MEMA NA MABAYA NI SEHEMU YA MAISHA: KWA NINI UNAPOTEZA MUDA KWA HOFU?

NENO LA LEO (JANUARI 28, 2021): MEMA NA MABAYA NI SEHEMU YA MAISHA: KWA NINI UNAPOTEZA MUDA KWA HOFU?

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni ukurasa mpya katika kitabu cha uhai wetu hapa Duniani. Ni katika ukurasa huu wa wazi ambao wote tunaalikwa kuendeleza yenye thamani ili yapate kuunda kitabu cha maisha yetu hapa Duniani. Kila siku ni wito kwa kila mmoja wetu kuhakikisha anatekeleza majukumu ya msingi ambayo kwa ujumla wake yanakamilisha kusudi kuu la maisha yake hapa Duniani.

 Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA 

Katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakukumbusha umuhimu wa kutambua kuwa kipindi cha mwanadamu hapa Duniani kinapitia katika nyakati za neema na nyakati ngumu. Hakuna ajuaye kuwa kesho yake ana uhakika wa kuepukana na ubaya au nyakati ngumu katika maisha yake. Vivyo hivyo, hakuna mwenye uhakika asilimia mia moja kuwa maisha yake yatakuwa na nyakati bora. Zipo nyakati ngumu katika maisha yetu ambazo tunajisababishia wenyewe kwa kujua au kutokujua na zipo nyakati ambazo zinasababishwa na majanga ya asili.

Ni ukweli kwamba kupitia matendo yetu ya kila siku tunaweza kupunguza uwezekano (chances) wa kupatwa matukio yasiyo rafiki katika maisha yetu lakini hiyo siyo tiketi ya kwamba tuna uwezo wa kudhibiti kabisa nyakati hizo zisitokee kwetu. Mfano, katika ajali hakuna ajuaye kuwa kesho itatokea ajali ya bodaboda, gari, treni, meli au ndege. Pamoja na kutokujua siyo kisingizio kuwa watu wasisafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Pia, hakuna anayejua kuwa kesho atapatwa na majanga ya asili kama athari za upepo mkali, mafuriko, ukame au tetemeko la ardhi. Hata hivyo, hiyo siyo tiketi kwa kila mmoja wetu kutulia na kuacha kujishughulisha kwa kuogopa athari za majanga hayo ya asili kwenye shughuli za uzalishaji, makazi au uhai wa mwanadamu.

Kila mmoja wetu katika maisha yake ya akila siku anafahamu namna ambayo amekuwa akipoteza muda kutokana hofu juu ya matukio ambayo haitabiriki yatatokea lini. Wapo watu ambao wanaogopa kuwekeza kwa kigezo cha kuogopa kupoteza pesa zao. Wapo watu ambao wanashindwa kuishi maisha yao kwa kigezo cha kuogopa kufukuzwa kazi. Wapo watu ambao wanashindwa kufanya uwekezaji wa muda mrefu kwa kigezo tu cha kuwa hawana uhakika wa kuishi kwa kipindi cha miaka kadhaa. Hofu kwa matukio ambayo yapo nje ya uwezo wetu wa kuyadhibiti inatawala maisha yetu kila siku. Matokeo yake tunashindwa kuishi maisha yetu kwa ukamilifu kutokana na hofu.

Kwa ujumla, wasiwasi ni zao la hofu. Wasiwasi juu ya matukio au hali ambazo ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya kwako katika siku za baadae hupelekea kuharibu utekelezaji wa mipango kwa ufasaha. Kuendelea kuwa na wasiwasi kwenye hali au tukio husika inapelekea kupoteza muda kutokana na kukosa maamuzi ya haraka kwenye tukio au hali iliyopo mbele yako. Hivyo, kuwa na wasiwasi juu ya siku zijazo hakukusaidia kupata suluhisho bora la shida iliyopo mbele yako na badala yake inapelekea katika hali ya kupingana kifikra juu ya kipi kifanyike bila kupatwa na mabaya.  Hali hii inapelekea kupoteza mawazo ya busara ambayo yangefaa kukupa maamuzi sahihi kulingana na wakati husika.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI  

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumeona kuwa mema au mabaya ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Hakuna anayeweza kujihakikishia maisha yenye matukio mema pekee kwa kuepuka mabaya. Kubwa tunachotakiwa kufanya ni kuepuka kupoteza muda kutokana na kushindwa kuchukua maamuzi kwa wakati sahihi kutokana na kuogopa kupatwa na mabaya. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

 πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(