Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo AJIRA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo AJIRA. Onyesha machapisho yote

FUNGUO 5 ZA KUTHIBITISHSA KUWA UTAJIRI NI HAKI YAKO YA KUZALIWA.

       NENO LA LEO (APRILI 18, 2021): FUNGUO 5 ZA KUTHIBITISHSA KUWA UTAJIRI NI HAKI YAKO YA KUZALIWA.

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine tunapewa kibali cha uhai. Ni siku ambayo tunaalikwa kuendelea kuwa bora katika maisha yetu. Je! ubora wa maisha yetu unapatikana wapi? Hili ni swali ambalo kila siku asubuhi tunatakiwa kujiuliza kabla ya kuzama katika majukumu ya siku husika. Kwa maana tunakuwa bora kupitia yale tunayofanya katika maisha yetu ya kila siku. Una nafasi ya kuyaboresha au kuyaharibu maisha yako kupitia matendo ya kila siku.

Je unahitaji kupata mafundisho ya aina hii kila siku? Jiunge kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, tafadhali BOFYA HAPA KUJIUNGA.

Karibu katina neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza funguo tano tofauti za kuthibitisha kuwa utajiri ni haki yako ya kuzaliwa kupitia maandiko matakatifu. Kwanza tunatakiwa kutambua kuwa Mungu ameumba mfumo wa kuzalisha utajilisha kwa kila mwanadamu ambao hauwezi kushindwa kutimiza hitaji hilo. Pesa inajibu kila hitaji la mwanadamu kwa ajili ya ukamilisho wa maisha ya utakaso wake.

Tunaweza kusema kuwa pesa ni halamu katika mtazamo hasi wa mafundisho ya dini lakini tukitafakari kwa msaada wa roho mtakatifu tunagundua kuwa Mungu anataka tuishi maisha ya kujitosheleza, naam maisha ya utajiri (soma Mhubiri 10:19). Mungu anataka uwe na pesa za kutosha kwa sababu tatu kuu: Moja, upate kufadhili kazi za kitume – enendeni Ulimwenguni kote na kuhibiri injiri. Mbili, kuhistili vyema familia yako – familia yako inatakiwa kuwa sehemu ya furaha na siyo sehemu ya manunguniko yanayotokana na kupungukiwa kifedha. Tatu, kuitawala dunia – tumepewa mamlaka ya kuitawala dunia kwa faida ya maisha yetu.

Soma: MAISHA YA UTAJIRI AU UMASIKINI: JE NI IPI HAKI YAKO YA KUZALIWA?

Ufunguo #1: Mungu ndiye chanzo halisi cha utajiri (Wafilipi 4:19). Hivyo, tuna kila sababu ya kutambua kuwa utajiri halali unatoka kwa Mungu ikiwa tunafanya kazi za kiroho ambazo zinamruhusu Mungu kuwa chanzo chako cha pekee cha utajiri. Pia maandiko matakatifu yanasema, "Hasiyefanya kazi, hapaswi kula" (2 Wathesalonike 3:10), na Mungu ndiye Muumba wa kazi. Hivyo, kwa Mungu tunapata nguvu za kuzalisha mali, tunapata kila rasilimali kwa ajili ya kukua kipesa, tunapata uwezo wa kiakili kutumia rasilimali zinazotuzunguka, na tunapata baraka ya kuzalisha mali zaidi (Kumbukumbu la Torati 8:18). Tafsiri yake ni kwamba, Daima Mungu atakupa kitu cha kuweka mikono kwenye yako, atakupaka mafuta uwezo wako, na atakupa baraka za kufanikiwa zaidi ikiwa unatii amri zake.

Ufunguo #2: Biashara ni Mfumo wa kukuwezesha kutengeneza utajiri (Luka 19:13). Hakuna utajiri ambao unapatikana bila mfumo maalumu wa uzalishaji mali. Hiyo haimaanishi kwamba kila mtu ameitwa kumiliki biashara-lakini kila mmoja wetu atajihusisha na biashara kwa namna moja au nyingine, iwe ni kwenye kazi, katika ununuzi au uwekezaji. Biashara ni kubadilishana bidhaa au huduma kwa faida au faida ya kiuchumi. Unapoajiriwa, unauza huduma zako. Hiyo inakufanya uwe sehemu ya mfumo. Japo pamoja na kuajiriwa bado una nafasi ya kujifunza zaidi kuhusu mfumo husika ili siku moja na wewe umiliki biashara yako. Hivyo, wote tumeitwa kumiliki na kutawala vitu vyote ili Ulimwengu huu uwe mahala pazuri pa kuishi.

Ufunguo #3: Kila aina ya biashara inakutaka ufanye kazi. Na kila kazi inayofanywa kwa bidii na maarifa inamzawadia mhusika faida na kutegemea faida bila kufanya kazi ni kujitafutia umasikini (Mithali 14:23). Kumbe, biashara ni kazi ni kazi ni biashara. Pia, tunatakiwa kutambua kuwa kazi siyo laana, na sio taabu. Hivyo, ikiwa unahitaji utajiri halali ambao tumeona kuwa ni haki yako ya kuzaliwa ni lazima uepuke malalamiko au manung’uniko kuhusu kazi. Kwa tafsiri hiyo, kazi unayoifanya unatakiwa kuitazama katika jicho la zaidi ya malipo, kwa maana chimbuko la kufanya kazi ni kutoka kwa Mungu ambaye anasema atabariki kazi ya mikono yako na kukuwezesha kuwa tajiri.

Ufunguo #4: Umiliki wa ardhi siyo wa hiari. Amri ya kwanza kabisa ambayo mwanadamu baada ya kuumbwa alipewa kulingana na maandiko matakatifu ni kuzaa na kuitawala dunia (Mwanzo 1:28). Hivyo, tumeumbwa kuwa watawala na katika msingi huo kumiliki ardhi siyo ubinafsi, siyo anasa bali ni kuitikia amri hiyo. Hatupaswi kuwa chini ya udhibiti wa Ulimwengu bali tunatakiwa kutumia kila kilichopo ndani yake kwa ajili ya kufikia ukuu katika kila sekta ya maisha yetu. Unapofanikiwa kutambua msingi wa amri hii katika kuvuta kila hitaji la maisha yako, utaingia katika viwango vya ustawi ambao haujawahi kuota katika kipindi cha maisha yako. Ni wakati wako kumiliki ardhi ambayo ni msingi wa biashara nyingi (Walawi 25: 23 – 28).

Ufunguo #5: Tumeumbwa katika sura na mfano wake. Tunasoma katika sura ya mwanzo ya Mwanzo kuwa Mungu alituumba kwa mfano wake, kulingana na sura yake (Mwanzo 1:26 – 28) na kumpa binadamu jukumu la uumbaji mdogo kwa kumuelekeza kuijaza na kuitawala dunia. Kupita amri sura na mfano wake tunatakiwa kuumba (ubunifu) vitu mbalimbali ambavyo vitaifanya ukuu wa Mungu uonekane katika uso wa Dunia. Kwa sura na mfano wake tumepewa uwezo wa kutengeneza vitu kupitia malighafi ambazo Mungu ametupa kwa wingi. Hivyo, sisi ni mawakili wa Mungu katika kutumia, kumiliki na kuumba (Zaburi 50: 10 – 12). Somo la kujifunza hapa ni kwamba mali tunazomiliki na tunazokusudia kumiliki tunapata kupitia uwezo ambao Mungu ametupatia. Utajiri tulionao ni wake na lazima utumike kulingana na matakwa yake. Tutafute na kuomba Mungu atupatie utajiri unabariki familia, jamii, na nchi. Baraka hiyo ni pamoja na kushiriki katika imani na upendo, kufanya kazi ambazo zina maana na zinaonyesha ubunifu wa Mungu ndani mwetu.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI

Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo nimekushirikisha funguo tano ambazo zinaonesha kuwa utajiri ni haki yako ya kuzaliwa. Mungu hapendi tuwe masikini na tunaposhindwa kuidai haki yetu ya kuzaliwa (haki ya kuwa tajiri) tunakuwa tunatenda dhambi. Mungu ametupatia kila kitu kwa ajili ya kutumia vitu hivyo kumiliki utajiri tunaotamani. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganishi hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema OFA hii.

๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

HAPA NDIPO WAAJIRIWA WANAKOSEA KATIKA MIRADI YAO

NENO LA LEO (JANUARI 04, 2021): HAPA NDIPO WAAJIRIWA WANAKOSEA KATIKA MIRADI YAO.

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni wakati mwingine tena tumepata kibali cha kuwa hai. Kitu pekee ambacho tuna deni kutokana na uhai huu ni jinsi tutakavyotumia siku hii ya leo kukamilisha majukumu yaliyopo mbele yetu. Wajibu uliopo mbele yetu ni kuhakikisha tunatumia siku hii kutoa thamani kwa jamii inayotunguka na viumbe vyote kwa ujumla. 

Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya kupata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, tafadhali JIUNGE SASA.

Katika neno la tafakari ya leo tutaona jinsi ambavyo waajiriwa wengi wamekuwa wakipoteza hela nyingi katika uanzishaji na uendeshaji miradi. Kwa waajiriwa inafahamika kabisa kuwa asilimia kubwa mishahara yao haiwezi kutosheleza mahitaji yote ya msingi. Ili wawe salama kifedha wengi wamekuwa wakianzisha miradi mbalimbali kama sehemu ya kujiongezea kipato. Hata hivyo, kwa wengi miradi hii imekuwa sehemu ya kupoteza fedha zaidi kutokana na sababu zifuatazo:-  

Kweli #1: Usimamizi mbovu. Waajiriwa wengi kutokana na kubanwa na majukumu yao ya kazi ambapo kuna nyakati wanalazimika kisafiri nje ya sehemu miradi yao ilipo wanajikuta miradi ilishaharibika kuliko ilivyotarajiwa. Mfano, kawaida kwa Waajiriwa kujihusisha kwenye miradi ya kilimo na ufugaji. Miradi hii yote ufanikiwe kupata faida inahitaji usimamizi wa karibu was mhusika. Siyo miradi ya kutegemea kupewa taarifa za mtu aliyepo kwenye mradi na ukaamini taarifa hizo. Hali ni tofauti kwa Waajiriwa kwa kuwa wengi wao wanaendesha miradi ya kilimo na ufugaji kwa rimoti. Matokeo yake inapofikia wakati wa mavuno wanajikuta wamepoteza hela nyingi kuliko ilivyotarajiwa.

Kweli #2: Hakuna taarifa za maandishi za mradi husika. Hela inayoingia na hela inayotoka hakuna taarifa zake sahihi. Wengi wanaendelea kuweka hela kwenye miradi husika kutoka katika vyanzo vingine bila kuandika sehemu yoyote. Matokeo yake kuna miradi mingi ambayo inaendeshwa kwa hasara hila kwa kuwa hakuna maandishi wengi wanahisi kuwa miradi hiyo inazalisha faida.

Kweli #3: Kutumia ushauri ambao haujafanyiwa uchunguzi. Wengi wanakurupuka katika uanzishaji wa miradi kwa maana hili neno sahihi ambalo nawezakutumia ili nieleweke kwa urahisi. Waajiriwa wengi wanaanzisha miradi yao kwa kutumia taarifa za kusikia au ushauri wa juu juu. Mtu akisikia kilimo cha tikiti kinalipa ghafla anakimbilia kulima tikiti, akisikia kuna faida katika ufugaji kuku ghafla nae anakimbilia huko au akisikia nyumba za kupanga zinalipa ghafla nae anazama. Kwa ujumla Waajiriwa wengi wanaanzisha miradi yao kwa kuigaina.

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza baadhi ya mapungufu yaliyopo katika uanzishaji na uendeshaji wa miradi kwa Waajiriwa. Kweli hizo tatu nilizoeleza hapo juu zinaweza kuwa zinamgusa yeyote kati yetu hivyo ni suala la kutazama upya kama mradi wako unazalisha faida au unaedelea kuwa sehemu ya kupoteza fedha zako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: 1. Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ 

https://fikrazakitajiri.blogspot.com/2020/01/orodha-ya-vitabu-nilivyosoma-katika.html?m=1.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Mambo Niliyojifunza Kwenye Kitabu cha So Smart But….: How Intelligent People Lose Credibility and How They Can Get It Back (Jinsi Watu Wenye Akili Wanavyopoteza Uaminifu na Jinsi ya Kuurejesha)

Habari ya leo rafiki na msomaji wa mtandao wa fikra za kitajiri. Ni matumaini yangu kuwa unaendelea kupambana kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Karibu tena katika mtandao wa FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya uchambuzi wa kitabu cha wiki hii. Leo hii ikiwa ni wiki ya 24 katika kipindi cha mwaka 2017 naendelea kukushirikisha uchambuzi wa vitabu nikiwa na lengo kubwa la kukupa maarifa ambayo ni wajibu wako kuyatumia ili ubadilishe kila sekta ya maisha yako.

Uamzi wa kubadilisha maisha yako upo mikononi mwako na hivyo kama mpaka sasa haujajifunza kitu chochote katika makala hizi nakushauri husiendelee kupoteza muda wako na badala yake ufanye mambo ambayo umezoea.

Ili uendelee kunufaika na makala za mtandao huu BONYEZA HAPA na ujaze fomu utakuwa umejiunga na mtandao wa fikra za kitajiri. Kwa kujiunga na mtandao huu utapata makala zinazochapishwa na mtandao wa fikra za kitajiri moja kwa moja kwenye barua pepe yako bila malipo yoyote.

Kabla ya kuendelea kushirikisha uchambuzi wa kitabu cha leo nitumie muda huu kuomba radhi kwa kuchelewa kukutelea uchambuzi huu ndani ya wiki iliyoisha jana. Hii imetokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu kwa kuwa mazingira niliyopo kwa sasa hayana nishati ya umeme ya uhakika.

Kitabu cha wiki hii ni “So Smart But…..” kutoka kwa mwandishi ALLEN N. Weiner. Mwandishi wa kitabu hiki amebobea katika tasnia ya mawasiliano na kwa muda mrefu amejihusisha katika utoaji wa semina mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa kocha kwa watu mbalimbali katika masuala ya mawasiliano na uzungumzaji. Semina zake mara nyingi zimejikita katika kuwafundisha watu namna wanavyoweza kuboresha ushawishi, hamasa binafsi pamoja na uaminifu bora kwa jamii inayowazunguka.

Mwandishi huyu alipata msukumo wa kuandika kitabu hiki mara baada ya kuona kuwa watu wengi wana taaluma mbalimbali kiasi ambacho wamefikia hatua ya kutambuliwa kama watu maarufu katika taaluma zao. Pamoja na watu hawa kufikia viwango vya juu vya taaluma, ajabu ni kwamba ni wachache kati ya watu hawa ambao wanaweza kujieleza mbele za watu na kueleweka. Wengi wao wanahitaji msaada katika mbinu za mawasiliano ili kufikisha ujumbe wanaokusudia. Tunafahamu fika kuwa bila mawasiliano mwanadamu hawezi kufanikisha jambo lolote na hii ndio sababu kubwa mwandishi wa kitabu hiki kuwaandikia watu kwa ajili ya kuwashirikisha misingi mikuu ya mawasiliano.

Karibu tujifunze wote machache niliyojifunza kutoka kitabu hiki:

1. Watu kadri wanavyokuwa na uzoefu wa kazi/biashara ndivyo inafikia hatua wanahisi kuwa kuna mtu juu yao ambaye hapendi kile wanachofanya. Mtu huyu anaweza kuwa ni bosi wako au mshindani wa biashara. Hata hivyo hisia hizo zinasababishwa na watu kutokufahamu mbinu za mawasiliano kwa kutumia lugha ya mwili. Zaidi ya asilimia sitini ya mawasiliano katika jamii uwasilishwa kwa mfumo husio wa maongezi ambao unahusisha lugha ya mwili. Mwandishi anatushirikisha kuwa unaweza kupata matinki ya mtu anayewasilisha kwa kusoma namna ambavyo anashirikisha viungo vya mwili wake katika kufikisha kuwasilisha ujumbe. Bahati mbaya ni wafanyakazi wachache sana ambao wanatambua mbinu hii ya mawasiliano na hivyo wengi wao wameshindwa kueleweka pindi wanapojieleza au pengine wameshindwa kuwaelewa wafanyakazi wenzao au waajiri wao.

2. Ni rahisi watu kutambua kiwango cha uaminifu/heshima yako kwa kuangalia lugha yako ya mwili (jinsi unavyoonekana kwa ujumla), mpangilio wa sauti yako pamoja na mpangilio wa maneno yako. Hivi ni vitu vitatu muhimu ambavyo vinamtambulisha mtu yeyeto pindi anapowasilisha mada yake kwa mtu mwingine au watu wengine. Na hapa ni muhimu kufahamu kuwa mwonekano wako pamoja na mpangilio wa sauti kwa pamoja vinachangia asilimia tisini ya kueleweka kwako ikilinginishwa na asilimia kumi tu ya mpangilio wa maneno. Muhimu, hapa unatakiwa kufahamu kuwa unahitaji kujitambulisha haraka kwa kutumia lugha ya mwili wako (mwonekano wako) pamoja na kuhakikisha kuwa unatoa sauti yenye kila chembe ya kujiamini kwa kadri uwezavyo.

3. Ili ueleweke kwa urahisi unahitaji vizingatia vitu vifuatavyo kwa ajili ya kuboresha mwonekano wako; i) matumizi ya nafasi yako pindi unapojieleza ii) matumizi bora ya kushikana mikono na wengine iii) matunmizi ya muda – zingatia kutumia vyema muda uliopewa iv) mwonekano wa uso wako v) matumizi ya viungo vyako vya mwili – fahamu namna ya kutumia kila kiungo cha mwili wako vi) zingatia mfumo wa mavazi yako pamoja na unene wa mwili wako; na matumizi bora ya mapambo ya nafasi.

4. Unapowasilisha mada yako vitu vifuatavyo vitakusaidia kuboresha mpangilio wa sauti yako; i) kiwango cha sauti yako – kuzungumza kwa sauti ya juu ili kila mmoja asikie; ii) mpangilio wa sauti – kupanda na kushuka kwa sauti kwa kutegemea kila sehemu unayozungumzia iii) kasi ya sauti yako iv) urefu wa sentensi zako v) matumizi fasaha ya lugha vi) zingatia rafudhi ya lugha husika vii) zingatia matumizi sahihi ya misamihati viii) zingatia matamushi sahihi ya misamihati ix) fahamu kwa kina mantiki ya kile unachowasilisha x) hakikisha unaongozwa na takwimu kuliko blah blah; na xii) hepuka kurudiarudia maneno mara kwa mara.

5. Fahamu kuwa unaendelea kuchunguzwa na wasikilizaji wako hata baada ya kumaliza wasilisho lako. Hapa mwandishi anatushirikisha kuwa ni muhimu kila mmoja afahamu kuwa wasikilizaji huwa wana tabia ya kuchunguza vitu vidogo kutoka kwa mtu anayewasilisha hata kama amemaliza kuongea. Mfano, wanaweza wakachunguza jinsi unavyotembea, namna ulivyokaa na hata namna unavyowasikiliza wengine.

6. Kuna njia tano za kukuwezesha kugundua kama unaeleweka kwa mada unayowasilisha na njia hizo ni; i) chanzo cha mada – fahamu kwa kina chimbuko la mada yako na namna unavyotakiwa kutumia lugha ya mwili kuiwasilisha; ii) ujumbe – fahamu nini hasa unataka wasikilizaji wasikie/wapate kutoka kwako; iii) chunguza sehemu ambapo wasilisho lako linafanyikia; iv) chunguza mtazamo wa wawasikilizaji – hii itakusaidia kutambua kama unaongea jamii unayohitaji hama vinginevyo; na v) nyakati – tambua mada unayowasilisha kama inaendana na nyakati zilizopo.

7. Watu wengi wana taaluma ambazo zimewafanya kujichanganua kama wataalam wabobevu katika sekta flani. Hata hivyo, ni wachache ambao wanaweza kuelezea kwa ufanisi kile wanachofahamu kwa jamii inayowazunguka. Hii inatokana na ukweli kwamba wengi wanashindwa kutafsri yale wanayofahamu katika taalamu zao kwenye mazingira halisia ya jamii inayowazunguka. Kutokana na hali hii wengi wanakosa uaminifu kwa jamii inayowazunguka ikiwa ni pamoja na mabosi wao au wafanyakazi wenzao.

8. Uaminifu wa mawasiliano yako kazini au jamii inayokuzunguka unapimwa kwa kuzingatia baadhi ya misingi kama ilivyoorodheshwa hapa; i) epuka kuongea maneno mengi ambayo hayatekelezeki – chagua maneno machache ya kuongea na hakikisha unaishi maneno yako; ii) mara zote jikite kwenye mantiki ya mada unayowasilisha – epuka porojo; iii) kuwa na uwezo wa kueleza mambo magumu katika lugha rahisi; iv) kuwa na mawazo mbadala mengi kwa ajili ya kukuza pato la mwajiri wako au kupunguza upotevu wa rasimali; v) mahusiano mema na wenzako – fanya kazi kama timu; vi) uwezo wa kuingilia kati na kushauri pale ambapo mambo hayaendi sawa; vii) uwezo wa kufanya majukumu yako kwa haraka; viii) kuwa mtu wa kufikiria kwa haraka; ix) kuwa mwandishi mzuri; x) jifunze kuwa msilikazaji mzuri; na xi) uwezo wa kujiamini kwa kile unachofanya. Misingi hii kwa ujumla, inalenga kumfanya kila mmoja wetu kuwa na picha kubwa katika majukumu ya kazi pamoja na mahusiano yake na jamii inayomzunguka.

9. Kuna mbinu tano ambazo unaweza kutumia kwa ajili ya kueleza na mada yako na ukaeleweka kwa ufasaha. Moja, ni kueleza mada yako ufupi lakini ukigusa maeneo yote muhimu. Mbili, ni kueleza mada yako kwa mapana zaidi. Tatu, ni kueleza mada yako kwa kina huku ukielezea kwa mapana kila eneo la mada yako – hapa unahitaji kuweka wazi uhakika wako kwenye mada husika. Nne, unahitaji kuainisha kwa mapana matokeo (faida au madhara) tarajiwa kutokana na kutekeleza/kutotekeleza ushauri wako. Tano, onyesha maono yako juu ya fursa/changamoto zilizopo katika mada unayowasilisha – hapa unahitaji kuonesha matumaini yako hasa chanya kwa siku zijazo endapo ushauri wako utazingatiwa. Mbinu hizi zinaweza kutumiwa kwa pamoja au kwa kuchagua baadhi yake pale ambapo mtu anakusudia kuwasilisha mada yake na akaeleweka vizuri kwa walengwa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba endapo utazingatia mbinu hizi kila mmoja atasema kuwa unafahamu malefu na mapana juu ya mada unayowasilisha na pia unafahamu matokeo tarajiwa endapo ushauri wako utachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwa na maono juu ya mada husika.


10. Baada ya kuwasilisha mada yako kwa ufasaha unahitaji kufahamu mbinu za kuchukua maswali na kuyajibu kwa ufasaha ili kukidhi mahitaji ya waulizaji. Mbinu hizi ni pamoja na i) kwanza unatakiwa kuhakikisha unaandika maswali yote na kila mtu aliyeuliza; ii) elewa kiini cha swali – tambua muulizaji anahitaji kufahamu nini; iii) tambua swali lina makusudi gani – kuna baadhi ya maswali yanalenga kukupima ufahamu wako juu ya mada husika; iv) jibu kwa ufasaha kuhakikisha ulefu wa majibu yako unaendana na ulefu wa swali uliloulizwa; na v) epuka kurudirudia – jibu moja kwa moja ulichoulizwa. Mwandishi anatushirikisha kuwa endapo kila mmoja atafuata mbinu hizi katika kujibu maswali atafanikiwa kujijengea heshima kutoka kwa wasikilizaji wake.

11. Unapotakiwa kuwasilisha mada yako ndani muda mfupi unatakiwa kuzingatia sehemu kuu tano za mada yako. Kwanza, ndani ya muda mfupi ainisha sehemu ya tatizo/fursa – hapa eleza kwa ufupi tatizo/fursa iliyopo. Mbili, ainisha kwa ufupi visababishi – hapa unahitaji kueleza chanzo cha tatizo au fursa husika. Tatu, ainisha madhara ya tatizo husika. Nne, eleza kwa ufupi ni nini suluhisho la tatizo husika – njia za kufuata kwa ajili ya kutatua tatizo. Tano, eleza nini kifanyike kwa ajili ya kutatua tatizo husika – toa maoni yako yanayolenga kumaliza tatizo. Sehemu hizi tano zinalenga kumwezesha mwajiriwa/mfanyakazi kurahisisha mada yake ili ionekane nyepesi kwa mwajiri wake hata kama mada husika ni ngumu.

12. Watu wengi uaminifu kwa vile wanashindwa kutambua tamaduni za jamii wanazofanyia kazi. Mwandishi anatushirikisha kuwa tamaduni za sehemu husika wakati mwingine zinaweza kuonekana ni mambo ya kizamani lakini yana mchango mkubwa katika kujenga uaminifu kwa mtu yeyote. Hii ni kutokana na ukweli kwamba pale ambapo utafanya tukio ambalo linaenda kinyume na tamaduni au hitifaki za sehemu husika moja kwa moja utaonekana mtu wa hovyo na hivyo kujishushia heshima yako.

13. Watu wengi wana akili lakini wanashindwa kuona vitu katika maono ya picha kubwa. Mwandishi anatushirikisha kuwa ni wafanyakazi wachache sana ambao wanakuwa na mtazamo wa picha kubwa katika mazingira ya kazi zao kwani walio wengi wanaishia kutazama picha ya mahitaji na majukumu yao tu. Ili kujitofautisha na watu wa namna hii mwandishi anatushirikisha kuwa kila mmoja anatakiwa kuwa na picha kubwa ambayo inajumuisha (a) maono ya taasisi au kiwanda (b) maono ya uongozi wa taasisi (c) maono ya idara (d) maono ya timu au wafanyakazi wenzako na (e) maono yako binafsi. Hapa utagundua kuwa wafanyakazi wengi huwa wanatanguliza maono binafsi na kusahau maono mengine.

14. Kila mfanyakazi mwenye malengo ya kudumisha uaminifu wake hana budi kuwa na maono ya ngazi tatu. Ngazi ya kwanza inajumuisha maono ya karibu yako – hii inajumuisha maono juu yako mwenyewe kwa maana ya unahitaji kuwa mtu wa aina gani, yapi unahitaji kuyakamilisha katika maisha yako kupitia kazi unayofanya. Ngazi ya pili inajumuisha maono ya kati – haya ni maono yako juu ya wafanyakazi wenzio au waajiriwa wako. Katika ngazi hii unatakiwa uwe na upeo wa kutambua mahitaji ya wanaokuzunguka kutoka kwako – nini hasa mchango wako kwa wale wanaokuzunguka. Ngazi ya tatu ni maono ya mbali – haya yanajumuisha ndoto zako. Ngazi hii inajumuisha mchango au mawazo yako ambayo unayatoa kwa taasisi au kampuni yako kwa ajili ya uendelevu wake. Kama mwajiriwa mwenye uaminifu unahitaji kuonesha ngazi za maono haya kupitia yale unayosema (mchango wako wa maneno), unayofanya (mchango wako wa vitendo) na jinsi unavyojihusisha na majukumu yako (kiwango cha ufanisi wako katika majukumu yako).

15. Wafanyakazi wengi katika ngazi za uongozi wa juu wanakosa uaminifu kwa vile wanashindwa kuwa na uwezo wa kuhimili misukosuko inayowakabili katika kazi zao. Hapa mwandishi anatushikisha kile ambacho mabosi wengi wanashindwa kutimiza kwa vile wengi wanakuwa ni waoga wa kusimamia maamuzi yao. Hili ni kosa ambalo linapoteza heshima kwa bosi yeyote yule kwa watu wake wa chini kwa vile ataendelea kuonekana hana msimamo katika maamuzi yake. Muda wote kama bosi watu wa chini yako wanahitaji wa kuone katika misingi ambayo haibadiliki mara kwa mara.

16. Watu wengi wanashindwa kueleweka kwa vile hawajui namna ya kuunda sentensi katika muuondo unaokubalika. Kwa ujumla ujumbe wowote ambao unatolewa kwa njia ya maandishi au maongezi ni lazima uhusishe muunganiko wa maneno ambayo kwa pamoja yanaunda sentensi ambazo nazo zinaunda haya za mada husika. Kwa mantiki hii kila neno katika stori na kila sentensi kwenye stori husika zinaunda mtiririko wa maana kwa msomaji au msikilizaji. Hivyo kila mwandishi au mzungumzaji hana budi kuzingatia utumiaji wa maneno na muunganiko wa sentensi zilizokamilika katika kila haya ya stori yake.

17. Njia nyingine ambayo inawafanya watu wengi washindwe kueleweka ni namna wanavyopangilia sentensi zao zenye maana hasi na chanya. Sehemu hii inahusisha mbinu za sentensi ipi kati ya chanya au hasi itangulie kwenye maongezi au maandishi ya mtoa stori. Mfano tazama sentensi kama hizi 1. “kazi yako ni nzuri japo kuna vitu unatakiwa kuviboresha”; 2. Kuna vitu unatakiwa kuviboresha japo unafanya kazi nzuri. Katika sentensi ya pili msikilizaji/msomaji atachukua maana ya mwisho ya sentensi na kuelewa kuwa anafanya kazi nzuri wakati katika sentensi ya kwanza msikilizaji/msomaji ataelewa kuwa pamoja na kufanya kazi vyema bado ana sehemu ambazo anahitaji kuboresha. Kama mwandishi au mtoa mada kwa njia ya maongezi ni lazima uwe tayari kutambua ni sehemu ipi kati ya sentensi chanya na hasi itangulie katika stori yako kwa ajili ya kufikisha ujumbe uliokusudiwa.

18. Watu wengi wanashindwa kuaminika katika jamii inayowazunguka kwa vile wanaishi katika falsafa ya kuamini kuwa wanafahamu kila kitu. Mwandishi anatushirikisha kuwa huu ni ugonjwa mwingine ambao unapoteza heshima kwa watu wengi kwa vile wanashindwa kufahamu kuwa katika maisha kila mtu anahitaji kujifunza kila siku kutoka kwa wanaomzunguka. Mtu anapoonekana kuwa yeye anafahamu kila kitu ni mara chache sana atachukulia kwa ukaribu maoni ya watu wanaomzunguka na hivyo kusababisha hasieleweke kwa jamii inayomzunguka.

19. Watu wengi wanapoteza heshima zao kwa vile wanatumia maneno ambayo yanaifanya jamii inayowazunguka hisipende matendo yao. Ni kawaida kusikia kusikia misemo kama “haijalishi kama wananipenda hama la cha msingi ni lazima waniheshimu”. Kiongozi anayetumia kauli kama hizi anakuwa sio mtu wa watu na badala yake anatumia mabavu kufanikisha majukumu yake kwa watu waliopo chini yake. Mwandishi anatushirikisha kuwa katika jamii ni lazima kwanza uwekeze kwenye mtaji wa kijamii kwa maana yakujiweka karibu na watu wa karibu yako. Hii ni pamoja na kujihusisha kwenye matukio ya kijamii ambayo waajiriwa au jamii inayokuzunguka wanajihusisha nayo katika nje ya saa za kazi.

20. Watu wengi wenye taaluma za juu wamepoteza uaminifu/heshima kutokana na tabia mbaya wanazoishi katika jamii inayowazunguka. Mwandishi anatushirikisha kuwa tabia ya mtu ni utambulisho wa mhusika kwa jamii inayomzunguka. Unaweza kuwa na taaluma ya juu sana lakini kama hauna tabia njema kamwe hauwezi kupata heshima kwa jamii inayokuzunguka.

Haya ni machache ambayo nimeweza kukushirikisha kati ya mengi yaliyo kwenye kitabu hiki. Kupata nakala ya kitabu hiki BONYEZA HAPA na ujiunge na mtandao wa fikra za kitajiri kisha nitumie ujumbe wa kuomba kitabu hiki kupitia barua pepe fikrazakitajiri@gmail.com.

Niendelee kukuomba usambaze jumbe hizi kwa kadri uwezavyo ili yale unayojifunza yawafikie wengi na hatimaye tufanikiwe kuibadilisha dunia hii kuwa mahali pazuri pa kuishi (Unaposambaza makala hizi hakikisha haukopi na kupest badala yake share link ili hatimiliki za mwandishi wa makala ziheshimiwe). Nakutakia mapambano mema.

Karibuni kwenye fikra za kitajiri ili upate elimu hisiyokuwa na mwisho.

Born to Win ~ Dream Big 

Augustine Mathias Bilondwa

Namba ya Simu:      +255 786 881 155
Mwanzilishi wa Mtandao wa 
fikrazakitajiri.blogspot.com
Barua pepe:  fikrazatajiri@gmail.com


Mambo Niliyojifunza Kwenye Kitabu cha Do More Great Work: Stop Doing Busy Work and Start the Work That Matters (Fanya Kazi Nyingi Zenye Tija Kubwa: Achana na Kazi Zisizo na Tija)

Habari ya leo rafiki na msomaji wa mtandao wa fikra za kitajiri. Ni matumaini yangu kuwa unaendelea kupambana kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Karibu tena katika mtandao wa FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya uchambuzi wa kitabu cha wiki hii. Leo hii ikiwa ni wiki ya kumi na nane katika kipindi cha mwaka 2017 naendelea kukushirikisha uchambuzi wa vitabu nikiwa na lengo kubwa la kukupa maarifa ambayo ni wajibu wako kuyatumia ili ubadilishe kila sekta ya maisha yako.

Uamzi wa kubadilisha maisha yako upo mikononi mwako na hivyo kama mpaka sasa haujajifunza kitu chochote katika makala hizi za uchambuzi wa vitabu nakushauri husiendelee kupoteza muda wako na badala yake ufanye mambo ambayo umeyazoea.

Ili uendelee kunufaika na makala za mtandao huu BONYEZA HAPA na ujaze fomu utakuwa umejiunga na mtandao wa fikra za kitajiri. Kwa kujiunga na mtandao huu utapata makala zinazochapishwa na mtandao wa fikra za kitajiri moja kwa moja kwenye barua pepe yako bila malipo yoyote.

Kitabu cha wiki hii ni “Do More Great Work” kutoka kwa mwandishi Michael Bungay Stanier. Michael Bungay Stanier ni mjasiliamali na mwanzilishi wa Kampuni Box Of Crayons ambayo inafanya kazi zake katika mataifa mengi duniani. Mwandishi huyu mwaka 2006 alichaguliwa kama kocha (mhamasishaji wa mafanikio) mwenye mafanikio zaidi nchini Canada.

Michael Bungay Stanier anatumia kitabu hiki kutufunulia umuhimu wa kufanya kazi zenye tija katika kufikia mafanikio yetu na kuachana na kazi ambazo zimekuwa zikitumia muda wetu mwingi huku zikiwa na tija au mchango mdogo katika kufikia ndoto za maisha yetu.

Mwandishi anatushirikisha kuwa kwa ujumla kazi zote tunazofanya katika maisha zinagawanyika katika makundi matatu ambayo ni (a) kazi mbaya – bad work (b) kazi nzuri – good work (c) kazi kubwa – great work.

Mwandishi anatushirikisha kuwa kundi la kwanza linajumuisha kazi ambazo zinapoteza muda, nguvu, rasilimali na hata maisha ya muhusika. Kundi la pili linajumuisha kazi ambazo mhusika anafanya mara kwa mara na muda mwingi anautumia katika kazi hizi. Mara nyingi kazi za namna hii zinatokana na taaluma au uzoefu wetu na hivyo ni kawaida muhusika kufanya kazi hii kwa kiwango cha hali ya juu hata kama tija yake ni ndogo. Kundi la mwisho linahusisha kazi zote ambazo kila mtu anatamani kufanya kwa maana ya kazi ambazo zinaleta mabadiliko katika maisha ya mhusika. Na kazi hizi zina sifa ya kumfanya mhusika afikirie kwa mapana, aifurahie kazi anayofanya na kila siku atamani kuendelea kufanya kazi pasipo kusukumwa na mtu yeyote.

Mwandishi anatushirikisha kuwa kila mmoja anapaswa afikirie kufanya kazi zenye sifa ya kundi la mwisho kwa vile kazi hizi zinaleta tija kubwa kwa muhusika, zinamfanya muhusika hasiridhike na hatua aliyonayo bali aendelee kupambana kwa ajili ya kuongeza zaidi na hatimaye akabiliane na kila aina ya changamoto. Kazi hizi ndizo zinatofautisha watu au taasisi katika jamii kutokana na ubunifu na utimilifu wa kazi husika kati ya mtu mmoja na mwingine au taasisi moja na nyingine.  

Hata hivyo watu wengi wameendelea kufanya kazi za kundi la pili kwa vile hawataki kujisumbua sana hasa katika kufikiri, wanaogopa kubeba au kuchukua maamzi magumu (risk), wanatafuta usalama wa kazi kuliko tija ya kazi husika na hawako tayari kuangaika mara kwa mara kutafuta maarifa mapya. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kazi za kundi la tatu zinabadilika mara kwa mara kutokana na muda, yaani kazi ya maana unayofanya leo hii baada ya miaka mitano haitakuwa kazi ya maana na badala yake itakuwa kwenye kundi la pili.

Karibu tujifunze wote machache niliyojifunza kutoka kitabu hiki:

1. Mwandishi anatushirikisha kuwa pamoja na kwamba kila mtu anatamani kufanya kazi kubwa tena zenye tija (kundi la tatu) ni lazima tutambue kuwa kazi hizo zinatokana na kazi zetu za kila siku. Kwa maana hii, hatupaswi kuacha kazi zetu za sasa na kuanza kutafuta kazi zenye tija bali tunachotakiwa kufanya ni kufanya kazi zetu za sasa kwa weledi, ubunifu na utimilifu ili kupitia kazi hizi tufanikiwe kuhamia kwenye kundi la kazi za aina ya tatu. Hivyo tunatakiwa kutumia kazi zetu za kila siku kufikia viwango vya mabadiliko makubwa katika kila sekta ya maisha yetu.

2. Mwandishi anatushirikisha kuwa kinachowasukuma watu kufanya kazi kubwa zenye tija ni ile hali ya kutaka kufanya vitu kwa njia ya upekee au utofauti. Kwa maana hii ni lazima kwanza mhusika atathimini hali ya kazi yake ya sasa na hatimaye afanye maamuzi ya kuiboresha kazi hiyo au pengine atafute kazi nyingine ambayo ina tija zaidi. Hata hivyo wengi wanatamani kufanya kazi kubwa zenye tija lakini ni wachache ambao wapo tayari kujitoa kwa ajili ya kazi hizo.

3. Kazi kubwa (great work) zina sifa ya kuwa rahisi au ngumu kwa kutegemea nyakati. Mwandishi anatushirikisha kuwa katika kufanya kazi kubwa kuna kipindi mambo yatanyooka na utaona kuwa kila kitu kinaitikia wito wako japo pia kuna nyakati ambazo utaona kila kitu kinakukimbia. Hivyo ni muhimu kujipanga kwa ajili ya kukabiliana na nyakati ngumu kipindi unapokuwa kwenye nyakati za neema.

4. Kufanya kazi kubwa zaidi inaweza kuwa sehemu ya maisha yako endapo utaweka mikakati ya kubadilisha kila sekta ya maisha yako ili iendane na kusudi la maisha yako. Hivyo ni wazi kuwa kazi kubwa sio lazima itazamwe kwa maana ya kipato inachokuingizia bali kila mmoja anatakiwa kutathimini kazi yake kwa kuangalia nini hasa kusudi la maisha yake hapa duniani. Kwa maana hii hatua ya kwanza kabisa ya kufanya kazi kubwa yenye tija ni lazima kufahamu kwanza wewe ni nani na kwa nini uliumbwa hivyo ulivyo kwa maana ya kutambua umuhimu wako katika ulimwengu huu.

5. Kabla ya kuanza safari ya kufanya kazi kubwa yenye tija ni lazima kwanza utambue ni wapi unaelekea na wapi ulipo kwa sasa. Mwandishi anatumia mfano wa kwamba ukiwa unasafiri kuelekea sehemu ambayo hujawahi kufika ni lazima utaweka maandalizi kwa kutafuta taarifa muhimu juu ya sehemu hiyo ikiwa ni pamoja na umbali wake. Ndivyo ilivyo hata kwenye kuianza safari ya kufanya kazi kubwa zenye tija, kwanza kabisa ni lazima utambue ni nini hasa unahitaji kutokana na kazi yako. Kwa maana ya kwamba ni nini matamanio ya maisha yako, nini hobi zako, ni vitu vipi vinakupa furaha ya kweli au vitu vipi vinaipa roho yako furaha ya kweli.

6. Unapoanza safari ya kufanya kazi kubwa zenye tija ni muhimu kwanza ujiulize maswali haya; (i) Ni nini hasa utambulisho wangu katika jamii? Hapa unatakiwa ujiulize sifa muhimu ulizonazo (ii) Je ni lipi lengo na mwelekeo wangu? Hapa jiulize ni vitu gani unataka kuvikamilisha katika maisha yako na kwani nini unataka vitu hivyo. (iii) Jiulize ni watu gani naweza kuambatana nao? Hakuna kazi ambayo utaifanya peke yako ni lazima pawepo timu ambayo utashirikiana nayo. (iv) Je ni changamoto zipi ambazo navutiwa kuzitatua? Kazi yoyote ni kutatua changamoto hivyo fahamu ni sekta ipi unajisikia huru kutatua changamoto zilizopo. (v) Ni jinsi gani naweza kujenga mtazamo/mazingira chanya juu ya kazi yangu?. (vi) Je naitikia vipi kwenye vikwazo vilivyopo mbele yangu? (vii) Je ni nini furaha yangu na (viii) Je ni jinsi gani naweza kuhimili vipindi vya mpito?.

7. Fanya tathimini ya viwango vyako vya juu kabisa katika utendaji kazi ambavyo uliwahi kufikia katika hisitoria yako. Mwandishi anatushirikisha kuwa katika kufikia viwango vya ufanyaji kazi kubwa zenye tija ni lazima kwanza uorodheshe ufanisi wako wa hali ya juu ambao unajivunia kuwahi kufikia. Hapa unatakiwa utambue kuwa ufanisi huu unatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine lakini pia unatofautiana kati ya aina ya kazi au tukio. Unapokuwa kumbuka nyakati za ufanisi wako wa hali juu inasaidia kujenga hamasa ya kwa nini husiendele kufanya vyema katika kazi au malengo yako unayojiwekea. Hii ni kutokana na ukweli kwamba nyakati hizo za ushindi zinakujengea picha ambayo inakufanya ujione kuwa wewe ni mshindi na kalama ya ushindi ipo ndani mwako.

8. Kila mtu ana asili ya ukubwa ndani mwake tokea uumbaji wake. Katika hili maandishi matakatifu yanatuambia kuwa “husiogope kwa kuwa Mimi Bwana wako nalikufahamu ungali tumboni mwa mama yako”. Huu ni urithi tosha wa kutufunulia kuwa kila mtu ana alama ya ushindi ndani mwake na hivyo unaweza kufanikiwa katika kila ya aina ya kazi ambayo umedhamiria kufanya endapo ataondoa hofu ambayo imemkwamisha kwa muda mrefu. Hivyo kuanzia sasa kila mara jisemee kuwa naweza kufanya kazi yoyote kubwa na yenye tija ya hali ya juu kwa kuwa ushindi upo ndani mwangu tangu siku niliyoumbwa.

9. Ushindi katika kazi yako au tukio lolote lile unaleta hali ya kujiamini ambako pia uambatana na hali ya kujiona wewe ni wa thamani na una uwezo wa hali ya juu. Vitu hivi si vigeni kwa mtu yeyote yule kutokana na ukweli kwamba kila mmoha alishawahi kushinda pasipo kujali ushindi wako ulikuwa wa tukio au kazi ipi. Kwa ujumla ni kwamba ushindi wowote ambao umepatikana kwa jitihada mahususi huwa unamfanya muhusika ajione mwenye fahari juu ya nafsi yake.  

10. Je unajitambua wewe ni nani? Mwandishi anatushirikisha kuwa kamwe hauwezi kufikia anga za kufanya kazi kubwa zenye tija endapo haujui kusudi la maisha yako hapa duniani. Hatua ya kwanza kabisa ni kutambua wewe ni nani na kwani nini mpaka sasa unaishi ikilinganishwa na wale wengine ambao pengine hawakufanikiwa kufikia umri wako. Kusudi la maisha yako ndo mwongozo wako wa kutambua ni kazi ipi unatakiwa kuikamilisha ulimwenguni humu.

11.  Tunajifunza kufanya kazi kubwa zenye tija kutoka kwa waliofanikiwa kufikia viwango vya juu. Hapa mwandishi anatushirikisha umuhimu wa kuwa na watu amabao ni ‘role model (mtu wa kuigwa)’’ wetu katika kufikia viwango vya ufanisi tunavyokusudia. Unaweza kuwa na role models wengi kwa kutegemea kila sekta ya maisha yako unayotaka kuiboresha. Hata hivyo, unatakakiwa kufahamu kuwa role model wako sio lazima awe mtu maharufu kwani watu wa namna hiyo wanatuzunguka kila sehemu. Role model wako anaweza kuwa baba au mama, padre/mchungaji, mwalimu au jirani yako kwa kutegemea sehemu ya maisha yako unayotaka kuboresha.

12. Ni vitu vipi vinakusukuma kufanya kazi yenye tija tofauti na unavyofanya kwa sasa? Mwandishi anatushirikisha kuwa kama unaongozwa na sababu zenye uzito itakuwa rahisi kufikia kule unakokusudia na kinyume chake ni kwamba kama haufahamu wapi unaelekea au unaongozwa na sababu finyu haitakuwa rahisi kwako kufikia viwango vya mafanikio makubwa. Hivyo hapa tunafundishwa umuhimu wa kujiuliza sababu za kwa nini tunaka kufanikiwa na baada ya kupata majibu ya swali hili tunakiwa kutengeneza ramani ili itumike kama mwongozo wa kuongoza hatua zetu.

13. Maisha ni kachumbari yenye mchanganyiko wa vitu vingi kama vile mahusiano, pesa, mapenzi, dini, elimu, afya, jamii, familia, ubunifu n.k. Katika mchanganyiko huu kila mmoja ana wajibu wa kujiendeleza na kuboresha maisha yake katika kila sekta. Kwa kufanya hivyo tunapata thamani halisi ya maisha yetu ambayo kimsingi inatokana na matendo yetu ambayo pia ni ukamilisho wa kazi zetu za kila siku. Hivyo kazi zetu pia ni ukamilisho wa wito wetu hapa duniani. Jambo la kujiuliza ni je unajua wito wako ni upi? Hii ni kutokana na ukweli kwamba kama haujui wito wako utaishia kufanya kazi ambazo sio wito wako na hatimaye utaishia kufanya kazi hizo kwa ufanisi mdogo sana.

14. Ni vitu vipi vinakuwasha mwili na kukuambia kuwa bado… bado…. bado…. Mwandishi anatushirikisha kuwa kama hauna sababu za kukusukuma zaidi ni rahisi kuangukiwa kwenye mtego wa kuridhika na hatimaye kujikuta unafanya kazi za kawaida. Hivyo ni muhimu kila hatua ujione kuwa safari bado ni ndefu, hii itakufanya uendelee kutatua changamoto nyingi zaidi zenye viwango tofauti na hatimaye uzidi kufanikiwa katika kila sekta ya maisha yako. MUHIMU kumbuka mafanikio sio pesa tu bali mafanikio ni kwenye kila sekta ya maisha kama ambavyo tumeona hapo juu kuwa maisha ni kachumbari yenye kila aina ya mchanganyiko wa viungo.

15. Wengi wetu tunafanya kazi kwenye taasisi au kampuni ambazo tumeajiriwa. Kama hatujaajiriwa basi tunaweza kuwa tumeajiri watu katika kampuni zetu. Hivyo wote kwa pamoja tunafamu kuwa jukumu kubwa la mwajiriwa ni kutimiza majukumu ya mwajiri wake kwani hiyo ndio njia pekee ya yeye kuendelea kwenye kibarua chake. Hata hivyo pamoja na kutekeleza majukumu ya mwajiri wetu tunafahamu kuwa ndani mwetu tunaweza kufanya vitu vikubwa zaidi ya haya tunayotekeleza kwa mwajiri. Kazi kubwa iliyopo mbele yako ni kuhakikisha kila siku unafanya kazi zaidi ya matakwa ya kazi yako. Hii itakusaidia kutumia nguvu iliyopo ndani mwako ambayo hajatumiwa ipasavyo.

16. Jifunze kusema HAPANA au NDIYO kulingana na swali unaloulizwa. Mwandishi anatushirikisha kuwa sio kila swali majibu yake ni ndiyo. Kabla ya kusema ndiyo ni lazima ujipe muda wa kutafakari swali unaloulizwa na pale ambapo unaona kuwa unachoulizwa/kuombwa ni vigumu kutekeleza tafuta namna ya kumjibu mhusika pasipo kuharibu uhusiano wake kwako. Hivyo hivyo kwa jibu la hapana, sio kila utakachoambiwa hapana ni hapana kweli, unatakiwa kutathimini jibu unalopewa kabla ya kuamua kusonga/kutosonga mbele.

17. Je upo tayari kufanya kazi kubwa yenye tija? Mwandishi anatushirikisha kuwa haitoshi kusoma kitabu hiki na kuhamasika bila kuanza kuchukua hatua halisia. Baada ya kusoma kitabu hiki hadi kufikia hapa naamini kuwa umepata mwanga wa kugundua nu changamoto zipi ambazo pengine zimekukwamisha kufikia uwezo wako wa juu katika utendaji kazi wako. Ni wajibu wako sasa kuamua ni wapi uboreshe ili uachane na maisha yako ya awali na hatimaye uanze kuishi msingi wa maisha mapya yenye kuongozwa na kauli mbiu ya kutumia uwezo wako wote katika kufikia mafanikio unayokusudia.

18. Kila mmoja ana wazo la kimafanikio na mawazo hayo yanatujia kila mara katika mfumo wa fikra zetu. Hata hivyo kwa kuwa hatujiamini tumekuwa tunapoteza mawazo ya kifursa na hatimaye tunaendelea kufanya vitu vya kawaida. Mwandishi anatushirikisha kuwa kama tunahitaji kutoka hapo tulipo kwa sasa ni lazima kwanza tujiamini kuwa tunaweza na mara moja tuanze kufanyia kazi mawazo yetu. Unaweza kuorodhosha mawazo kadhaa uliyonayo na ukayapa maksi kila mmoja kutoka na umuhimu na uwezekano wake kiutendaji na hatimaye ukachagua wazo moja lenye maksi nyingi ili uanze kulitekeleza mara moja.

19. Je una ujasiri kiasi gani wa kufanya kazi kubwa zenye tija? Ili ni swali ambalo unatakiwa kujiuliza kabla ya kuanza safari yako. Swali linatakiwa likupe nafasi ya ya kujitafakari kama kweli una nia ya dhati ya kubadilika. Safari unayoianza ni safari ambayo inahitaji bidii ya kweli na nidhamu binafsi ya hali ya juu. Hakuna mtu wa kuja kugongea kengele kuwa umechelewa au muda umeisha. Wewe ndo mhusika mkuu katika kila tukio, yapo matukio ambayo yatakuwa na nia ya kukukatisha tamaa kama haujasimama vizuri unaweza kurudi nyuma kwa kasi kubwa. Hivyo unapoianza safari hii unatakiwa ufahamu kuwa kuna milima na mabonde mbele yako na yote hayo yapo kwa ajili ya kupima uimara wako katika kukabiliana nayo.

20. Ainisha msaada unaotaka kabla ya kuanza safari yako. Mwandishi anatushirikisha kuwa kabla ya kuanza safari yetu ya kufanya kazi kubwa zenye tija ni lazima kwanza tuainishe msaada unaotakiwa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kazi hizi hatuwezi kufanya peke yetu ni lazima tufanye kwa kushirikiana na jamii inayotuzunguka na hatimaye tufanikiwe kufikia malengo yetu.

Haya ni machache ambayo nimeweza kukushirikisha kati ya mengi yaliyo kwenye kitabu hiki. Kupata nakala ya kitabu hiki BONYEZA HAPA na ujiunge na mtandao wa fikra za kitajiri kisha nitumie ujumbe wa kuomba kitabu hiki kupitia barua pepe fikrazakitajiri@gmail.com.

Niendelee kukuomba usambaze jumbe hizi kwa kadri uwezavyo ili yale unayojifunza yawafikie wengi na hatimaye tufanikiwe kuibadilisha dunia hii kuwa mahali pazuri pa kuishi (Unaposambaza makala hizi hakikisha haukopi na kupest badala yake share link ili hatimiliki za mwandishi wa makala ziheshimiwe). Nakutakia mapambano mema.

Food of thought “In the long run, we shape our lives, and we shape ourselves. The processs never ends until we die. And the choices we make are ultimately our own responsibility”. (Eleanor Roosevelt)


Karibuni kwenye fikra za kitajiri ili upate elimu hisiyokuwa na mwisho.

Born to Win ~ Dream Big 

Augustine Mathias Bilondwa

Namba ya Simu:      +255 786 881 155
Mwanzilishi wa Mtandao wa 
fikrazakitajiri.blogspot.com
Barua pepe:  fikrazatajiri@gmail.com