Duniani. Wajibu wetu ni ule ule wa kuhakikisha kila siku tunatoa thamani ili kupitia thamani hiyo tupate kuifanya Dunia kuwa mahali pazuri pa kuishi kwa viumbe vyote.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.    

Naamini kila mmoja wetu amejiwekea malengo kwa ajili ya kuhakikisha mwaka 2021 unakuwa miongoni mwa miaka ambayo imefanikisha ukuaji katika kila sekta ya maisha yetu. Ni jambo la kheri kuwa na malengo japo changamoto kubwa iliyopo mbele yetu ni kuona tunayaishi malengo hayo katika maisha yetu ya kila siku.

Ninaposema kuishi malengo katika maisha yako ya kila siku namaanisha unatakiwa kutafsiri malengo yako katika vitendo vya kila siku. Hatua hii inahusisha kuvunja vunja malengo kwenye kazi/shughuli za utekelezaji ambapo shughuli hizo zinatakiwa kuwa sehemu ya ratiba yako katika siku husika. Pia, shughuli hizo zinatakiwa kujidhihirisha katika bajeti yako ya kila siku ikiwa umejiwekea malengo yanahusisha ukuaji wa kiuchumi.

Ukitazama kwa undani, utekelezaji wa malengo unahusisha kubadilisha mfumo mzima wa maisha yako ikiwa ndo mwaka wako wa kwanza kufanya hivyo. Hatua hii inakutaka kubadilisha baadhi ya tabia ambazo zinaenda kinyume na malengo yako. Hapo ndipo mpinzani wako halisi anakoanza kujitokeza.

Je mpinzani wako halisi ni yupi katika maisha ya kila siku? Mpinzani halisi wa kutimiza malengo yako ni nafsi yako mwenyewe. Hivyo, katika maisha ya kila siku upinzani wenye madhara makubwa kwa malengo yetu ni ule upinzani wa kutoka ndani ikilinganishwa na upinzani wa kutoka nje. Katika maisha ya kila siku tunaweka jititihada za kupambana na upinzani wa kutoka nje bila kutambua kuwa upinzani wa nje msingi wake mkubwa ni upinzani wa ndani.

Jiulize ni mara ngapi unaweka ratiba ya siku lakini unashindwa kuitimiza? Jiulize mara ngapi unasema unataka kudhibiti matumizi ya pesa yasiyo ya msingi lakini unajikuta unanunua bidhaa au huduma ambazo zinaenda kinyume na kanuni za udhibiti wa pesa? Jiulize ni mara ngapi umedhamiria kuwa mbali na makundi ya watu ambayo hayana tija kwako lakini ghafla unajikuta umeshawishika kuendelea na makundi hayo? Jiulize ni tabia zipi hatarishi kwa afya ya mwili, roho na uchumi wako ambazo umedhamiria kuziacha lakini ghafla unajikuta unaendelea na tabia hizo?

Ikiwa unahitaji mwaka 2021 uwe wa tofauti ni lazima uanze kupambana na upinzani wa kutoka ndani ikilinganishwa na upinzani wa nje. Mara nyingi kabla ya kufanya jambo lolote huwa kuna mawasiliano ya ndani kwa ndani (roho na nafsi). Mara nyingi huwa roho inakuuliza kwanza maswali ambayo yanatakuta kujiridhisha dhidi ya hatua ambazo unakusudia kuzichukua ikiwa hatua hizo ni za lazima. Mawasiliano hayo ni muhimu kwa ajili ya kukabiliana na upinzani wa kutoka ndani. Kwa maana, katika mawasiliano hayo ndipo utakiwa kurudi kwenye muunganiko halisi wa malengo dhidi ya hatua ambazo unakusudia kuchukua kwa wakati huo. Pia, katika siku unatakiwa kutenda muda maalum wa tafakari kwa ajili ya kupata muunganiko wa roho na mwili. Katika muda huo wa tafakari unapata kurudi kwenye muunganiko wa malengo yako ikilinganishwa na hatua unazochukua kila siku. 

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa mpinzani halisi wa utekelezaji wa malengo yetu ya kila siku yupo ndani ya nafsi zetu. Hata hivyo, bila kujua mara nyingi tumekuwa tukitafuta upinzani wa kutoka nje na mwisho wake tunajikuta katika hali ya kutotimiza malengo tunayojiwekea. Anza kwa kupambana na mpinzani wa ndani kabla ya kutafuta upinzani wa nje. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com


onclick='window.open(