👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza bidii kwa ajili ya kupata ushindi mdogo mdogo katika siku hii mpya katika maisha yako. Endelea kujiandalia ushindi huo maana ni kupitia katika ushindi huo unaendelea kujiwekea alama katika maisha yako.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha mbinu ya kujifunza kutoka jamii inayokuzunguka. Mbinu hii si nyingine bali ni kujifunza kuwa msikilizaji kuliko kuwa mzungumzaji. Mwanafamanikio Robin Sharma katika kitabu chake cha "The Greatness Guide" anatushirikisha kuwa sababu kubwa ya kupewa masikio mawili na mdomo mmoja ni kwa ajili ya kusikiliza mara mbili zaidi ya tunavyoongea.
✍🏾Katika jamii watu wengi wanapenda kuongea pindi wanapokuwa kwenye mkusanyiko wa watu kuliko wanavyosikiliza. Wengi huwa wanaamini hoja zao ni bora kuliko za wengine. Wengi wanaamini kadri wanavyoongea ndivyo wanajijengea umaarufu katika kundi husika. Wengi hata pale wanaposikiliza wanafanya hivyo huku kichwani wakiwa wanawaza baada ya mtu flani kuongea Mimi nitaongea pointi yangu ili kumzidi alichochangia.
✍🏾Katika hali kama hiyo mhusika awezi kujifunza kutokana mada iliyopo mezani kwani yeye anakuwa na mawazo yake kichwani ambayo kwake anaona ni bora kuliko mawazo ya wengine. Matokeo yake ni kwamba ataendelea kuishi katika mawazo yale yale bila kuruhusu mawazo mapya kutoka kwa wengine.
✍🏾Kama ambavyo tumeona kwa wale mliosoma sehemu ya kitabu cha Principles and Power of Vision cha Dr. Mayles Munroe ambacho niliwashirikisha jumapili iliyopita kuwa kila mwanadamu ameumbwa kwa ajili ya kukamilisha kusudi maalumu hapa Duniani. Kila mwanadamu ana kipaji chake cha kipekee. Maana yake ni kwamba kila mwanadamu ana kitu kipya ambacho unaweza kujifunza kutoka kwake. Pale unaposhindwa kuwa na tabia ya kuwa msikilizaji unakosa nafasi ya kujifunza vitu vingi kutoka kwa watu inayokuzunguka.
✍🏾Hivyo, kuanzia sasa jifunze kuwa msikilizaji nawe utapata faida kubwa kutoka kwa watu wanaokuzunguka. Uzuri ni kwamba watu wengi hawana siri kwenye kazi au biashara wanazofanya. Wengi wanaongelea kazi au biashara zao kama sehemu ya kupata sifa kutoka kwa wasikilizaji wao. Hapo ndipo unatakiwa kuwa mdadisi kwa ajili ya kujifunza kitu kutoka kwao ambacho unaona kina faida kwenye yale unayofanya.
✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tunafundishwa siri ya kuwa na tabia ya kusikiliza kuliko tunavyoongea. Kila sehemu unayoenda katika kusanyiko la watu hakikisha kwanza unaifundisha roho yako isikilize zaidi kuliko kuongea. Na katika mada inayoongelewa masikio yako yawe tayari kukuruhusu kuchambua mawazo ambayo ni ya muhimu kufikia mafanikio unayotamani.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(