NENO LA LEO (MACHI 3, 2020): TAHADHARI! FAHAMU JINSI MAFANIKIO YANAVYOANGUSHA WATU WENGI.

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia wa FIKRA ZA KITAJIRI. Ni furaha yangu kuona kuwa nimeamka salama na nipo tayari kujitengenezea ushindi mdogo mdogo katika siku hii ya leo. Furaha yangu zaidi nikuona kuwa umeamka salama na umepata muda wa kuendelea kujifunza maarifa sahihi ambayo hakika kama unayafanyia kazi mafanikio kwako ni lazima.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BUREJiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Asubuhi hii ya leo karibu katika neno la tafakari ambapo nitakushirikisha namna unavyoweza kuanguka kutokana na mafanikio unayopata. Kila mmoja anahitaji mafanikio na kila mmoja anaweza kupata mafanikio ya kila aina katika maisha endapo amedhamiria kwa kuchukua hatua zinazomfikisha kwenye mafanikio ya maisha anayotamani. Ndiyo, unaweza kupata mafanikio ya ndoto yako hata kama kwa sasa unaona giza nene katika maisha yako ya baadae.

✍🏾Kadri unavyoanza kupata mafanikio katika maisha yako jihadhari sana na mafanikio hayo kwani mafanikio ni chanzo cha kuanguka kimaisha. Wapo watu wengi ambao waliteseka kwa muda mrefu kutafuta maangaiko na baadae wakajikuta katika ombwe kubwa kwenye maisha yao. Mafanikio ni chanzo cha kuanguka katika maisha kwa kuzingatia makundi mawili yafuatayo kwa watu waliofanikiwa katika jamii:

✍🏾 Kundi la kwanza linajumuisha Watu wanaofikiria kuwa endapo watafanikisha hitaji flani katika maisha yao ndipo maisha yatabadilika kuelekea kwenye hali flani ya maisha. Mfano, wengi wanaamini kuwa siku wakiwa na pesa za ndoto yao ndipo watakuwa na furaha ya maisha. Kweli, wanaweka bidii sana na kufanikiwa na uhuru wa kifedha katika maisha yao. Baada ya kupata fedha walizohitaji wanajikuta pamoja nakupata fedha walizohitaji lakini bado maisha yao hayana furaha kabisa bora hata ilivyokuwa awali. Kumbe, mafanikio yao badala ya kuwasogeza kwenye hitaji la moyo yamekuwa chanzo cha kuwadidimiza.

✍🏾 Kundi la pili linajumuisha watu ambao baada ya kupata mafanikio wanashindwa kulinda kanuni ambazo zimewafikisha kwenye mafanikio hayo na matokeo yake ni kwamba mafanikio yao yanadumaa au wanarudi mwanzo kabisa. Mfano, katika jamii tunafahamu watu ambao walifanikiwa kuanzisha biashara na biashara kukua kiasi cha kuwa na wateja wengi. Baada ya muda flani biashara hizo zilidumaa na nyingine kufungwa kabisa kutokana na wamiliki kushindwa kuendeleza kanuni muhimu za biashara walizotumia hapo awali.

✍🏾Kufafanua zaidi kuhusiana na kundi hili la pili, kwenye jamii tuna mifano mingi ya aina za biashara kama hizo ambazo pengine wamiliki walianza kutumia vibaya faida wanayotengeneza kwenye biashara au walianza kuwa na lugha mbaya kwa wateja na matokeo yake wateja wakahamia sehemu nyingine. Kumbe, kilichowaponza si kingine bali ni kiburi cha mafanikio waliyopata.

✍🏾Mwisho, Nelson Mandela aliwahi kutoa kauli ambayo inatakiwa kutuongoza katika maisha ya mafanikio tunayokimbilia kila siku katika maisha yetu. Na nukuu kauli hiyo hapa “ baada ya kupanda kilima na kufika kileleni ndipo niligundua kuwa kuna vilima vingi vya kupanda kuliko nilivyodhania awali”. Kutokana na neno la tafakari ya leo, tunafundishwa kuwa hatupaswi kupotoshwa na mafanikio tunayopata badala yake tunatakiwa kuongozwa na kanuni muhimu katika maisha yetu. Kanuni hizo hazipaswi kubadilika hata kama tumefanikiwa kimaisha. Pia, tunajifunza kuwa furaha katika maisha haipatikani kutokana na mafanikio tunayotamani bali furaha ya kweli inatengeneza kila siku katika mazingira yanayotuzunguka.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG 

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(