👉🏿Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama ukiwa na nguvu ya kutosha kwa ajili ya kuendeleza bidii inayolenga kukusogeza mbele zaidi ya pale ulipoishi jana. Kumbuka kuwa nguvu ya kazi inatokana na hamasa katika yale unayofanya na hamasa ya kweli ipo ndani mwako kwa maana hamasa unajipa mwenyewe.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linatukumbusha umuhimu wa kuishi maisha yenye furaha. Watu wengi katika jamii wanaishi kwa kuiweka furaha yao katika mizania ya vitu au hali flani vya nyakati zijazo. Kwa maneno rahisi ni kwamba, watu wanaishi kwa kuisogeza mbele furaha yao wakitegemea kuwa endapo watakuwa na hali au kumiliki vitu flani ndipo watakuwa na maisha yenye furaha ya kweli. Ndivyo maisha ya wanadamu wengi yalivyo.
✍🏾Mwandishi na Mtawa wa Kibuddha "Thich Nhat Hanh" kupitia chake cha “The Art of Power” anatushirikisha siri moja muhimu kuwa furaha ya kweli inatokana na “Sanaa na Sayansi ya Utulivu wa Akili”. Maana yake ni kwamba wanadamu wengi hatuna furaha ya kweli katika maisha kwa kuwa tunakosa utulivu wa akili kwenye kila kitu tunachofanya au hali inayotuzunguka. Akili zetu hazitulii kwenye jambo moja kwa wakati husika.
✍🏾Utulivu wa akili ni dhana pekee ya kumwezesha mtu kufikia mafanikio makubwa katika ulimwengu wa roho na mwili. Dhana hii imejengwa kwenye siri ya kuhakikisha akili yako kila wakati inatambua ni kipi kinatakiwa kufanyika kwa wakati huo na kipi hakipaswi kupewa nafasi. Mfano, kama unakula akili yako yote inatakiwa kuwa kwenye tendo hilo kuanzia jinsi unavyochukua chakula kwenye sahani, mkono unavyoweka chakula mdomoni, unavyotafuna chakula husika na hatimaye unavyomeza. Vivyo ndivyo inatakiwa kuwa kwenye kila tendo unalofanya.
✍🏾Jamii ya karne hii bahati mbaya sana imezungukwa na vitu vingi ambavyo muda wote vinaifanya akili iruke ruke kama chura. Mfano, mtu anakula huku anaperuzi simu matokeo yake ni kwamba akili haijatulia kwenye kula wala kuperuzi simu. Tafsiri yake ni kwamba hakuna anachofurahia kati ya matendo yote mawili. Kutokana na hali hii ya kushindwa kutuliza akili mwanadamu wa karne hii anakabiliwa na tabia ya kutokukamilisha majukumu au mipango yake kwa wakati.
✍🏾Pamoja na kwamba hakuna mwenye uhakika kuwa ataendelea kuwepo kesho lakini bado watu wanaishi kwa kusogeza mipango muhimu ya maisha yao mbele (wana ugonjwa wa kuhairisha). Kupitia dhana ya utulivu wa akili unatakiwa kuishi katika ukamilifu wa majukumu katika kila sekta ya maisha yako huku ukifurahia majukumu hao. Mfano, kama umetenga muda wa kuwa na mwenzi wako hakikisha unakaa naye katika penzi la dhati kana kwamba hautakuwa na muda mwingine wa kukaa naye.
✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha kuishi maisha yenye furaha ya kweli. Tunatakiwa kuishi katika msingi wa utulivu wa akili kwani nguvu hii itatuwezesha kuepuka kufanya makosa pamoja na madhara mengi ya kiafya, kiroho, kiuchumi na kijamii.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(