NENO LA LEO (MACHI 28, 2020): *[SWALI] KWA NINI UNAENDELEA KUFANYA KAZI ZENYE MALENGO YA BAADAYE?*

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Kadri tunavyoelekea mwezi April, 2020 naendelea kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kukuletea kazi hii kila siku asubuhi. Ni kazi ambayo inahitaji nidhamu ya hali ya juu kuikamilisha lakini dhamira yangu nikuiendeleza nikiamini kuwa wapo vijana wengi ambao watabadilika na kuishi kusudi la maisha yao kupitia kazi hii. Kati ya vijana 100 wanaosoma kazi zangu nikifanikiwa kuwabadilisha hata 10 kati yao kwangu ni ushindi.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha siri inayotusukuma kufanya kazi kwa ajili ya kukamilisha malengo muhimu katika maisha yetu. Kazi ni kipimo cha thamani yetu hapa Duniani kutokana na ukweli kwamba ni kupitia kazi tunaweza kutatua changamoto za jamii.
✍🏾 *Swali muhimu la kujiuliza ni kwa nini tunaendelea kufanya kazi kwa ajili ya maisha ya baadae?.* Ukweli ni kwamba kinachotusukuma kufanya kazi ni LILE TUMAINI JEMA kwenye maisha yajayo. Tumaini hilo ndilo linatusukuma kuendelea bidii kwa ajili ya kuwa na maisha bora kwenye siku za usoni.
✍🏾Yajayo yanafurahisha. Kama ulivyo msemo huu wa tangazo ndivyo unatakiwa kuwa na tumainia matukio ya maisha yako ya baadaye. Tumaini bora ndilo litakuondolea hofu na kuendeleza jitihada za kila siku zinazolenga kuboresha maisha yako.
✍🏾Ni ukweli kwamba hakuna mtu hata mmoja ambaye anajua kesho itakuwaje. Hila kwa pamoja tunakubaliana kuwa Ulimwengu wa kesho utakuwa bora zaidi ikilinganishwa na Ulimwengu wa leo.
✍🏾Ni kutokana na tumaini bora katika maisha watu wanaendelea kufanya kugunduzi/uvumbuzi wa vitu vipya ambavyo vinalenga kuboresha maisha ya mwanadamu kwa siku zijazo. Hakika maisha ni kutumainia yaliyo bora siku za baadaye.
✍🏾Biashara, kampuni na taasisi mbalimbali zinaanzishwa kutoka kwa watu ambao wanatumainia kesho iliyo bora ikilinganishwa na sasa. Kumbe unapokuwa na tumaini bora kwenye maisha ya baadae unaanza kufikiria na kufanya kazi zilizo nje ya boksi.
✍🏾Tumaini bora kwenye maisha yajayo linakujenga kupita kwenye nyakati ngumu za maisha. Haijalishi utaanguka mara ngapi au kuahindwa mara ngapi, ukiwa na tumaini hakika utafanikiwa kwenye kazi unayoiona kuwa ngumu. Mfano, *Thomas Edison* alishindwa zaidi ya mara 1000 katika jaribio la kutengeneza bulb ya mwanga. Hata hivyo kutokana na msukumo wa tumaini la baadae aliendelea mpaka kufanikiwa kutengeneza bulb ya mwanga. Ni kutokana na tumaini lake Ulimwengu wa sasa unatumia bulb za umeme kwa ajili kuondokana na Giza.
✍🏾Tumaini bora ndilo linatufanya kuendelea kuweka jitihada kubwa katika kazi bila kujali umri wetu. Hakika watu wanaofanikisha mambo makubwa katika maisha yao ni wale ambao wamejiwekea kuishi kanuni ya kuamini kuwa umri siyo kigezo cha kuweka mipango ya maisha ya baadaye. Mfano, *Colonel Sanders* alistaafu akiwa na umri wa miaka 65. Kutokana na tumaini bora aliweza kutumia pension yake kuanzisha biashara ya mgahawa baada ya kujifanyia tathimini na kugundua kuwa alikuwa anaweza kupika kuku kwa mapishi matamu sana. Ni kutokana na mgahawa huo alifanikiwa kubadilisha historia ya maisha yake katika umri huo.
✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha kuwa ili kazi zetu ziwe na thamani ni lazima tuwe na tumaini jema kwenye maisha ya baadaye. Hakikisha unajenga tumaini jema kwa kujifunza kila mara kupitia mbinu mbalimbali bila kusahau usomaji wa vitabu. *Naendelea kukumbusha kupata nakala yako ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho utapata kanuni 107 kuhusu pesa.*
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

*BON TO WIN ~ DREAM BIG*
🗣🗣 *Mwalimu Augustine Mathias* 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii:https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw
onclick='window.open(