👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Namshukuru Mungu kwa asubuhi hii ya leo kwa ni muhimu kwangu kwa ajili ya kuendeleza pale nilipoishia jana. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza bidii kwa ajili kufanikisha malengo muhimu katika kila sekta ya maisha yako.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nakukumbusha siri moja muhimu ya kuepuka madeni katika safari yako ya kuwa tajiri. Mara nyingi katika Jamii ni kawaida kukopa kutoka taasisi za kifedha au watu binafsi. Wapo wanaokopa kwa malengo kwa ajili ya kukamilisha hitaji muhimu katika maisha yao na wapo watu wengine wanakopa tu ili mradi amesikia kuna mkopo wenye masharti nafuu sehemu flani.
✍🏾Niliwahi kuandika kuwa unapochukua mkopo wowote unatakiwa kutambua kuwa umechukua kipato chako cha siku za mbeleni kabla hakijakomaa (kuiva). Kama ingekuwa ni chakula tungesema umelazimisha kula kabla ya kuiva. Na kwa asilimia kubwa mikopo huwa inaambatana na riba juu (interest). Hivyo unatakiwa kuwa makini kwenye kila mkopo unaochukua.
✍🏾Yawezekana kwa sasa tayari una madeni makubwa lakini nia yako ni kupiga hatua kwenye sekta uchumi wako. Unahitaji kuwa tajiri wakati kwa sasa una mzigo wa madeni makubwa. Siyo kosa, hila ninachokushauri kabla ya kusonga mbele na kuweka mikakati ya kupata utajiri unaotamani hakikisha unaanza kwa kuweka mpango wa kulipa madeni yote ambayo unadaiwa kwa sasa.
✍🏾Pia, katika mpango unatakiwa kutambua kuwa njia ya kumaliza madeni ni kuacha kukopa. Husikope kwa ajili ya kulipia deni maana unavyofanya hivyo sawa na kujikuta upo ndani ya shimo katika kupanga mbinu za kutoka kwenye shimo hilo moja ya mbinu ukapendekeza kuendelea kuchimba shimo. Matokeo yake ni kwamba kadri unavyoendelea kuchimba ndivyo utaendelea kuzama shimoni.
✍🏾Tumia kanuni kuu ya kukopa ambayo nilijifunza kutoka kwa Robert Kiyosaki kuwa mkopo mzuri ni ule ambao utalipwa kutokana na faida inayotengenezwa kwenye biashara. Kumbe, kabla ya kuchukua mkopo wowote unatakiwa kujiuliza nitautumia vipi mkopo huo kutengeneza faida ambayo itawezesha kulipia deni husika pasipo kuathiri kipato chango.
✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya linakukumbusha umuhimu wa namna gani tunatakiwa kuzingatia kulipa madeni tunayodaiwa kabla ya kupanga kusonga mbele katika safari yetu ya kuutafuta utajiri. Kanuni ni kwamba kila mkopo unatakiwa kuzalisha faida na si vinginevyo.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(