👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa siku hii ya leo ambayo tunaianza wiki ya mwisho ya mwezi Machi, 2020. Ni siku ambayo wote kwa pamoja tuseme asanthe kwa Muumba kwa kutuwezesha kuwa hai kiasi ambacho bado tuna deni la kuibadilisha Dunia hii kuwa mahala pazuri pa kuishi kwa viumbe wote.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linalenga kutukumbusha umuhimu kuishi kanuni ambazo waliotangulia wametumia kanuni hizo na hakika wameweka alama kwenye uso wa Dunia. Neno la tafakari ya leo linabeba kichwa cha habari kutoka kwenye moja ya sheria za asili ambayo inasema “mavuno yanategemeana na mbegu unayopanda (the Law of sow and reap)”.
✍🏾Kupitia neno hili nitakushirikisha tabia ambazo zimepelekea ushindwe kufikia malengo yako kwa kuwa unaendelea kuvuna kulingana na mbegu unayopanda. Tatizo kubwa ni kwamba watu wengi hasa Vijana wa sasa tunatamani kuvuna maharage kutoka kwenye shamba la viazi au tunatamani kuvuna tani kadhaa kutoka kwenye shamba lenye uwezo wa kuzalisha gunia kumi. Karibu upitie kwenye hizi mbegu kandamizi ambazo umekuwa ukipanda katika maisha yako ya kila siku.
✍🏾 Mbegu ya kwanza ni tabia ya kulalamika. Tabia hii unaweza kuiona ya kawaida lakini ukweli ni kwamba ina athari kubwa kwenye maisha yako. Tafsiri ya kulalamika ni kwamba mhusika anakuwa haridhiki na tukio au hali iliyopo mbele yake kutoka kwa mamlaka au watu wanaomzunguka. Maana yake ni kwamba kadri unavyolalamika ndivyo unajitoa kwenye kuhusika katika tukio/hali unayolalamikia. Mfano, ni kawaida kukuta Vijana wengi wakiulizwa kwa nini hawajapiga hatua kiuchumi, utapata majibu kama vile hatuna ajira maana Serikali imetutelekeza; hali hii ya uchumi imesababishwa na wazazi wangu; Serikali ina mifumo mibovu ya kuwainua Vijana n.k. Kati ya majibu yote hayo ni nadra sana kupata jibu ambalo lina mgusa mhusika. Hivyo, athari kubwa ya kulalamika ni kujiondolea uwajibikaji na kuona kuwa kuna mamlaka au kundi la watu ambalo linatakiwa kuwajibika kwa ajili yako.
✍🏾 Mbegu ya pili ni kuwa na matumizi yasiyo ya lazima. Wapo watu wengi katika jamii ambao kila akipata pesa hawezi kutulia mpaka aone pesa hiyo imeisha kabisa. Pesa inakuwa kama inamuwasha kiasi ambacho anajikuta kwenye matumizi yasiyo na mpangilio. Niliwahi kuandika kuwa pesa inakaa sehemu ambazo inapendwa zaidi, hivyo, unapopata pesa kama haujui misingi ya kuipenda pesa ni lazima itafute milango ambayo itarudi sehemu ambako inapendwa zaidi. Vijana wengi wa sasa wanahitaji kupata utajiri lakini ni wachache ambao wanaweza kuweka akiba kwenye kila shilingi inayoingia mikononi mwao. Matokeo yake ni kwamba hauwezi kuvuna mazao ambayo haupo tayari kujibidisha katika kupanda na kupalilia mbegu.
✍🏾 Mbegu ya tatu ni tabia ya kuhairisha. Dunia inazunguka na kadri inavyozunguka masaa yanasogea, siku zinapita na miaka inapita. Hata hivyo, kadri yote hayo yanavyotokea umri wako unasogea na siku ulizoandikiwa kuishi hapa Duniani zinapungua. Huo ndiyo ukweli wa maisha yetu hapa Duniani, pamoja na kwamba maisha yetu hapa Duniani yana ukomo watu wengi bado wanaendelea kuishi kwa kusogeza matukio muhimu mbele. Hali inapelekea wengi kujichelewesha wenyewe kwa kuwa jambo ambalo lingewezekana leo linasogezwa mbele hadi linasahaulika.
✍🏾 Mbegu ya nne ni tabia ya kutaka matokeo ya haraka. Nimekuwa nikipigwa simu na vijana wengi ambao baada ya kuona blogu yangu (fikrazakitajiri.blogspot.com) tafsiri yao ya haraka wanajua kuwa hapa kuna utajiri wa majini. Wengi wanahitaji kuunganishwa na utajiri wa majini ambao wanategemea walale masikini na kuamka tajiri. Ukiwa na mawazo hayo finyu hakika kamwe utajiri utakuwa ni ndoto kwako hata pale ukifanikiwa kuwa tajiri kwa mbinu hizo chafu hakika furaha katika maisha yako itakuwa ni kitendawili.
✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha kuwa chochote tunachotamani kufanikisha katika maisha yetu ni lazima tuweke jitihada zinazolenga kupata mafanikio hayo. Kwa kifupi ni kwamba tutavuna kulingana na jitihada tunazoweka katika uzalishaji kwenye kila sekta ya maisha yetu.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.