NENO LA LEO (MACHI 25, 2020): IWE MASIKINI AU TAJIRI WOTE WANA MATATIZO YA PESA.

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Namshukuru Mungu kwa ajili ya asubuhi hii ya leo na kwa ajili yako ambaye unaendelea kujifunza kitu kutokana na masoko ninayokushirikisha kila siku. Wajibu wetu mkubwa ili kazi hii iwe na tija ni kuweka mipango ambayo tunaitekeleza kwenye majukumu yetu ya kila siku. Kumbuka kuwa hata mbuyu ulianza na kama mchicha hivyo husitishike wala kukatishwa tamaa na hali yako ya sasa.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha jinsi ambayo tajiri na masikini walivyo na matatizo ya kipesa japo matatizo yao yanatofautiana. Wakati masikini anaangaika kupata pesa za kukidhi mahitaji yake ya kila siku upande wa pili tajiri nae anaangaika kulinda pesa zake ili ziongezeke. Karibu tupitie kwa pamoja matatizo ya kipesa yanayowakabili tajiri na masikini.

✍🏾Kwa kuanzia ngoja tuangalie matatizo ya kipesa ya masikini. Masikini kila kukicha hana anakabiliwa na maisha ya wasiwasi yanayoambatana na jinsi gani ataweza kukidhi mahitaji ya maisha kama vile pango la nyumba, chakula, bili za umeme na maji, ada za watoto na mahitaji muhiu kwa ajili ya tiba na afya bora. Haya ni mahitaji makuu ya maisha ambayo masikini kila anapoamka anaweza ni jinsi gani ataweza kutoboa na kufanikisha maisha yake kwa siku za baadae. 

✍🏾Ni kutokana na matatizo hayo ya kipesa, masikini anaendelea kujitumbukiza kwenye mikopo ya mara kwa mara ili kukidhi mahitaji muhimu ya maisha. Kadri anavyokopa ndivyo anajiingiza kwenye shimo kubwa la umasikini na matokeo yake ni mzunguko husiyo kuwa na mwisho. Hata hivyo, matatizo mengi ya kipesa kwa masikini yanaambatana na kukosa elimu ya msingi ya kuhusiana na pesa hali inayopelekea aendelee kufanya maamuzi mabovu kuhusu sekta ya pesa. 

✍🏾Kwa upande wa tajiri yeye anakabiliwa na matatizo ya kipesa yanayoambatana na jinsi gani ataweza kulinda utajiri wake. Changamoto kubwa ambayo tajiri anapambana nayo kila siku ni namna gani ataweza kukuza utajiri wake huku akiendelea kuishi maisha yenye furaha. Hapa tajiri anakabiliwa na maamuzi magumu ambayo yanaambatana na uhakika wa kupata: washauri wazuri wa kifedha; wanasheria wazuri; wafanyakazi waliobora; miradi ipi anatakiwa kuwekeza kwa ajili ya kukuza mtaji; namna gani atalipia kodi na kukidhi matakwa ya kisheria bila kuathiri uwekezaji wake; na jinsi gani ataweza kutimiza mahitaji ya jamii inayomzunguka ili hasionekane mtu mbaya.

✍🏾Pia, changamoto nyingine ambayo tajiri anapambana nayo ni jinsi gani ataweza kumudu majukumu yake ya kibiashara huku akiendelea kuwa na familia yenye misingi bora ya malezi. Hapa ndipo unakuta watoto wa matajiri wengi wanakua bila kuwa na misingi bora ya malezi kwa vile wazazi wao wanakuwa hawana muda wa kutosha wa kukaa nao.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha kuwa tajiri au masikini wote wana matatizo ya kipesa. Matatizo hayo yanatatuliwa kwa kuwa na elimu sahihi ya msingi kuhusu pesa (financial education). Kumbe, uwe tajiri au masikini wote ni muhimu kuwa na elimu hii ya pesa ili kutatua changamoto za kipesa zinazokukabili. Pata nakala yako ya uchambuzi wa Kitabu cha Rules of Money kwa bei ya ofa ya TSHS 5,000/= upate maarifa sahihi kuhusiana elimu ya pesa. 

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG 

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(