👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Namshukuru Mungu kwa ajili ya siku hii ya leo ambayo ni deni kwangu kuendeleza jitihada za kuliishi kusudi la maisha yangu. Pia, namshukuru Mungu kwa ajili yako ambaye unaendelea kujifunza kila kukicha kwa ajili ya kufikia mafanikio katika kila sekta ya maisha yako.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha jinsi ubongo wa mwanadamu ulivyo kiungo muhimu cha kukuwezesha kufanikisha mahitaji ya maisha yako. Neno la leo limetoka kwenye sehemu ya mafundisho niliyojifunza kutoka kwenye kitabu cha “Brain Rules” kutoka kwa mwandishi John Medina ambaye ni mtaalamu mbobevu wa elimu ya viumbe (biologist) na amejikita sana kwenye sehemu ya mfumo wa ubongo.
✍🏾Ubongo wa mwanadamu ni sehemu ndogo katika mwili wa mwanadamu ambapo sehemu hii ni takribabi ya asilimia 2 tu ya sehemu yote ya mwili wa binadamu. Sehemu hii pamoja na kwamba ni ndogo ikilinganishwa na sehemu nyingine za mwili inatumia karibia asilimia 20 ya nishati yote inayohitajika mwilini. Kama ilivyo kwenye sehemu nyingine za mwili, njia pekee ya kufanikisha seli za ubongo ziendelee kufanya kazi ni mzunguko wa damu kuendelea kusambaa.
✍🏾Hapa ndipo tunatakiwa kufanya mazoezi kwa ajili ya kuwezesha damu iweze kuzunguka haraka na kwa kasi na hivyo kufanikisha usambazaji wa hewa ya oksijeni katika seli za ubongo sambamba na kuwezesha kuondoa sumu kwa njia ya jasho katika sehemu mbalimbali za mwili.
✍🏾Mfumo wa ubongo ni sehemu ya hali ya juu katika viungo vya mwanadamu kiasi kwamba sehemu hii ndiyo inapima ufanisi wa kila mtu. Ufanisi huu unatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kulingana namna ambavyo kila mmoja amezoesha akili yake katika matukio ya maisha ya kila siku. Kwa maana hii mfumo wa ubongo ni teknolojia ya mawasiliano yenye ubora wa hali ya juu kuliko technolojia yoyote ile katika ulimwengu huu.
✍🏾Hata hivyo, watu wengi wameshindwa kutumia teknolojia hii ya hali ya juu kwa ajili ya kuboresha maisha yao kutokana na ukweli kwamba wengi hawafahamu namna ambavyo mfumo wa ubongo unavyofanya kazi. Hali hii inasababishwa na mfumo wa elimu ambao kuanzia elimu ya msingi hadi chuo hakuna sehemu ambapo wanafunzi wanafundishwa ni jinsi gani wanaweza kutumia mfumo wa ubongo kwa ajili ya kupata mafanikio makubwa katika maisha yao. Kinachofundishwa ni kumtaka mwanafunzi kukalili sehemu za ubongo na kazi zake basi.
✍🏾Matumizi ya ubongo yanatuwezesha kukabiliana na changamoto zinazotukabili katika maisha yetu. Katika kukabiliana na changamoto hizo, kuna njia mbili ambapo: Njia ya kwanza ni kutumia nguvu zaidi na njia ya pili ni kuwa na uwelevu/akili zaidi. Njia ya pili ni nzuri zaidi kwa vile inatuwezesha kutawala ulimwengu huu kwa kutumia nguvu kidogo huku tukitumia ubongo wetu. Njia hii ya pili ndiyo inamtofautisha mwanadamu na viumbe wenye ukaribu nae kama vile Gorila.
✍🏾Ubongo wa mwanadamu unamwezesha kuchanganua na kuumba vitu vipya kwa kutumia picha ya vitu husika inayojengeka akilini. Nyenzo hii ni muhimu kwani kupitia uwezo wa kuumba vitu kizazi kimoja kinaendelea kujitofautisha na vizazi vingine. Pia, kupitia uwezo wa uumbaji wa kila aina, mwanadamu anaendelea kuboresha mazingira yake ya utendaji kazi ikilinganishwa na vizazi vilivyotangulia.
✍🏾Ubongo ni kiumbe hai sawa na viumbe hai wengine, hivyo unahitaji haki zote ili uendelee kuishi. Haki kubwa kabisa ya kuwa hai si nyingine zaidi ya kuhitaji kuboreshwa kutoka chini kwenda juu kithamani (evolution) kupitia kwenye sheria ya asili ya kuchagua.
✍🏾Kiumbe yeyote anayeishi ni lazima apate chakula cha kutosha na baada ya kula ili kiumbe huyo aendelee kuwepo siku zijazo ni lazima pawepo kuzaliana kwa ajili ya kupitisha tabia moja kwenda kizazi kingine. Hivi ndivyo ubongo wa mwanadamu umekuwa ukiendelea kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Hapa utagundua kuwa ubongo unaboreshwa kutoka kwenye ubongo wa kutegemea asili (mizizi na matunda) hadi kufikia kwenye ubongo wa kutaka kuishi katika mwezi.
✍🏾Mfumo wa ubongo wa mwanadamu umesukwa tofauti kutoka mtu mmoja kwenda mwingine kulingana na shughuli zinazofanywa na mhusika. Hii ndiyo inapelekea watu kuwa na vipaji tofauti. Ndiyo maana kuna mchezaji kama Christiano Ronaldo ambaye amefanikiwa katika soka lakini ukimpeleka katika mpira wa kikapu hawezi kufikia mafanikio ya Michael Jordan.
✍🏾Hali hii ndiyo inatofautisha mafanikio ya wanadamu katika jamii tunamoishi. Habari njema ni kwamba ubongo unaweza mfumo wa ubongo unaweza kusukwa upya kutokana na mazoea ya kazi unayofanya. Ni kutokana na ukweli huu mwanadamu anahimarika kila siku kutokana na kazi ambayo amezoea kuifanya mara kwa mara kwa vile ubongo unazoea kile ambacho kinafanyika mara kwa mara.
✍🏾Seli za ubongo ndani mwake zina vinyuzi vidogo ambavyo uitwa neurons. Vinyuzi hivi vinafanya kazi sawa na nyaya za umeme ambapo katika mfumo wa ubongo vinasaidia kusafirisha taarifa moja kutoka kwenye ubongo kwenda kwenye viungo vingine vya mwili. Kumbuka kuwa mfumo wa ubongo ni sawa na Kompyuta ukiweka “gabage in gabage – ukiingiza uchafu utegemee kupata uchafu”. Ndivyo ilivyo kwenye mfumo wa ubongo, ukiujaza na taarifa zisizo na maana moja kwa moja utegemee kupata matokeo ya ovyo. Kumbe, ili upate matokeo chanya mfumo wako wa ubongo unatakiwa kujazwa na taarifa zenye matokeo chanya tu.
✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tunajifunza kuwa mwanadamu ameumbwa katika hali ambayo inampendelea kuitawala Dunia hii. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mfumo wa ubongo unamwezesha kila mmoja kujifunza vitu vipya na kutumia vitu hivi katika maisha yake ya kila siku. Kwa maana hii tunaweza kujifunza vitu vipya au kuboresha vitu vipya kwa kutumia silaha pekee ya seli za ubongo. Hapa ni mekushirikisha sehemu tu nilichojifunza kutoka kwenye kitabu hiki. Unaweza kupata uchambuzi wa kitabu chote katika mfumo wa nakala tete (pdf) kwa kuchangia kiasi cha Tshs. 4,000/= tu.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(