👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Namshukuru Mungu kwa ajili ya asubuhi ya lee. Namshukuru Mungu pia kwa ajili yako ambaye tumeendelea kuwa pamoja katika kundi hili. Ni kupitia muunganiko huu naamini kuwa kazi yangu hata kama ni kwa sehemu ndogo lakini kuna kitu itabadilisha kwenye Jamii.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo ambalo linaendelea kutukumbusha umuhimu wa hamasa katika maisha yetu hasa katika kipindi ambacho unaandamwa na kila aina ya changamoto katika maisha. Ukweli ni kwamba hakuna mwanadamu ambaye anapenda nyakati ngumu zitokee katika maisha yake japo katika uhalisia wa maisha nyakati hizo ni lazima zitokee.
✍🏾Kipindi cha nyakati ngumu huwa ni kipimo cha Imani ya mhusika katika yale anayofanya kwenye maisha yake ya kila siku. Kumbuka kuwa ndoto yoyote katika maisha yako ni lazima iambatane na Imani ambayo inakuwezesha kuwa na uhakika kuwa ipo siku ndoto hiyo itaumbika kwenye uhalisia wake. Hata hivyo, mwanadamu anakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinapelekea majaribu kwenye kila Imani aliyonayo katika maisha.
✍🏾Yamkini kuna kipindi ambapo utaona kama vile nguvu unayoweka haileti matokeo unayotaka kufikia. Kuna kipindi ambacho utaona jamii inakutenga na hakuna anayekuelea hasa katika kanuni muhimu za maisha ulizojiwekea. Kuna kipindi utaona kama vile mbele ni giza tupu hakuna upenyo ambao upo wazi kwa ajili yako kufikia mafanikio ya Imani ulizonazo. Kuna kipindi utaona kana kwamba hakuna tumaini la maisha huko mbeleni ambayo yataendana na Imani ulizonazo.
✍🏾Neno la tafakari ya leo linatukumbusha kuwa katika kipindi ambacho Imani yako inajaribiwa ni nyakati ambazo unatakiwa kuwa na hamasa kubwa kuliko kipindi chochote kile. Ni hamasa pekee ambayo itakuwezesha kusonga mbele na kuendelea kufanya yale unayofanya hata kama pengine hayaonyeshi dalili ya kufanikiwa siku za karibuni. Ni hamasa pekee ambayo itakuwezesha kufikria kwa mapana juu ya maboresho yapi unaweza kufanya ile kupata mafanikio unayotarajia. Ni hamasa pekee ambayo itakufanya uamini kuwa upo kwenye kipindi cha mpito na huko mbeleni kuna mafanikio yanayokusubiria. Ni hamasa pekee ambayo itakuwezesha nyakati ngumu kuziona kama sehemu ya kukuandaa na kukujenga kuelekea kwenye tabia halisi ya mafanikio.
✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tunakumbushwa kuwa yale yote tunayofanya kila siku ya maisha yetu ni lazima yapitie kwenye kipindi cha kujaribiwa Imani yako. Ni katika kipindi hiki wengi huwa wanakata tamaa na kurudi nyuma. Wengi huwa wanaacha kabisa na kupoteza Imani walizokuwa nazo kwenye yale wanayofanya. Neno leo linatujenga na kutupa tumaini jipya kuwa katika nyakati ngumu wanaovumilia huwa ndio wanafanikisha malengo. Kumbuka kuwa hata dhahabu ili ing’ae ni lazima ichomwe kwanza. Ndivyo ilivyo hata kwa mwanadamu, kipindi cha nyakati ngumu ni maalindalizi ya kumfikisha kwenye mafanikio ya kweli.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(