👉🏾Habari ya asubihi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Namshukuru Mungu kwa zawadi ya siku ya leo kiasi ambacho sasa naweza kuendeleza moto wa kutengeneza ushindi mdogo mdogo unaolenga kutimiza malengo yangu. Pia, namshukuru Mungu kwa ajili yako ambaye unaendelea kujifunza kutokana na neno la tafakari ninalokushirikisha kila siku.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha siri moja kuu ya kukuza kipato chako kwa kutumia moja ya hisia za mwanadamu. Katika mauzo ya bidhaa/huduma zozote unatakiwa kutambua kuwa watu hawanunui kwa moyo bali wananunua pale unapogusa hisia zao. Kwa lugha ya wenzetu kanuni hii inatafsiriwa kuwa “people don’t buy with heart instead they buy when their feelings are excited”.
✍🏾Kutokana na kanuni hiyo ya mauzo tunajifunza kuwa kila unapokusudia kukuza mauzo ya bidhaa/huduma zako ni lazima ujiulize ni hisia zipi unalenga kuzigusa katika soko lako kulingana na nyakati husika. Hisia za mwanadamu zinabadilika kila mara kulingana na mazingira yanayomzunguka pamoja na matukio mbalimbali yanayoendelea katika mazingira hayo.
✍🏾Katika neno la tafakari ya leo nakushirikisha hisia ya mwanadamu inayoitwa “HOFU” na namna unavyotakiwa kuitumia kutengeneza pesa. Katika Dunia ya leo mwanadamu anakabiliwa na HOFU ya kupoteza uhai kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa CORONA (Covid 19). Ugonjwa huu ni janga la kila mmoja wetu kulingana na namna unavyosambaa kwa kasi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
✍🏾Hata hivyo, katika jicho la kijasiliamali kila changamoto ina fursa kwa ajili ya kukuza uchumi. Kwenye kila changamoto zinazomkabili mwanadamu wajasiliamali wenye waliojiandaa huwa ndo wanafaidika kutokana kutokana na fursa zilizopo kwenye changamoto husika.
✍🏾Mwanadamu aliyepo kwenye kila kona ya Dunia anatawaliwa na hofu dhidi ya ugonjwa wa CORONA na kutokana na hofu hiyo yupo tayari kununua chochote ambacho ataambiwa kuwa kinasaidia kujikinga au kuponya ugonjwa huu hatari. Zipo fursa nyingi ambazo zimejificha ndani ya hofu hiyo na baadhi ya fursa hizo ni zipo kwenye ushauri unaotolewa kwenye namna ya kujikinga na ugonjwa huu.
✍🏾Tunaambiwa kuwa moja ya njia ya kujikinga na ugonjwa huu ni kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia viua wadudu (disinfectant). Hii ni fursa ya kuuza viua wadudu na kutengeneza faida kubwa katika kipindi hiki. Pia, tunaambiwa kuwa unaweza kujikinga na ugonjwa huu kwa kutumia viziba pua na mdomo (protector). Hii ni fursa ambayo soko lake lipo kila kona ambapo ugonjwa huu umethibitishwa kuwepo.
✍🏾Fursa nyingine unayoweza kutengeneza pesa kupitia hofu ya watu dhidi ya ugonjwa wa CORONA ni vyakula vyenye Vitamin C. Vyakula hivi vinasaidia kwa ajili ya kukuza kinga ya mwili dhidi ya vidudu vinavyoushambulia. Baadhi ya matunda yenye Vitamini C ni pamoja na Limau na Machungwa. Vyakula hivi havihitaji uwe na mtaji mkubwa ili uanze biashara hii.
✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tunajifunza kuwa watu hawanunui tu ili mradi wamenunua bali wananunua kwa ajili ya kukidhi hisia walizonazo. Wajibu wetu ni kuwa na macho yenye kuona hisia ambazo mwanadamu anapitia katika nyakati tofauti.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii: https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw
onclick='window.open(