NENO LA LEO (MACHI 16, 2020): ACHA KUPAMBANA PEKE YAKO CHEZA KAMA TIMU

✍🏾Habari ya asubuhi mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Namshukuru Mungu kwa siku hii ya leo ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuendeleza bidii ya kufanikisha malengo muhimu ya maisha yangu. Pia, namshukuru Mungu kwa ajili yako ambaye umeendelea kujifunza kitu kutokana na mfululizo wa neno la tafakari ya kila siku.



JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha umuhimu wa kutekeleza majukumu yako kwa kushirikiana na watu muhimu katika familia yako. Mara nyingi katika jamii inayotuzunguka tumezoea kuona biashara nyingi zinasimamiwa na baba peke yake kiasi ambacho anakuwa ni mhimili mkuu katika biashara au miradi ya familia.

✍🏾Katika familia nyingi za Kiafrika, baba ndo anajua ndani na nje ya kila mradi wa familia na wanafamilia wengine wanaendelea kuwa watazamaji. Inashangaza kuona kuwa familia inaundwa na baba, mama na watoto lakini baba pekee ndio mwenye kujua miradi ya familia.

✍🏾Hali hii inasikitisha sana kwa kuwa biashara au miradi ya aina hiyo uendelevu wake ni mdogo mno. Pale inapotokea baba hana nguvu za kuendelea kusimamia biashara au miradi hiyo moja kwa moja na biashara zinadorora kiasi cha kufa kabisa.

✍🏾Mifano ni mingi katika jamii inayotuzunguka ya familia ambazo zilikuwa katika viwango vya utajiri lakini kwa bahati mbaya baada ya kuondokewa na mhimili wa familia kila kitu kilipotea. Miradi yote imekufa kwa vile hakuna usimamizi unaoeleweka maana hakuna watu wenye uzoefu katika miradi hiyo.

✍🏾Kama ambavyo ushirikiano ni chachu ya kupatikana ushindi kwenye mchezo wa aina yoyote ndivyo ilivyo pia katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio ya kila aina katika maisha ya familia. Hakuna mchezo ambao utaweza kutoa matokeo mazuri na ya kufurahisha kama wachezaji wa timu husika hawana ushirikiano.

✍🏾Kama unahitaji kufika mbali hakikisha kila mmoja ndani ya familia anashiriki kwa nafasi yake ili kwa pamoja mtengeneze timu ya ushindi katika malengo ya familia na malengo binafsi. Kama ni biashara hakikisha kila mmoja anafahamu namna manunuzi yanavyofanyika, faida inavyotengenezwa, usimamizi wa mtaji, washirika muhimu katika biashara husika na usimamizi wa biashara ya ujumla wake.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha umuhimu wa kujenga ushirikiano imara ndani ya familia kwa ajili ya kufikia malengo muhimu kama familia na malengo binafsi. Pia, tumeona namna ambavyo biashara nyingi zilivyokufa baada ya kuondokewa na msimamizi wa biashara kwa kuwa waliobakia hawakuwa na uzoefu wa biashara husika.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii: https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw
onclick='window.open(