NENO LA LEO (MACHI 27, 2020): UMESOMA VITABU VINGAPI?

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Namshukuru Mungu kwa ajili ya siku ya leo ambayo ni zawadi muhimu ya kuendelea kuujenga ukuta was mafanikio. Pia namshukuru Mungu kwa kuendelea kuniunganisha na wewe. Ni matarajio yangu muunganiko wetu humu ndani umetuwezesha kujifunza kitu kwa ajili ya kuboresha maisha yetu.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linatukumbusha umuhimu wa kusoma vitabu katika maisha yetu ya kila siku. Jamii ina kundi kubwa la watu ambao hawana utaratibu wa kupata maarifa mapya kutoka kwenye vitabu vinavyohusiana na maendeleo binafsi katika kila sekta ya maisha yao.
✍🏾Ndani ya kundi hilo la watu wapo ambao wanaona kusoma kitabu ni kupoteza muda kwa kuwa kitabu husika hakina uhusiano na fani au kazi yake. Hivyo, ukiendelea library utakuta vitabu vingi vinavyofunuliwa kwa wingi ni vile ambavyo mara nyingi vinalenga kuwasaidia wahusika kwenye hitaji la wajibu wa lazima. Mfano, mwanafunzi atasoma kitabu kinachohusiana na mada anazotakiwa kujibia mtihani. Mbaya zaidi wanafunzi wa siku hizi hats nao hawasomi vitabu bali wanatumia notisi nyepesi ama walizopewa na wakufunzi wao au kutoka kwa watangulizi wao.
✍🏾Watu wengi baada ya kumaliza masomo wanasahau kabisa kuwa kuna kujisomea. Matokeo yake jamii imejaa watu ambao wana maarifa duni kuhusiana na maendeleo binafsi kwenye kila sekta ya maisha yao.
✍🏾Nasema maarifa duni kwa kuwa ni ukweli husiopingika kuwa elimu ya mafanikio haifundishwi popote katika silabasi za mfumo wa elimu. Ndio maana utakuta kuna Profesa lakini bado anaangaika kifedha.
✍🏾Tafsiri yake ni kwamba kama hauna utaratibu wa kujisomea vitabu maarifa ya kujiendeleza unayapata kupitia uzoefu binafsi, wazazi wako au jamii inayokuzunguka. Hapa ndipo kuna anguko la watu wengi katika jamii.
✍🏾Nasema kuna anguko kwa kuwa mtoto wa masikini atajifunza mbinu kuhusu misingi ya usimamizi wa fedha kutoka kwa mzazi masikini. Matokeo yake ni kwamba mbinu za kimasikini kuhusu pesa zinaendelea kutumiwa na mhusika na matokeo yake ataendelea kuwa masikini au na pato la kawaida.
✍🏾Kuendelea kuishi maisha ya kutojenga tabia ya kujisomea vitabu kwenye kila sekta ya maisha yako ni sawa na kutegemea muujiza wa mafanikio ndani ya giza nene. Kila unalotaka kufanikisha katika maisha yako lilishafunuliwa kutoka gizani na kuwekwa kwenye nuru ndani ya vitabu.
✍🏾Kitabu kimoja kina nguvu za kubadilisha mtazamo wa maisha yako kwa ujumla. Mfano nilibadirika kuhusiana na pesa kwa ujumla kupitia kitabu cha Robert Kiyosaki cha Rich Dad Poor Dad. Ni kitabu ambacho nashauri kila mmoja akisome na kutumia mbinu zilifunuliwa ndani yake.
✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha kuwa hakuna haja ya kuendelea kuishi katika giza wakati nuru ilishafunuliwa kupitia maarifa mbalimbali yaliyopo kwenye vitabu. Naendelea kukumbusha kupata nakala yako ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho utapata kanuni 107 kuhusu pesa.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BON TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii:https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw
onclick='window.open(