👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza majukumu yako ya kila siku. Hongera kwa siku hii ambayo Mungu anaendelea kutuzawadia kwa ajili ya kufanya kitu ambacho kitaweka alama kwenye maisha yetu. Alama hiyo ndiyo tunaweka bidii kila siku ili baada ya maisha yetu hapa Duniani, majina yetu yaendelee kuishi vizazi na vizazi.
✍🏾Ni kutokana umuhimu wa pesa kwenye maisha ya kila siku ya mwanadamu, zipo Imani nyingi zinazoambatana na upatikanaji wa pesa. Mfano, wapo wanaoamini kuwa pesa zipo kwa wateule wachache ambao wameandikiwa kufanikiwa kifedha na kundi kubwa la watu katika jamii limeandikiwa kuwa na fedha za kawaida.
✍🏾Wapo wanaomini kuwa ili tajiri ni lazima uwe pesa nyingi. Ni kutokana na Imani hii watu wengi wameshindwa kuchukua hatua hasa katika kuanzisha biashara kwa kuwa wanasubiria wawe na mtaji wa kutosha ndipo waanzishe biashara. Ukweli ni kwamba siyo kweli kwamba ili uwe tajiri ni lazima uwe na pesa nyingi. Wapo watu wengi ambao walipata pesa nyingi labda kutokanba na urithi, kushinda bahati na sibu au kupitia njia za wizi lakini cha kushangaza baada ya kipindi flani muda kupita walijikuta wamerudi kwenye hali yao ya zamani.
✍🏾Siyo kweli kwamba ukifanikiwa kupata madini ya thamani ndipo utakuwa tajiri. Wapo wachimbaji wengi wa madini ambao walibahatika kukutana na zari la mentari kwa kupata madini ya thamani kama dhahabu au almasi lakini baada ya muda walijikuta pesa yote imeyeyuka.
✍🏾Siyo kweli kuwa biashara au ajira vyote vikiambatana na kufanya kazi kwa bidii ndivyo vitakufanya uwe tajiri. Ukweli ni kwamba wapo watu wengi ambao wanajituma kila kukicha kwenye biashara au ajira zao lakini bado wanaangaika kifedha. Unatakiwa kufanya kazi kwa bidii lakini ili uwe tajiri ni lazima uwe na siri ambayo nitakushirikisha kupitia makala hii.
✍🏾Siyo kweli kwamba elimu ndiyo itakufanya uwe tajiri. Ukweli ni kwamba wapo Maprofesa ambao wanaishi kwa msongo wa mawazo uliopitiliza kutokana na uhaba wa fedha ikilinganishwa na mahitaji halisi ya maisha yao. Vivyo hivyo, siyo kweli kwamba aina ya fani ambayo umeajiriwa nayo ndiyo itakufanya uwe tajiri. Ukweli ni kwamba wapo Waandisi, Wanasheria, Wahasibu au Madaktari wabobevu ambao bado wanateseka kifedha.
✍🏾 Ili niwe tajiri natakiwa kufanya nini? Najua una hamu ya kufahamu siri ninayokushirikisha leo kwa ajili ya kuwa tajiri. Siri inasema “ili uwe tajiri unatakiwa kuwa na elimu sahihi ya pesa (financial education)”. Hapa simaanishi kuwa unatakiwa ukasomee fani za fedha kama vile uhasibu la hasha. Ninachomaanisha hapa ni kwamba ili uwe tajiri unatakiwa kuwa na maarifa sahihi kuhusiana na namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia kila shilingi unayopata kwenye maisha yako ya kila siku. Kumbuka pesa inaenda kule inakopendwa zaidi – tafsiri yake siyo kwamba ukiwa na mapenzi na hela moja kwa moja pesa itakufuata. Tafsiri yake halisi ni kwamba ili upate pesa za kutosheleza mahitaji yako ni lazima ufuate kanuni zinazohusiana na pesa.
✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha kuwa siyo pesa, biashara, ajira au madini ya thamani ambavyo vitatufanya kuwa tajiri bali utajiri umejificha kwenye maarifa sahihi kuhusiana pesa. Mwandishi Richard Templar anatushirikisha kanuni 107 za kutengeneza pesa kupitia kitabu chake cha Rules of Money. Nimechambua kitabu hiki kwa lugha rahisi ya Kiswahili na uchambuzi huu una kurasa 48 ambazo zipo katika mfumo wa Pdf. Uchambuzi huu unapatikana kwa bei ya punguzo ya TSHS. 5000/= kwa wanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. punguzo hili ni sawa na asilimia 50 maana gharama halisi ni TSHS. 10,000/= karibu uwe wa kwanza kupata Ofa hii.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambao nitakushirikisha siri moja muhimu ambayo kuanzia sasa unatakiwa kuitumia kwa ajili ya kufikia mafanikio ya uhuru wa kifedha. Ni ukweli husiopingika kuwa kila mtu kwenye Jamii tunayoishi anataka kuwa na uhuru wa kifedha. Pesa imekuwa ni nyenzo muhimu ambayo inasaidia mwanadamu apate mahitaji muhimu ya maisha yake ya kila siku.✍🏾Ni kutokana umuhimu wa pesa kwenye maisha ya kila siku ya mwanadamu, zipo Imani nyingi zinazoambatana na upatikanaji wa pesa. Mfano, wapo wanaoamini kuwa pesa zipo kwa wateule wachache ambao wameandikiwa kufanikiwa kifedha na kundi kubwa la watu katika jamii limeandikiwa kuwa na fedha za kawaida.