👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza bidii kwa ajili kupata ushindi mdogo mdogo katika siku hii ya leo. Kumbuka ni kupitia ushindi mdogo mdogo wenye maboresho ya kile tunachofanya tunajikuta katika ngazi ya mafanikio makubwa sana.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linalenga kutukumbusha umuhimu wa kuishi maisha yanayoongozwa na kanuni tulizochagua kuishi na sio kuishi maisha ya maigizo. Watu wengi katika jamii wamepoteza dira ya maisha kwa kuwa wamekosa kanuni zinazowaongoza na matokeo yake wanaishi tu ili mradi siku zinaenda.
✍🏾Kila nafsi hapa Duniani imeumbwa kwa ajili ya kazi maalumu na ya kipekee. Kazi hiyo umepewa nguvu na uwezo wa kila aina wa kuhakikisha unaitekeleza kwa ufanisi kwa kadri ya mapenzi ya Muumba wako. Hata hivyo, kutokana na watu wengi kuishi maisha ya kuigiza wameshindwa kugundua na kuishi kazi ambayo wameumbwa kwa ajili ya kuikamilisha.
✍🏾Wengi wanaishi katika mtazamo wa kuiogopa jamii inayowazunguka kuchukua hatua. Hofu ya kwamba nitaonekana vipi kwa watu wa karibu yangu inatawala ndani ya mioyo ya watu hao na matokeo yake hofu hiyo inaendelea kuwa kandamizi kwao kufikia malengo ya kuishi kazi ya kusudi la maisha yao. Hofu ya kuchukua hatua zinazolenga kubadilisha maisha ya mazoea na kuingia kwenye Ulimwengu wa kusudi la maisha yao inaendelea kuwazuia kuwa wao na matokeo yake ni kuzunguka huku na huko wakiaangaika kupata maisha ya matamanio yao.
✍🏾Neno la tafakari ya leo linakusudia kukumbusha kuwa Dunia nzima wewe ni wa kipekee na aliyekuumba hajakosea. Achana na kauli kuwa Duniani ni wawili wawili, mnaweza kufanana kwa sura lakini kamwe hamuwezi kufanana kwenye tunu iliyopo ndani ya mioyo yenu. Dunia nzima hakuna mwingine kama wewe na hivyo unatakiwa kutambua kuwa kuendelea kuogopa kuchukua hatua kwa kigezo cha utaonekana vipi ni kupoteza muda na dira ya maisha yako.
✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha kuishi maisha ya kusudi la Muumba wetu na kuachana na tabia ya kuiogopa jamii. Ndani ya kila mmoja wetu kuna chemichemi ambayo haijatumika hivyo wajibu kujiuliza kama maisha yako yanaenenda katika dira inayokuridhisha au kila mara unahisi kuna sehemu hauitendei vyema nafsi yako. Chukua hatua sasa achana na maisha ya kuigiza.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com