NENO LA LEO (MACHI 22, 2020): HAPA NDIPO UKOMBOZI WA KIFIKRA UNAKOANZIA.

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza moto unaolenga kutimiza malengo yako kwenye kila sekta ya maisha yako. Hongera kwa zawadi hii ambayo hakika ni deni kwako kuhakikisha unafanya kitu cha ziada ambacho kinalenga kukufikisha kwenye tumaini kuu la maisha yako.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza kuwa ukombozi halisi wa kifikra unaanzia kwenye kujitambua wewe ni nani na uhai ulionao una thamani gani katika uso wa Dunia hii. Pengine umezunguka sana huku na kule kwa kujaribisha kila aina ya kazi au biashara lakini unaona kila ukijitathimini unaona kuwa bado haujafikia hata chembe ya mafanikio unayotamani katika maisha yako.

✍🏾Huo ndiyo ukweli halisi kwa kundi kubwa la watu katika jamii. Watu wengi wanaishi bila kujitambua wao ni nani na kwa nini bado wanaishi. Tafsiri ya haraka ni kwamba wengi wanashindwa kutambua fumbo la maisha waliyopewa ni kwa ajili ya ukamilisho wa nini hapa Duniani. Hivyo, hatua ya kwanza kabisa kwenye ukombozi wa kifikra ni kujitambua wewe ni nani na maisha yako yapo kwa ajili ya ukamilisho wa jambo gani hapa Duniani.

✍🏾Kumbe, chochote unachofanya kwa lengo la kufanikiwa kimaisha itakuchukua muda sana kufanikiwa kama bado haujatambua thamani ya maisha yako. Mafanikio ya kweli utayapata pindi utakapogundua kusudi kubwa la maisha yako. Na baada ya kugundua kusudi la maisha yako ndipo utaanza kuishi maisha yenye furaha maana chochote utakachofanya kitakuwa ni ukamilisho wa furaha halisi katika maisha yako ya kila siku.

✍🏾Wapo watu wengi wanafanya kazi nzuri lakini moyoni mwao wamejawa na huzuni kubwa inayotokana na kutoridhika na mateso au usumbufu wa kazi hizo. Vivyo hivyo, wapo wafanyabiashara wengi wanapata faida ya kutosha kutokana na biashara zao lakini hawana furaha na maisha hayo. Tatizo hili linawakumba watu wengi katika jamii na chanzo chake kinaanzia pale ambapo wahusika wengi wanapochukulia kazi au biashara zao kama sehemu ya kutengeneza pesa.

✍🏾Ikiwa unafanya kazi au biashara kwa lengo kubwa la kutengeneza pesa hakika itakuchukua muda sana kufanikiwa kimaisha. Hapa naomba tuelewane kuwa mafanikio halisi katika maisha si pesa tu bali pamoja na pesa unayotengeneza ni lazima uone kuna kitu cha ziada ambacho kinakusukuma kufanya kazi au biashara. Hapa ndipo unatakiwa kujiuliza maswali haya: Je ninafurahia kazi au biashara yangu? Je kazi/biashara yangu inanipa uhuru kiasi gani? Je ningekuwa na pesa za kutosheleza mahitaji yangu na vizazi vyangu vyote ningeedelea kufanya kazi/biashara hii? Je kazi/biashara yangu inagusa vipi maisha ya jamii inayonizunguka?

✍🏾 Je nifanye nini kwa ajili ya kufikia ukombozi halisi wa kifikra? Ili ujitambue wewe ni nani na umeumbwa kwa ajili ya kukamilisha nini Duniani hapa huna budi ya kufanya mambo haya: unatakiwa kuwa na Muunganiko wa kweli na Muumba wako kupitia sara; unahitaji kujenga tabia ya kujisomea vitabu kwa ajili ya kupata maarifa kwenye kila sekta ya maisha yako; unatakiwa kuwa na watu waliofanikiwa kimaisha ambao unatamani kufikia mafanikio yao (role model); unatakiwa kutafuta watu muhimu wa kukuongoza kwenye kila sekta ya maisha yako (kiroho, kifedha, maendeleo ya nafsi yako na kijamii); na hakikisha unafanya unatanguliza thamani kwenye kila unalofanya badala ya kutanguliza pesa.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha kuwa pamoja na kukimbizana na pesa kila kukicha tuna wajibu wa kutambua kuwa ukombozi wa kifikra unaanzia pale tunapotambua thamani halisi ya maisha yetu. Hapa ndipo tunatakiwa kutambua kuwa maisha yetu si kwa ajili ya mafanikio binafsi pekee bali ni kwa faida ya viumbe vyote vyenye uhai katika uso wa Dunia hii.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG 

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(