Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo USHAURI. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo USHAURI. Onyesha machapisho yote

[MUHIMU] Fahamu Sehemu Muhimu Ya Mwili Ambayo Unaisahau Kila Mara.

NENO LA SIKU_FEBRUARI 8/2022: Muhimu! Fahamu Sehemu Muhimu Ya Mwili Ambayo Unaisahau Kila Mara.


📌Unaendeleaje rafiki na mfuatiliaji wa masomo ya mtandao wa Fikra za Kitajiri! Ni mategemeo yangu kuwa umeianza siku vyema kwa kutimiza majukumu yako ya msingi huku ukizingatia maslahi mapana ya nafsi yako, jamii kwa ujumla wake na mazingira yanayokuzunguka.


Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA

📌Karibu tena katika makala ya leo upate chakula cha ubongo ili akili yako ipate kuendelea kuwa hai. Katika makala ya leo nitakushirikisha moja ya kiungo muhimu katika mwili wako ambacho kinahitaji umakini wako sawa unavyoweka malengo na mikakati muhimu kwa ajili ya sehemu nyingine za mwili na kila sekta ya maisha yako. 


📌Mwili wa mwanadamu unaundwa na seli mbalimbali ambazo kwa pamoja zinaunda viungo vya mwili kama vile mifupa, nyama, damu na ubongo. Katika mtazamo wa kemia, mwili wako unaundwa na maji na muunganiko wa elementi za kaboni ambazo hujumuisha mafuta, protini, wanga na asidi. Hata hivyo, pamoja na kwamba miili ya wanadamu inaundwa vitu vya aina moja, kinachopelekea wanadamu wawe na maumbo yenye mwonekano tofauti ni taarifa za kijeni (genetic information), mazingira ya nje na tabia ambazo zinaweza kubadilisha mwonekano wa mwili hasa katika kufanya kazi vizuri kwa ajili ya maendeleo ya mhusika.


📌Katika mwonekano wa nje, maumbile ya mwanadamu yanajumuisha sehemu tano za msingi ambazo ni kichwa, shingo, kifua, mikono na miguu. Makala hii itajikita kwenye kuelezea jinsi ambavyo sehemu ya ndani ya kichwa cha mwanadamu ambayo imekuwa si kipaumbele kwa wengi pindi wanapojiwekea malengo muhimu ya maisha. Kwa muonekano, sehemu ya kichwa cha mwanadamu ni ndogo ikilinganishwa na sehemu nyingine za mwili wa mwanadamu japo sehemu hii ndiyo inabeba kiungo muhimu katika suala zima la kuratibu sehemu zote za mwili. Sehemu ya juu ya kichwa hufunika seli laini ambazo muunganiko wake unaunda kiungo cha mwanadamu kijulikanacho kama ubongo.


📌Ubongo wa mwanadamu ni kiini tete au laini chenye mfumo wa nevu za mwanadamu ambapo kwa kuungana na uti wa mgongo hufanikisha kazi zote za mfumo wa fahamu na utambuzi. Kiungo hiki humwezesha mwanadamu kukamilisha kazi zote za mwili kama vile mijongeo, vitendo vya mwili, kuongea (lugha), kuhisi na kuitikia vichocheo sambamba na kutunza kumbukumbu. Kwa kifupi, ubongo ni chanzo na hazina ya akili ya mwanadamu.


📌Pamoja na umuhimu wa ubongo kwa mwanadamu, kiungo hiki kinasahaurika kwa asilimia kubwa ya watu pindi wanapojiwekea malengo muhimu ya maisha. Sawa na ilivyo kwa mwili, ubongo au akili ya mwanadamu inahitaji kutunzwa na kuendelezwa. Mara nyingi watu wanazama kwenye kuweka malengo ya kufanikisha au kudumisha upatikanaji wa chakula, afya bora, kazi au uchumi lakini wanasahau jinsi gani wanatakiwa kulisha ubongo wao.


📌Kama ilivyo muhimu katika kuamua ni nini unapaswa kula kwa ajili ya kuboresha afya ya mwili wako, ni muhimu pia kuilisha akili yako na vitu muhimu ambavyo vinaiwezesha kukua na kuendelea. Kitu cha kwanza ambacho lazima utambue ni kwamba akili yako ndiyo msingi na injini ya kuwezesha maendeleo katika kila sekta ya maisha yako. Hivyo, kuipenda akilli yako ni kujipenda mwenyewe, wengine wanaokuzunguka na mazingira unayoishi. Tunaweza kutafsiri kwa maneno mengine kuwa, jinsi unavyoipenda akili yako angalau kidogo, ndivyo upendo unavyozidi kuenea kwa wale walio karibu nawe. 


📌Upendo huu wa ndani utaendelea kukua ikiwa utaendelea kuijali akili yako kwa kuhakikisha inachuja na kufyonza vitu vya msingi kati ya mengi yanayokuzunguka. Hii ni sawa na unavyochagua vyakula sahihi kwa ajili ya mwili wako badala ya kula pasipo kuzingatia mfumo maalumu wa chakula. Unavyolisha akili yako na maarifa sahihi ndivyo akili inakua na kujiendeleza kwa kukuwezesha kupata ufunuo wa uwezo wako halisi katika kila sekta ya maisha. Hata hivyo, kadri ujinga unavyoijaza akili yako, ndivyo inavyozidi kudhoofika. Mfano, ikiwa akili unaijaza na vitu vya giza, hofu, chuki, hasira, choyo, wivu, filamu zisizo na maana, vibweka au vibonzo vya mtandaoni na mambo mengine ya hovyo; ni wazi kuwa akili yako haitakuwa na ubunifu au mawazo chanya yenye manufaa kwako, jamii na mazingira kwa ujumla. 


📌Kama huna malengo ya kuendeleza akili yako ni dhahiri kuwa unainyima akili yako kitu cha muhimu sana. Ukweli ni kwamba akili yenye maarifa sahihi ni hazina yenye faida maana unaweza kupoteza kazi yako, unaweza kupoteza watu na vitu vyote, lakini huwezi kupoteza maarifa na ujuzi uliojifunza na kuhifadhiwa  akilini mwako. Akili ni sehemu nyingine ya maisha yako ambayo kuanzia sasa unatakiwa kutumia pesa, nguvu na muda kwa ajili ya uwekezaji unaolenga kuikuza na kuiendeleza. 


📌Je! Mwaka huu umelenga kusoma vitabu vingapi? Umepanga kusikiliza programu ngapi au semina ngapi zinazolenga kujifunza maarifa mapya? Kitu kimoja ambacho unatakiwa kufahamu ni kwamba "Maarifa ni kama chakula cha ubongo, huwezi kula mara moja na kusema yatosha. Unatakiwa kuulisha ubongo wako na maarifa sahihi mara kwa mara." Fikiria kama kila siku ungekuwa na mpango wa kujifunza jambo moja jipya, katika mwaka mmoja ungejifunza mangapi? James Allen katika kitabu chake cha "As A Man Thinketh" anasema “Mwanadamu ni, na vile anavyofikiri, ndivyo alivyo”. Mtazamo wa maneno haya kuhusu mwanadamu jinsi alivyo na jinsi navyofikiri unatupeleka katika kufikiria umuhimu wa chakula cha akili yenye uwanda mpana husio na ukomo wa kujifunza.


📌Maisha si lolote zaidi ya kuishi, kuchunguza, kupata uzoefu mpya, kujifunza na kushirikisha wengine kama ushauri au masomo kwa walio tayari kupokea. Kushirikisha maarifa muhimu ni moja ya zawadi kuu ambayo mtu anaweza kutoa kwa wengine. Hamu yangu kubwa ni kuishi maisha ya kujifunza kila mara na kuhakikisha nashirikisha wanafunzi ambao kwa hiari yao wapo tayari kujifunza. Hapa ninamaanisha kuwa sio kila mtu anataka kujifunza au kuongeza maarifa. Unaweza kuchagua kupoteza muda wako kutazama televisheni, kufuatilia mambo ya hovyo kwenye mitandao ya kijamii, au kujumuika na marafiki zako, au kutumia muda huo kwa ajili ya kujifunza maarifa sahihi. Unaweza kusoma vitabu kuhusiana na fani yako, biashara, kiroho au vitabu vinavyosaidia katika ukuaji wa jumla wa nafsi yako. 


📌Sina lengo la kukuchosha! Hivyo, nihitimishe kwa kusema kuwa katika mwendelezo wa kukushirikisha maarifa sahihi nimekuandalia kitabu cha MAISHA YENYE THAMANI ambacho ni zawadi kwa yeyote mwenye hitaji la kuacha alama ya maisha. Zawadi hii ni kwa ajili ya kuhakikisha unaamsha akili yako ili isije kudhoofu na mwisho wake ikafa. Mtu mwenye akili mfu ni miongoni mwa watu ambao tunasema wanatembea lakini wamekufa!  Uzoefu unaoesha watu waliofanikiwa kwenye kila sekta ya maisha ni wale ambao wamewekeza vya kutosha kwa ajili ya kujifunza kuhusu sekta husika. Anza sasa kuilisha akili yako na maarifa sahihi ili upate kutambua uwezo wako halisi. Ikiwa akili inakua kwa kile inachokula, Je mwezi uliopita umeilisha akili yako ni nini? Je! Mwaka huu umepanga kusoma vitabu vingapi na hadi sasa umeshaanza kusoma hata kimoja? 

 

PATA NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI KUJIFUNZA ZAIDI KUHUSU MISINGI YA MAISHA BORA HAPA DUNIANI

Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.


Kwa Asili Tumeumbwa Kuwa Watafutaji! Kwa Nini Tumepoteza Wajibu Huo?

 NENO LA SIKU_JANUARI 27/2022: Kwa Asili Tumeumbwa Kuwa Watafutaji! Kwa Nini Tumepoteza Wajibu Huo?

📝Habari ya rafiki yangu na mfuatiliaji wa masomo ya mtandao wa Fikra za Kitajiri. Ni wakati mwingine napata nafasi ya kukushirikisha machache kwa ajili ya ukombozi wa maisha yetu. 


Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA


📝Lengo la masomo haya ni kugusa maisha ya wengi ili jamii ipate kutambua kuwa ulimwengu unatudai vitu vya ziada kupitia maisha haya mafupi. Ikiwa wote tutambua Ulimwengu unataka nini kutoka kwetu, maisha kwa viumbe wote yatakuwa endelevu na kwa kufanya hivyo tutapunguza mateso ya kila aina katika maisha yetu.


📝Toka siku ambayo kila mmoja wetu aliumbwa, Ulimwengu ulianza kudai kitu cha ziada kutoka kwenye maisha yake na kitu hiko hauwezi kukilipa ikiwa hautambui thamani ya maisha yako ni ipi! Kumbe, hatua ya kwanza katika kutimiza deni unalodaiwa na Ulimwengu ni kutambua vitu muhimu vinavyoshikilia thamani ya maisha yako.


📝Katika hilo la kudaiwa na Ulimwengu, hatuna budi kutambua kuwa: “Kwa Asili Wote Tumeumbwa Kuwa Watafutaji.” Kwa maana, tumeumbwa kwa ajili ya kuutafuta “ukweli” ambao unahusisha kutafuta majibu ya maswili mengi kama vile: Ni kipi chanzo cha maisha yetu? Kwa nini tunaishi katika ulimwengu huu? Je! Sisi ni nani na maisha yetu ni kwa ajili ya nini? Je! Tunapaswa kufanya nini kwa ajili ya kuishi maisha ambayo yataacha alama vizazi na vizazi?


📝Hata hivyo, pamoja na kwamba kwa asili tumeumbwa kuwa watafutaji, tumepoteza asili kwa kujua au kutokujua. Mwanamahesabu na Mwanafalsafa wa Kifaransa Paschal Braise ndipo aliwaweka watu katika makundi mawili: Watafutaji (Seekers) na Wasio-watafutaji (Non-seekers). 


📝Kundi la Watafutaji mara zote wanatamani zaidi kuongeza uzoefu wa maisha na kutumia uzoefu huo kwa faida ya ulimwengu na wao wenyewe. Mara nyingi, Watafutaji hutamani kutazama nyuma kwenye nyakati za maisha yao na kufarijika kutokana na matendo ambayo wameishi huku wakitazamia kuendelea kutoa michango zaidi kwa ulimwengu wa kesho. 


📝Kundi la Watafutaji huongozwa na msukumo halisi kutoridhika na kwa kufanya hivyo hujiona wana deni kubwa la kuendelea kutafuta zaidi. Watafutaji ndani mwao huwa wana "hekima angavu" ambayo uwaongoza kuona umuhimu wa kutafuta zaidi kwa faida ya watu wote. Hekima hii angavu mara zote inalia ndani mwao kwa ajili ya kufungua njia mpya za kupunguza mateso kwa wanadamu na viumbe wote.


📝Mfalme Sulemani, mtafutaji na mwandishi wa kitabu cha Mhubiri katika Biblia Takatifu, aliona hekima hii angavu kama zawadi kuu na mzigo mkubwa. Aliiona hekima hii kama hamasa ya kuishi maisha yanayojikita katika kupata wema halisi na yenye thamani ya kweli ambayo inadumu hata baada ya ukomo wa maisha. 


📝Kwa kutumia hekima hiyo, Mfalme Sulemani alifanikiwa kuishi maisha yenye kila aina ya mafanikio. Hakuna mtu aliyefanikiwa zaidi katika maisha ya dunia hii kuliko Mfalme Sulemani. Alikuwa tajiri kupita kiasi. Alikuwa mfalme mwenye nguvu zaidi wa siku zake. Alijenga majengo makubwa ya usanifu, alipanda misitu, alilima bustani nzuri, alikuwa na mifugo wengi, dhahabu na kila aina ya utajiri. 


📝Mfalme Suleimani, alitumia utajiri wake mwingi kupata na kujionea starehe kuu zinazopatikana katika maisha haya—maisha ya anasa, mamlaka ya kijamii na kisiasa, anasa za kimwili za chakula, vinywaji, na ngono. Hata hivyo alikata kauli kwamba hiyo maisha yalikuwa sawa na “kufukuza upepo” tu ikilinganishwa na ukweli halisi wa kuishi maisha ya thamani aliyoyataka. 


📝Hilo ndilo fumbo kuu la maisha, fumbo ambalo watu katika kundi la watafutaji wanatakiwa kuliishi katika maisha yao ya kila siku. Ni kwa bahati mbaya kuwa Ulimwengu tunaoishi una watu wachache sana kwenye kundi la Watafutaji ikilinganishwa na wale ambao hawana la kupoteza yaani wale ambao asubuhi jua lichomoze na jioni jua lizame, kwao kila kitu katika maisha yao ni sawa tu.


📝Hata hivyo, watu wengi wapo kwenye kundi la Wasio-Watafutaji si kwa mapenzi yao bali kwa kuwa hawana msingi sahihi wa kutambua maisha yao si kwa ajili ya kutimiza matakwa yao tu bali faida ya Ulimwengu kwa ujumla.


📝Katika kuhakikisha nakuwa sehemu ya watu ambao wanaishi kwa ajili ya kuacha alama katika Ulimwengu huu, nimetumia kipindi cha maumivu kutokana na ajali niliyopata kuandika kitabu cha MAISHA YENYE THAMANI. Hiki ni kitabu ambacho kinaleta nuru palipo na giza. Hivyo, ni kitabu muhimu kwa ajili ya kupunguza idadi ya watu katika kundi la Wasio-Watafutaji.


📝Ni kitabu ambacho kitakufanya utambue kuwa umepewa kuishi mara moja si kwa faida ya nafsi yako tu au ndugu zako bali faida ya watu wote katika Ulimwengu na viumbe vyote vilivyomo ndani yake.


📝Ni kitabu ambacho kitakufanya kila mara utimize wajibu wako vijana kwa wazee, wazazi, mtumishi wa umma, mfanyabiashara, mkulima au mfugaji, kiongozi wa Serikali, tasisi za dini au taasisi binafsi.


📝Nihitimishe makala hii kwa kusema kuwa: “Hatuwezi kufanikiwa kimaisha ikiwa hatujui misingi halisi ya kuumbwa kwetu sambamba na umuhimu wetu kuendelea kuishi.” Kupitia kitabu cha MAISHA YENYE THAMANI utafanuliwa vya kutosha ili uweze kurudi kwenye misingi ya asili kulingana na makusudi ya kuumbwa kwako.


Kitabu hiki kwa sasa kinapatikana kwa mfumo wa Nakala tete (soft copy) KWA BEI YA ZAWADI ya Tshs. 10,000/= badala ya Tshs. 20,000/=



Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.


Born to Win ~ Dream Big

 
Mwalimu Augustine Mathias 
Namba ya Simu:      +255 786 881 155
Mwanzilishi wa Mtandao wa 
fikrazakitajiri.blogspot.com
Barua pepe:  fikrazatajiri@gmail.com

Ujumbe wa Jonathan Lucas KWIYEGA Kuhusu Maudhui ya Kitabu Cha MAISHA YENYE THAMANI

📝Namshukuru sana rafiki yangu Augustine Mathias Mugenyi  kwa kunipa heshima ya kuwa mtu wa kwanza kusoma kitabu cha MAISHA YENYE THAMANI.

📝Kwa heshima hiyo, nimefanikiwa kusoma na kufuatilia kwa karibu sana maudhui ya kitabu hiki kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho.

📝Hakika ni kitabu muhimu sana kwa mwanadamu wa karne hii ya 21 kwa kuzingatia kuwa idadi ya watu inaongezeka na kusababisha kasi ya ongezeko la changamoto za maisha katika kila kona ya dunia.

📝Hii ni karne ambayo kuna kila sababu ya mwanadamu aliye hai kimwili na kiroho kufahamu kwa nini anaishi na wajibu wake ni upi kwake yeye mwenyewe, watu wengine, mazingira na kubwa zaidi kwa Muumba wake.

📝Kutambua wajibu huo ni muhimili na msingi muhimu wa kumfanya mwanadamu wa sasa aweze kuishi maisha kamili, tosherevu na yenye furaha. 


📝MAISHA YENYE THAMANI ni kitabu kinachotoa ufafanuzi wa kina kuhusu nyakati za maisha, mahitaji na hatua za ukuaji wa mwanadamu tangu kuzaliwa hadi kufa.

📝Katika kitabu hiki mwandishi ameelezea namna mwanadamu anavyoweza kujitambua na kuishi maisha yenye manufaa, furaha na amani. Ameelezea kwa kina namna ambavyo nadharia mbalimbali za maendeleo na ukuaji wa mwanadamu zinavyoathiri utu wa mwanadamu ambao ni msingi mkuu wa maadili katika jamii.

📝Pia, mwandishi ameainisha misingi ya imani na mapokeo ya dini mbalimbali jinsi inavyojibu swali kuu la msingi wa kitabu hiki, yaani majibu kuhusu “chanzo na maana ya maisha hapa duniani.”

📝Mwanadishi amefafanua falsafa mbalimbali za maisha na jinsi zinavyoeleza mahitaji na mchango wa nafsi ya mwanadamu anayeweza kujitambua na kutoa mchango wake katika jamii.

📝Aidha, Mwandishi ameleezea kwa kina namna sahihi ambayo kila mwanadamu anavyoweza kutumia falsafa hizo kufanyika mtu wa thamani hasa kuwa mtu mwenye maono, mwenye kuwekeza katika maeneo ya uwezo binafsi na kuzalisha huduma na bidhaa zinazobadili au kuleta mabadiliko chanya katika mazingira yake.

📝Vile vile, Mwandishi amefafanua umuhimu wa  busara na hekima ya uongozi katika kuongoza wengine ili kuleta mabadiliko chanya wakati mwanadamu anapoishi ndoto yake ama kutekeleza maono yake kwa furaha.

📝Mwandishi pia amegusia mambo yanayomfanya mwanadamu kupoteza thamani ya maisha, ambayo kwa sehemu kubwa yanatokea ndani ya nafsi ya mwanadamu na mazingira yake ya karibu.

📝Pia, katika kuhakikisha unapata mwongozo wote wa maisha yenye kuacha alama, Mwandishi amechambua changamoto zinazokabili dunia ya sasa na kuonyesha jinsi gani kila mmoja wetu anaweza kushiriki katika utatuzi wa changamoto hizo.

📝Kama hiyo haitoshi, Mwandishi ameelezea baadhi ya Sheria za Asili (Universal Laws) ambazo ni msingi wa ufanisi katika maisha.

📝Hakika haya ni mambo ambayo mtu akifanikiwa kuyafahamu na kujua namna ya kuyaishi, inamuiya rahisi kuishi maisha yenye thamani kubwa sana kwa kizazi chake na kuacha alama kwa vizazi vijavyo.


📝Kitabu hiki ni muhimu sana kusomwa na kila mtu hasa vijana na watu wazima. Ni kitabu muhimu sana kwa wazazi na walezi wa familia, viongozi wa taasisi na ngazi zote ili kujiongezea uwezo na ufahamu wa maisha.

📝Nimalizie kwa kusema kuwa, kitabu cha MAISHA YENYE THAMANI ni msaada wa kumfanya kila mtu apate kuishi maisha yenye mchango chanya katika jamii.

📝Ni maono yangu kuwa katika jamii iliyoshiba maudhui ya kitabu hiki kutakuwa na amani, furaha, uadilifu, utosherevu na maendeleo endelevu.

📝Mtu akisoma kitabu hiki kwa makini anapata shauku  na hamasa kubwa ya kuacha alama, kuhudumia jamii  na taifa lake kwa uadilifu akijua kwamba amepewa kuishi mara moja na kwamba kila siku ni muhimu kwake kukua, kuchanua  na kuonesha tunu iliyopo ndani mwake.

Jonathan Lucas Kwiyega

🖊️Mkurugenzi wa Shirika la Wanasihi wa Uhifadhi na Mandhari ya Nchi (LCMO); 

🖊️Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Chemichemi za Urejesho (SRM); na 

🖊️Mwandishi wa Vitabu zaidi ya Nane (8) vya Maarifa mbalimbali.


Kitabu hiki kwa sasa kinapatikana kwa mfumo wa Nakala tete (soft copy) kwa bei ya zawadi ya Tshs. 10,000/= badala ya Tshs. 20,000/=



Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.

BAADA YA KIMYA KIREFU, HII NDIYO ZAWADI YANGU KWAKO

Hii ndiyo zawadi ya kipekee ambayo nimekuandalia kwa ajili ya kuboresha maisha yako

⏩Hongera kwa jumapili iliyo bora. Ni matumaini yangu kuwa siku imemalizika salama. Waswahili wanasema "kimya kingi kina mshindo wake". 


Ni kweli kuwa toka tarehe 20 mwezi Aprili, 2020 hadi sasa nimepitia mawimbi ya maumivu ya mwili kutokana na ajali mbaya ambayo Mungu aliniepushia. 


Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA


Pamoja maumivu hayo ilifikia sehemu nikawa kwenye tafakari nzito ya kujiuliza ikiwa ningekufa katika ajali ile ningeacha alama gani katika mioyo ya watu wanaofuatilia masomo yangu na familia yangu kwa ujumla. 


Katika tafakari hiyo nikapata wazo la kuandika kitabu na ndipo nikaona nina deni la kuelimisha kuhusu jinsi gani kila mmoja wetu anaweza kuishi MAISHA YENYE THAMANI yaani maisha yanayoacha alama chanya katika Ulimwengu tunaoishi. 


Hata hivyo, pamoja na maamuzi hayo changamoto ilibakia ni kwa jinsi gani nitaweza kuandika kitabu hicho katika kipindi ambacho napitia maumivu makali kiasi ambacho siwezi kukaa muda mrefu. Pia, ni kipindi ambacho Kompyuta yangu mpakato ilikuwa na hitilafu. 


Yote hayo yakaonekana kama kikwazo cha kunizuia kukamilisha azma yangu ya kuandika kitabu ambacho ni msingi wa kuelimisha jamii hasa wafuatiliaji wa masomo yangu ili wapate kuishi maisha yenye kuacha alama baada ya ukomo wa maisha ya haya.


Ili kuondokana na changamoto hiyo ilinibidi nitafute kwenye mitandao jinsi gani naweza kuandika kitabu kupitia simu yangu ya mkononi. 


Majibu niliyopata yamewezesha leo hii niwe mwenye furaha kwa kufanikisha kuandika kitabu changu cha kwanza. Huwezi amini lakini huo ndiyo ukweli, nimefanikiwa kuandika kitabu chenye zaidi ya kurasa 150 kupitia simu yangu ya mkononi.


MAISHA YENYE THAMANI ni kitabu kinachotoa ufafanuzi wa kina kuhusu nyakati za maisha, mahitaji na hatua za ukuaji wa mwanadamu tangu kuzaliwa hadi kufa. 


Katika kitabu hiki nimeelezea namna mwanadamu anavyoweza kujitambua na kuishi maisha yenye manufaa, furaha na amani. 


Nimeelezea kwa kina namna ambavyo nadharia mbalimbali za maendeleo na ukuaji wa mwanadamu zinavyoathiri utu wa mwanadamu ambao ni msingi mkuu wa maadili katika jamii. 


Pia, katika kitabu hiki nimeainisha misingi ya imani na mapokeo ya dini mbalimbali jinsi inavyojibu swali kuu la msingi wa kitabu hiki, yaani majibu kuhusu “chanzo na maana ya maisha hapa duniani.”


Aidha, nimechambua changamoto zinazokabili dunia ya sasa na kuonyesha jinsi gani kila mmoja wetu anaweza kushiriki katika utatuzi wa changamoto hizo. 


Kama hiyo haitoshi,  nimeelezea baadhi ya Sheria za Asili (Universal Laws) ambazo ni msingi wa ufanisi katika maisha. 


Hakika maudhui ya kitabu hiki, mtu akifanikiwa kuyafahamu na kujua namna ya kuyaishi, inamuiya rahisi kuishi maisha yenye thamani kubwa sana kwa kizazi chake na kuacha alama kwa vizazi vijavyo.


Hakika hiki ni kitabu muhimu sana kwa wazazi na walezi wa familia, Vijana, viongozi wa taasisi na ngazi zote katika kujiongezea uwezo na ufahamu wa maisha.


Kitabu hiki kwa sasa kinapatikana kwa mfumo wa Nakala tete (soft copy) kwa bei ya zawadi ya Tshs. 10,000/= badala ya Tshs. 20,000/= 


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba  +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.