NENO LA LEO (MACHI 15, 2020): KAZI NI KIPIMO CHA THAMANI YA MAISHA YAKO. JE UNAFANYA KAZI IPI?

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matuimani yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza bidii katika majuikumu yako ya kila siku. Kama ambavyo hauwezi kuacha kula angalau siku moja ndani ya wiki ndivyo unapaswa pia kuhakikisha kila siku unafanya kitu kinacholenga kukusogeza mbele katika safari yako ya mafanikio.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha umuhimu wa kufanya kazi zenye tija na kuachana na kazi ambazo zinatumia muda mwingi wakati tija yake ni ndogo. Ni kupitia kazi pekee tunaweza kuishi kusudi la maisha yetu na ni kupitia kazi tunazofanya tunatakiwa kuona ndoto zetu zikiumbika kwenye uhalisia wake.

✍🏾Mwandishi Michael Bungay Stanier katika kitabu chake cha Do More Great Work anatuonesha kuwa kazi zote hapa Duniani zinagawanyika katika makundi matatu ambayo ni: (a) kazi mbaya (bad work); (b) kazi nzuri (good work) na (c) kazi kubwa (great work). Makundi haya yanapatikana kulingana na matokeo yanayozalishwa kulingana na jitihada inayowekwa kwenye kazi husika.

👉🏾 Je makundi haya yanatofautiana vipi? Kundi la kwanza linajumuisha kazi ambazo zinapoteza muda, nguvu, rasilimali na hata furaha ya maisha ya muhusika. Kundi la pili linajumuisha kazi ambazo mhusika anafanya mara kwa mara na muda mwingi anautumia katika kazi hizi. Mara nyingi kazi za namna hii zinatokana na taaluma au uzoefu wetu na hivyo ni kawaida muhusika kufanya kazi hii kwa kiwango cha hali ya juu hata kama tija yake ni ndogo.

✍🏾 Kundi la mwisho linahusisha kazi zote ambazo kila mtu anatamani kufanya kwa maana ya kazi ambazo zinaleta mabadiliko katika maisha ya mhusika. Na kazi hizi zina sifa ya kumfanya mhusika afikirie kwa mapana, aifurahie kazi anayofanya na kila siku atamani kuendelea kufanya kazi pasipo kusukumwa na mtu yeyote.

✍🏾Kumbe kama unahitahi kufikia mafanikio makubwa katika maisha ni lazima kufanya kazi zenye sifa ya kundi la tatu. Kazi hizi zinaleta tija kubwa kwa muhusika, zinamfanya muhusika hasiridhike na hatua aliyonayo bali endelee kupambana kwa ajili ya kuongeza zaidi na hatimaye akabiliane na kila aina ya changamoto. Kazi hizi ndizo zinatofautisha watu au taasisi katika jamii kutokana na ubunifu na utimilifu wa kazi husika kati ya mtu mmoja na mwingine au taasisi moja na nyingine.

✍🏾Hata hivyo watu wengi wameendelea kufanya kazi za kundi la pili kwa vile hawataki kujisumbua sana hasa katika kufikiri, wanaogopa kubeba au kuchukua maamzi magumu (risk), wanatafuta usalama wa kazi kuliko tija ya kazi husika na hawako tayari kuangaika mara kwa mara kutafuta maarifa mapya.

✍🏾Watu wengi pia wanashindwa kufanya kazi za kundi lata tatu kwa kuwa kazi za kundi hilo mara nyingi zinabadilika mara kwa mara kutokana na muda. Tafasri yake ni kwamba ni lazima uwe mtu wa kujifunza mara kwa mara bila kufanya hivyo utapotea kwenye ramani. Hapa ndipo unatakiwa kufahamu kuwa kazi unayofanya leo hii baada ya miaka mitano haitakuwa kazi ya maana na badala yake itakuwa kwenye kundi la pili. Hii ni kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ambavyo vinabadilika kila mara.

✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tunajifunza kuwa mafanikio yetu yanapimwa kutokana na kazi tunazofanya. Hata hivyo kazi hizo zinaweza kutoleta matokeo tarajiwa kama hatujatambua kuwa zinaangukia katika kundi lipi. Baada ya neno la tafakari ya leo ni wajibu wetu kujiuliza kama kazi tunazofanya zinaleta tija inayolingana na nguvu, rasilimali na muda tunaouweka kwenye kazi husika.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii: https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw
onclick='window.open(