UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Mambo 5 Ya Kuzingatia Unapoamua Kujilipa Kwanza.

NENO LA SIKU_FEBRUARI 28/2022: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Mambo 5 Ya Kuzingatia Unapoamua Kujilipa Kwanza.
Habari ya leo rafiki yangu na mfuatuliaji wa mtandao wa Fikra za Kitajiri. Hongera kwa kuendeleza jitihada zinazokusogeza kwenye ukamilisho wa vipaumbele vya maisha yako.

Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA

Karibu katika makala ya leo ambayo ni mwendelezo wa makala iliyohusu kujilipa kwanza. 

Makala iliyopita tuliona jinsi unavyoweza kutumia mbinu ya kujilipa kwanza kujenga tabia ya kuweka Akiba na Uwekezaji. 


Tuliona unaweza kutumia mbinu hii kwa ajili ya kukusanya pesa kwa ajili malengo tofauti.

Katika makala hii tutajifunza mbinu tano ambazo unatakiwa kuzingatia wakati unapoendelea kujilipa kwanza.

Naamini mpaka sasa umedhamiria kujilipa kwanza na tayari umeshaamua kiwango ambacho utakuwa unajilipa kwa siku, wiki au mwisho wa mwezi. 

Pia, umeshaainisha malengo ambayo unahitaji kufanikisha kupitia tabia hii mpya ya kujilipa kwanza. 

Kama majibu yako ni ndiyo karibu ujifunze mambo matano ya kuzingatia katika safari yako mpya:-

Chagua kiwango rafiki kulingana na uwezo wako. Makala iliyopita nilieleza kuwa inashauriwa kutenga kati ya asilimia 10 hadi 20 ya kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba, yaani kwa ajili kiwango unachojilipa. 

Hata hivyo, wakati unaanza asilimia 10 inaweza ionekane kuwa kwako! 

Hali hii huwatokea watu wengi kutokana na ukweli kwamba kujenga tabia mpya ni zoezi gumu ikilinganishwa na kuendeleza tabia ambayo imezoeleka kwako. 

Kujilipa Kwanza ni tabia sawa na zilivyo tabia nyingine, unahitaji kujifunza taratibu hadi iwe sehemu ya mazoea yako. 

Wakati unaanza unaweza kujilipa hata asilimia 5 ya pato lako na hakikisha unafanya hivyo bila kuacha angalau kwa kipindi cha mwaka mmoja. 

Baada ya kipindi hicho, angalia kiasi ulichofanikiwa kukusanya na jiulize kama ni utaratibu mzuri wa kuendelea nao kabla ya kuamua kuongeza au kupunguza kiwango cha kujilipa. 

Chagua sehemu salama ya kuwekeza kiasi unachojilipa. Kuna watu wengi ambao hufanikiwa kujilipa kwanza lakini hujikuta katika mtego wa kutumia kiwango wanachojilipa kinyume na malengo yao ya awali. 

Asilimia kubwa ya watu hawana uwezo wa kujizuia kutotumia pesa ambayo ipo sehemu ambako inafikiwa kirahisi. 

Kuna watu wanakusanya pesa kwa malengo maalumu kwa kuidumbukiza kwenye kibubu lakini ghafla kibubu huvunjwa kabla ya muda uliokusudiwa awali. 

Wapo watu ambao hufungua akaunti ya benki na kukusanyia pesa huko lakini kwa kuwa kadi ya benki inakuwa mikononi mwao hujikuta wametoa hela yote na kuidumbukiza kwenye matumizi mengine nje ya malengo ya awali. 

Kumbe, ili ufanikiwe kujilipa kwanza na kutimiza malengo yako ni vyema pesa unayojipa iwekwe kwenye akaunti maalumu yenye masharti yanayokubana. 

Mfano, benki nyingi zina akaunti maalumu ambazo unaruhusiwa kukusanyia pesa yako na huruhusiwi kuchukua pesa hiyo mpaka kipindi cha mwaka au zaidi. 

Sehemu nyingine ambapo unaweza kuwekeza pesa unayojilipa ni Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (Kwa hapa kwetu UTT AMIS). 

Muhimu! Iwe benki katika akaunti maalumu au sehemu yoyote ile, unashauriwa kuwekeza pesa yako sehemu ambako kuna ongezeko la riba (interest).

Ainisha kipindi cha Uwekezaji au Akiba unayokusudia kujilipa kwanza. Hapa unatakiwa kujua ni kiasi gani unahitaji kukusanya kadri unavyojilipa na kwa muda gani. 

Yawezekana unakusanya hela kwa ajili ya mpango wako wa kustaafu! 

Yawezekana unakusanya hela kwa ajili ya masomo ya chuo kikuu kwa mwanao ambaye yupo shule ya msingi kwa sasa! 

Yawezekana unakusanya kusanya mtaji kwa ajili ya kuanzisha biashara! 

Yawezekana unakusanya pesa kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa nyumba au kununua gari! 

Kwa ujumla, lengo la kiasi cha pesa unachohitaji kukusanya hupelekea kuamua kipindi maalumu ambacho unatakiwa kujilipa hadi kufanikisha lengo husika.

Mshirikishe Mwenza Wako Kama Yupo. Kama tayari umefanikiwa kumpata mwenza wako hakikisha anakuwa Mshirika wa karibu katika malengo yako ya kujilipa. 

Mshirikishe unakusudia kujilipa kiasi gani na kwa muda gani bila kusahau chanzo cha pesa. 

Mshirikishe malengo ya muda mfupi na muda mrefu katika kukuza pato na miradi ya familia kupitia utaratibu wa kujilipa kwanza. 

Mhamasishe umuhimu wa yeye kuwa upande wako ili kwa pamoja mfanikishe malengo unayokusudia. 

Tunza rekodi. Kumbukumbu ni muhimu kwenye kila shilingi unayojilipa. 

Ikiwa hauna kumbukumbu hauwezi kujua umejilipa kiasi gani na kiasi gani kimezalishwa kupitia ongezeko la riba. 

Pia, kumbukumbu ni njia ya kudumumisha shauku na hamasa ya kuendelea kujilipa kwanza kadri unavyoendelea kujenga tabia mpya. 

Kufanikisha hilo, unashauriwa uwe na utaratibu wa kupitia kumbukumbu zako mara kuwa mara.

NB. Husisite kuwasiliana nami ikiwa unahitaji mwongozo zaidi juu ya jinsi gani unaweza kudhibiti matumizi yako ikilinganishwa na pato lako halisi. Nitumie ujumbe kupitia WhatsApp +255 786 881 155.

WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI 


Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.

Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.

UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Tumia Siri Hii Kukuza Utajiri Wako

NENO LA SIKU_FEBRUARI 26/2022: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Tumia Siri Hii Kukuza Utajiri Wako.
Hongera rafiki yangu kwa siku ya leo. Naamini siku hii imeitumia kwa faida kwa ajili ya kuendelea kuboresha maisha yako. Hata kama kuna changamoto kadhaa umekutana nazo husife moyo na badala yake jipe moyo mkuu kwa ajili ya kuendelea kusonga mbele.

Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA

Karibu katika makala ya leo ambapo nitakushirikisha siri nyingine ambayo itakuwezesha kukuza utajiri wako. 

Makala zilizopita nilikushirikisha siri ya kwanza ya kutengeneza utajiri ambapo nilikutaka kuhakikisha unatenga kati ya asilimia 10 hadi 20 ya pato lako. Kupitia siri hiyo nilikushirikisha umuhimu wa kutenga bajeti binafsi inayoendana na pato lako halisi.


Kupitia siri ya kwanza tunapata siri ya pili ambayo matajiri hutumia kukuza utajiri wao. Siyo mara kwanza kuandika kuhusu siri hii, hila kwa kuwa kipindi hiki nimedhamiria kukushirikisha siri zote za kukuza utajiri wako inabidi nirudie tena kukumbusha. 

Siri hii inasema; "kabla ya kutumia unatakiwa kutenga pesa kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba." Siri hii hujulikana pia kama "KUJILIPA KWANZA." 

Nilijifunza siri hii kupitia vitabu viwili vya Robert Kiyosaki (Rich Daddy, Poor Daddy na Rich Daddy's Conspiracy of Rich). 

Hata hivyo, siri hii imeandikwa kwenye vitabu vingi vya uhamasishaji wa mafanikio japo ni watu wachache sana wanaotumia siri hii. 

Kutokana na hilo, haishangazi kuona idadi ya matajiri katika jamii ni ndogo ikilinganishwa na masikini au watu pato la kati. Kadri unavyoifahamu siri hii na kuitumia mapema ndivyo itatenda muujiza kiasi cha kujuta kwa nini umekuwa ukijichelewesha mwenyewe.

Kujilipa kwanza si kingine zaidi ya kuhakikisha kila shilingi inayoingia mikononi mwako unatenga asilimia maalumu kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba. 

Katika siri ya kwanza tuliona kuwa inashauriwa kiasi unachojilipa kiwe kati ya asilimia 10 hadi 20. 

Kwa wale ambao wameajiriwa katika sekta rasmi wanaweza kutengeneza mfumo wa moja kwa moja (automatic system) ambao unawezesha kiasi cha kujilipa kwanza kiingizwe kwenye akaunti maalumu ya Uwekezaji na Akiba bila kuingizwa kwenye akaunti ya mshahara. 

Hata hivyo, haizuii kuhakikisha wanajilipa kwanza kwenye kila shilingi inayoingia mikononi mwao nje ya mshahara. 

Pia, Wafanyabiashara nao wanaweza kujilipa kwanza kwa kuhakikisha kila mwezi wanatenga pesa ya Uwekezaji na Akiba kabla ya matumizi mengine.  

Kwa nini siri hii ni mkombozi kwako? 

Wakati ambao unaendelea kuhoji kuhusu umuhimu wa siri hii kwenye maisha yako, naomba uwe mkweli kujibu maswali haya; 

Je, una akiba kiasi gani? Je, leo hii ukipata dharura ya kawaida unaweza kuitatua bila mkopo au bila utegemezi kutoka kwa watu wengine? 

Je, ikitokea unaachishwa kazi au unashindwa kuendelea na kazi ikiwa ni miongoni mwa watu wengi ambao ili wape mkate ni lazima watoke na kufanya kazi utaweza kumudu gharama za kuishi? 

Kama majibu ya maswali hayo ni HAPANA au una WALAKINI, Siri ya JILIPE KWANZA imefika tena mezani mwako! 

Mtu yeyote ambaye hana utaratibu wa kutenga akiba, ni dhahiri kuwa hana pesa za kutosha kwa matumizi ya siku zijazo. 

Siri ya kujilipa kwanza inataka ikuondoe kwenye kundi la watu wa aina hiyo. Ukiachana na dharura, kuna fursa ambazo utazikosa kwa kuwa huna Akiba ya kutosha. 

KUJILIPA KWANZA ni kanuni ya dhahabu itakayowezesha kuwa na akiba yenye kuongezeka kulingana na ongezeko la pato lako. 

Ili uweze kutumia Kanuni hii kwa faida, unachotakiwa kufanya ni kujitoa kila mara kutenga akiba kabla ya kutumia. 

Kabla ya kulipa bili zako, kununua chakula, kulipa ada ya watoto wako, au kulipia king'amuzi cha TV unapaswa KUJILIPA KWANZA. 

Kiwango unachojilipa inabidi iwe ni bili ya kwanza ambayo lazima uilipe na kisha ndiyo upange matumizi mengine. 

Kufanikisha hilo, unapaswa kuongozwa na nidhamu binafsi. 

Siri hii inaweza kuonekana rahisi lakini kama hauna nidhamu binafsi hutofanikiwa kujilipa kwanza. 

Nidhamu binafsi ndiyo nyenzo ambayo itakuwezesha kuona kiasi unachojilipa kama deni tena ambalo husipolipa madhara yake ni makubwa. 

Nihitimishe kwa kusema; nje ya siri hii kukuwezesha kukuza utajiri wako, kuna faida nyingi unapoamua siri hii iwe sehemu ya maisha yako. 

Moja, kupitia kujilipa kwanza utakuwa na uhakika na mwendelezo wa kutenga akiba. 

Pili, kujilipa kwanza ni njia bora ya kutenga akiba kwa ajili ya kuwezesha manunuzi makubwa kwa kadri ya mpango wako, ujenzi au kutenga akiba ya kusomesha watoto wako. 

Tatu, kwa kujilipa kwanza unaweza kukusanya mtaji wa biashara. 

Nne, kwa kujilipa kwanza unaweza kutenga fedha kwa ajili ya kipindi chenye mahitaji makubwa ya pesa kama vile nyakati za likizo au kutembelea sehemu kufurahi maisha na familia. 

NB. Husisite kuwasiliana nami ikiwa unahitaji mwongozo zaidi juu ya jinsi gani unaweza kudhibiti matumizi yako ikilinganishwa na pato lako halisi. Nitumie ujumbe kupitia WhatsApp +255 786 881 155.

WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI 


Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.

Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.

UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Fahamu Mambo Ya Kuzingatia Unapoandaa Bajeti Binafsi

NENO LA SIKU_FEBRUARI 25/2022: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Fahamu Mambo Ya Kuzingatia Unapoandaa Bajeti Binafsi  


πŸ“ŒRafiki yangu naamini unaendelea vyema katika kutekeleza majukumu yako ya leo. Hongera kwa kuendeleza moto wa mafanikio kupitia yote ambayo umefanikisha katika ratiba yako ya leo. Hata kama umekutana na changamoto, husife moyo endeleza shauku ya kutaka kufikia kilele cha malengo yako.


Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA

πŸ“ŒMakala ya leo ni mwendelezo wa kujifunza kuhusu bajeti binafsi kama msingi namba moja wa kuwezesha ukuaji wako kiuchumi. Katika makala zilizopita tulijifunza Kanuni muhimu ya kuzingatia wakati wa kuandaa bajeti binafsi inayoendana na pato lako halisi. Tuliona jinsi unavyotakiwa kugawanya pato lako katika makundi matatu ya matumizi; mahitaji ya lazima (50%), mahitaji ya ziada au yasiyo ya lazima (30%) na Uwekezaji/Akiba.


SOMA: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Jifunze Zaidi Kanuni Ya 50/30/20


πŸ“ŒKatika makala hii tutajifunza mambo saba ya kuzingatia wakati unapoandaa bajeti yako. Vitu hivi ni maandalizi ya awali ambayo endapo utayazingatia yatakuwezesha uandae bajeti inayotekelezeka. Muhimu! Tukumbuke lengo zima la bajeti binafsi ni kukupatia dira ya jinsi gani unatakiwa kuelekeza pato lako kwenye matumizi mbalimbali. Hivyo, kupitia bajeti unatakiwa kutambua sehemu ambako hela zako huwa zinaelekezwa. Ili ufanikishe lengo hilo huna budi kuzingatia ushauri huu:-


πŸ“ŒKuwa na sababu zinazokusukuma kuandaa bajeti binafsi, Ili ni jambo la msingi wakati unaandaa bajeti binafsi! Bajeti binafsi haipaswi ionekane kana kwamba ni adhabu kwenye matumizi ya pato lako. Ikiwa hauna sababu za msingi zinazokusukuma kuwa na bajeti binafsi, hutoweza kufurahia bajeti hiyo. Katika kipengele hiki unatakiwa kujibu maswali muhimu kuhusu wewe na bajeti yako. Huna budi kuelezea kwa undani malengo makuu ambayo unahitaji yafanikishwe kupitia utekelezaji wa bajeti yako. Ainisha malengo ya muda mfupi na mrefu katika kila sekta ya maisha yako ambayo unahitaji kuona yanatekelezeka kupitia utekelezaji wa bajeti yako.


πŸ“ŒHapa unaweza kujiuliza maswali kama vile: Je! Nina deni ambalo napaswa kulipunguza au kulimaliza kabisa kupitia bajeti hii? Je! Kupitia bajeti hii ninataka akiba kwa ajili ya kukamilisha kitu gani cha msingi? Yawezekana unataka kupitia bajeti ufanikiwe kukusanya mtaji, ujenzi, ada n.k? 


πŸ“ŒChagua maneno ambayo yatakupa hamasa na shauku katika kuitekeleza bajeti yako, pengine neno 'bajeti' halikupi hamasa au msukumo. Kama ndivyo, huna budi kuwa na maneno yako ambayo yatakufanya ufurahie utekelezaji wa bajeti yako katika maisha ya kila siku. Wengi wetu linapotajwa neno bajeti hufikiria maisha ya kujibana, ubahili au uhaba wa pesa. Ikiwa na miongoni mwa watu hao, ni vyema ukawa maneno yako ambayo yatakufanya ufurahie bajeti yako. Unaweza kutumia maneno kama vile mpango wangu wa matumizi, kwa mwezi…, au orodha ya vitu ambako nitaelekeza pesa zangu kwa mwezi…. 


πŸ“ŒChagua mbinu au Kanuni sahihi ya kukuongoza kwenye sehemu za msingi kuelekeza pato lako, mara zote pesa haijawahi kutosha na itaendelea kuwa hivyo mpaka unakufa. Hata wale unaodhania ni mamilionea huwa wanaelekeza pato lao kwenye vitu vya msingi. Hapa ni lazima utambue vipaumbele muhimu vya maisha yako. Katika makala zilizopita tuliona unaweza kutumia Kanuni ya 50/30/20 kama mwongozo wa matumizi ya pato lako. Pia, unaweza kubadilisha kanuni hii kulingana na mahitaji halisi ya bajeti yako. Muhimu! Kumbuka bajeti unayopanga ni kwa ajili ya kufanikisha nini? 


πŸ“ŒAinisha vipaumbele muhimu vya kutengea bajeti, makala zilizopita nilieleza kwa kina maana ya mahitaji ya lazima (needs), mahitaji ya ziada au yasiyo ya lazima (wants) na Uwekezaji/Akiba (investments/savings). Haya ni makundi muhimu ambayo yanapaswa kubeba vipaumbele vyote vya bajeti yako. Hapa unatakiwa kuainisha vipaumbele ambavyo utafurahia kuona pesa inatumika kwa ajili ya ukamilisho wa vipaumbele hivyo. Husiainishe vipengele vya bajeti ambavyo kesho na kesho kutwa utaanza kujuta mara baada ya pesa kutumika. Ainisha vitu ambavyo roho yako inapenda kulingana na maadili, kanuni binafsi au ndoto za maisha yako.


πŸ“ŒAcha nafasi ya dharura, si mara zote mambo yataenda kulingana na mpango wako wa bajeti. Kuna matukio nje ya uwezo wako ambayo yanaweza kuathiri mpango wako wa matumizi. Kuna nyakati mfumuko wa ghafla (inflation) unaweza kuathiri makadirio ya matumizi ya pesa kwenye makundi makuu matatu ya bajeti yako. Kuna nyakati matukio ya asili yanaweza kuathiri mpango wako wa Uwekezaji na akiba. Yote hayo yanakupa nafasi ya kufikiria matukio ya dharura wakati unaandaa bajeti yako. Ili uwe salama na matukio ya aina hii huna budi kuchukua tahadhari mapema.


πŸ“ŒTathimini na rekebisha vipengele vya bajeti yako kila mwezi, ni matumizi yatabadilika mara kadhaa kulingana mahitaji ya mwezi husika. Mfano, matumizi katika mwezi Disemba hayawezi kuwa sawa na matumizi ya mwezi Agosti au Januari. Kuna miezi ya kulipia ada za wanafunzi, kodi za nyumba, likizo au siku kuu. Ili bajeti iwe salama kila mwezi unashauriwa kuipitia bajeti yako kila mwezi.  Pia, bajeti inatakiwa iendane na mabadiliko kwenye mapato yako katika mwezi husika. Miezi ambayo kipato kimeyumba huna budi kupunguza matumizi ambayo siyo ya lazima na hata kutafuta mbadala kwa mahitaji ya lazima. Kama ulikuwa unakaa kwenye nyumba ya gharama unaweza kutafuta nyumba ya gharama nafuu. Kama ulikuwa unafanya manunuzi 'super markets', unaweza kufanya manunuzi yako kwenye masoko ya kawaida. 


πŸ“ŒEpuka kununua kwa mikopo au kuongeza mikopo mibaya,  hapa unatakiwa kuelewa kuwa mikopo ni matumizi ya pato la baadae kwa wakati wa sasa. Maana yake ni kwamba unatumia pato lako la baadae kabla ya wakati wake. Pia, epuka manunuzi unayofanya kwa mikopo yakiwa na ongezeko la bei. Watu wengine wanaingia kwenye mikopo midogo midogo kupitia manunuzi ya bidhaa kutokana na kushawishiwa kuwa watalipa kwa awamu kila mwisho wa mwezi. Wengi huwa hawajui kuwa wauzaji wanakuwa wameongeza bei za bidhaa kama gharama ya kufuatilia malipo. Ili uwe salama huna budi kuepuka mitego ya namna hiyo. Ikiwa unahitaji kununua bidhaa au kitu chochote cha thamani hakikisha unaingiza kwenye mpango wako wa bajeti wa muda mfupi au mrefu. 


πŸ“ŒNahitimisha makala hii kwa kusema, uandaaji na utekelezaji wa bajeti binafsi ni vitu viwili tofauti. Wengi wanaandaa bajeti lakini wanashindwa kuitekeleza. Ili hujitenge kwenye kundi la watu hawa huna budi kuzingatia sehemu muhimu za maandalizi ya awali nilizokushirikisha katika makala hii. Nakutakia kila lenye kheri katika kuandaa na kuitekeleza bajeti yako.


NB. Husisite kuwasiliana nami ikiwa unahitaji mwongozo zaidi juu ya jinsi gani unaweza kudhibiti matumizi yako ikilinganishwa na pato lako halisi. Nitumie ujumbe kupitia WhatsApp +255 786 881 155.


WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI 

Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.

UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Jifunze Zaidi Kanuni Ya 50/30/20

NENO LA SIKU_FEBRUARI 24/2022: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Jifunze Zaidi Kanuni Ya 50/30/20.  



πŸ“ŒHongera rafiki kwa kufanikiwa kuendeleza jitihada za kuboresha maisha yako. Ni siku nyingine ambayo umezawadiwa kwa ajili ya kuendeleza bidii zinazolenga kupata matokeo chanya katika kila sekta ya maisha yako.


πŸ“ŒNinafurahi kusikia ushuhuda wako. Nitumie ujumbe ukielezea jinsi ambayo masomo yangu yamesaidia kubadilisha maisha yako. Unaweza kutuma ujumbe wako kupitia barua pepe fikrazakitajiri@gmail.com au WhatsApp namba +255 786 881 155. Ujumbe wako ni muhimu sana katika kufanikisha uendelevu wa masomo haya. 

Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA


πŸ“ŒKaribu katika makala ya leo ambayo ni mwendelezo wa kujifunza kuhusu jinsi gani unaweza kutenga bajeti binafsi.


πŸ“ŒMakala ya leo ni mwendelezo wa makala ya jana hasa kwenye jinsi gani unaweza kutumia Kanuni ya 50/30/20 kuratibu matumizi ya pato lako.


SOMA: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Fahamu Mbinu Ya Kubajeti Pesa Zako.


πŸ“ŒKuelewa vizuri jinsi unavyoweza kutumia Kanuni hii katika kudhibiti matumizi yako huna budi uelewe maneno haya; 'Needs'; 'Wants' na 'Savings/Investments'. 


πŸ“ŒNEEDS - Katika makala ya jana nilitumia maneno ya kiswahili "matumizi ya lazima" kujumuisha matumizi yote yanayoingia ndani ya kundi hili.


πŸ“ŒKwa ujumla, haya ni matumizi ambayo ni ya lazima katika kufanikisha uendelevu wa maisha yako.


πŸ“ŒHaya ni matumizi ambayo huwezi kuyakwepa, yaani pasipo gharama hizo huwezi kuishi au utakosa haki zako za msingi.


πŸ“ŒMatumizi haya yanaweza kujumuisha; 

  • Kodi ya kila mwezi,

  • Bili za umeme na maji

  • Usafiri

  • Bima (afya, gari, au kipenzi)

  • Chakula na vinywaji vya lazima

  • Ada za wanafunzi

  • Kulipia madeni ya lazima kama vile mikopo ya benki au SACCOS, Loan Boards n.k


πŸ“ŒIkiwa unatumia Kanuni ya 40/30/20 kupanga bajeti binafsi, kundi hili linatakiwa kutengewa 50% ya pato lako baada ya kodi.


πŸ“ŒWANTS - Kwenye  makala ya jana nilitumia maneno "matumizi yasiyo ya lazima, starehe au matumizi ya ziada".


πŸ“ŒKatika kundi hili kuna matumizi yanayokufanya ufarahie kuishi. Ni matumizi ambayo siyo lazima yapatikane ili uendelee kuishi. Unaweza kukosa matumizi haya na maisha yako yakaendelea kama kawaida.


πŸ“ŒNi kundi linalojumuisha matumizi kama vile:-

  • Mtoko wa kifamilia kwa ajili ya chakula cha jioni au kuburudika zaidi

  • Manunuzi ya nguo mpya

  • Vifurushi vya kuangalia chaneli za TV au vifurushi vya simu

  • Unywaji wa vilevi katika kumbi za starehe

  • Vyakula vya bei ya gharama

  • Manunuzi kwenye maduka gharama


πŸ“ŒNjia rahisi ya kutofautisha 'needs' na 'wants' ni kujiuliza hivi nikikosa kulipia huduma hii nitashindwa kuendelea na maisha? Au mara zote jiulize, Je! ni upi mbadala wa huduma hii? 


πŸ“ŒMfano, kama nimezoea kununua nguo kwenye duka ambalo gharama ipo juu, unaweza kununua nguo ya ubora huo huo kwenye maduka ya hadhi ya kawaida.


πŸ“ŒBadala ya kwenda kula chakula hoteli ya gharama, kula kwenye hoteli yenye hadhi ya kawaida. Kwa kufanya hivyo unaweza kuokoa ongezeko la zaidi ya asilimia 20 kwenye manunuzi ya mwezi.


πŸ“ŒKWA mujibu wa Kanuni ya 50/30/20 tuliona kuwa kundi hili linatakiwa kutengewa asilimia 30 ya pato lako. Hila katika makala ya jana tuliona kuwa unaweza kupunguza gharama katika kundi hili na kuongeza kwenye kundi la Uwekezaji na Akiba.


πŸ“ŒSAVINGS/INVESTMENTS - Kwenye makala ya jana nilitumia maneno "Uwekezaji na Akiba" kuelezea matumizi katika kundi hili. Ni kundi muhimu kwa ajili ya kukuza pato lako, yaani kukuza utajiri wako.


πŸ“ŒKatika kundi hili unatakiwa kutenga bajeti itakayokuwezesha kuwa na akiba kwa ajili ya fursa za uwekezaji zinazoweza kujitokeza. Hata hivyo, unatakiwa kuhakikisha fursa hizo ziwe zinaendana na Mpango wako wa Uwekezaji.


πŸ“ŒPia, kundi hili linajumuisha akiba kwa ajili ya matukio ya dharura au siku ambazo unaweza kushindwa kuendelea kufanya kazi. Hivyo, unaweza kutumia kundi hili kufanya maandalizi siku ambazo hutashindwa kufanya kazi au pindi utakapostaafu.


πŸ“ŒNi kundi ambalo unatakiwa kuwa na mpango wa Uwekezaji wa muda mfupi (mwezi, mwaka) na muda mrefu (miaka mitano na kuendelea). 


πŸ“ŒZaidi ya yote, katika kundi hili takribani 10% ya pato lako (50% ya kundi hili) inatakiwa itengwe kwa ajili ya  kurudisha kwenye jamii kwa njia ya sadaka.


πŸ“ŒInashauriwa pesa unayotenga kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba iwekwe kwenye akaunti maalumu ya Akiba/Uwekezaji au iwekezwe kwenye Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja, kwa hapa kwetu unaweza kuwekeza katika Mifuko ya UTT AMIS.


πŸ“ŒBaada ya ufafanuzi wa kina kuhusu Kanuni ya 50/30/20 unachotakiwa kufanya hatua ya kwanza ni kujua pato lako halisi baada ya kuondoa kodi katika kipindi maalumu cha bajeti yako.


πŸ“ŒKama wewe ni mfanyabiashara, hakikisha unajua faida yako kwa kipindi hicho maalumu baada ya kuondoa kodi ya Serikali, pango la framu gharama za wasaidizi. Kiasi kinachobakia ndilo pato halisi unalotakiwa kuliingiza kwenye Kanuni ya 50/30/20.


πŸ“ŒKama umeajiriwa katika sekta rasmi, kwako ni rahisi maana pato lako ni pesa halisi baada ya makato inayoingizwa kwenye akaunti yako ya benki kila mwisho wa mwezi (take home).


πŸ“ŒHata hivyo, kuna makato ambayo unatakiwa uyarejeshe kwenye pato lako kabla ya kuingiza kwenye Kanuni. Mfano, makato ya bima ya afya, malipo ya mikopo ya madeni makubwa ya benki au Loan Board.


πŸ“ŒBaada ya kupata pato lako halisi hatua inayofuata ni kuingiza kwenye Kanuni ya 50/30/20. Kumbuka, malipo ya madeni makubwa au bima ambayo umeyarejesha kwenye pato lako yanatakiwa yaingizwe katika kundi la kwanza, yaani kundi la matumizi ya lazima (50%).


πŸ“ŒHatua ya pili baada ya kutambua pato lako halisi katika kipindi maalumu cha bajeti ni kugawanya matumizi yako kulingana na makundi matatu tuliyojifunza hapo juu, yaani needs, wants na Savings/investments.


πŸ“ŒKufanikisha zoezi hili, unaweza kupitia matumizi yako kwa miezi ya iliyopita. Angalia ni matumizi yapi huwa yanajirudia katika miezi kadhaa na tambua kila tumizi linaangukia kwenye kundi lipi kati ya makundi matatu.


πŸ“ŒBaada ya zoezi hili unatakiwa kufahamu kiasi cha pesa kinachotumika kugharamia Chakula, Afya, Kodi, Ada, Ankara za maji na umeme, usafiri, mawasiliano, malipo ya ving'amuzi au starehe.


πŸ“ŒKisha tenga matumizi yote uliyoainisha katika makundi matatu; mahitaji ya lazima, mahitaji ya ziada au Uwekezaji na Akiba. 


πŸ“ŒHatua ya mwisho, tathimini ni sehemu zipi unapaswa kurekebisha ili upate kukidhi matakwa ya Kanuni ya 50/30/20 kwa ufasaha.


πŸ“ŒNjia bora ya kufanya hivyo ni kutathmini ni kiasi gani unatumia kwa kila kundi kutoka kwenye tathimini ya matumizi uliyofanya kwa miezi iliyopita.


πŸ“ŒHakikisha 50% ya pato lako inatengwa kwa ajili ya kugharamia mahitaji ya lazima, 30% au pungufu itengwe kwa ajili ya mahitaji ya ziada, na 20% ielekezwe kwenye akaunti maalumu ya Uwekezaji na Akiba.


πŸ“ŒNihitimishe kwa kukumbusha kuwa, Kanuni ya 50/30/20 hurahisisha upangaji bajeti kwa kugawa mapato yako ya baada ya kodi katika makundi matatu ya matumizi: mahitaji ya lazima, mahitaji yasiyo ya lazima na Uwekezaji au Akiba.


πŸ“ŒKujua ni kiasi gani cha kutumia kwa kila kundi kutarahisisha kudhibiti matumizi yako na kuwezesha kuondoa matumizi ya hovyo. 


πŸ“ŒNB. Husisite kuwasiliana nami ikiwa unahitaji mwongozo zaidi juu ya jinsi gani unaweza kudhibiti matumizi yako ikilinganishwa na pato lako halisi. Nitumie ujumbe kupitia WhatsApp +255 786 881 155.


WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI 


Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.

UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Fahamu Mbinu Ya Kubajeti Pesa Zako.

NENO LA SIKU_FEBRUARI 23/2022: Fahamu Mbinu Ya Kubajeti Pesa Zako.  
πŸ“ŒHabari rafiki yangu na hongera kwa kuendelea kufuatilia masomo ya mtandao wa Fikra za Kitajiri. Naamini masomo haya yamesaidia kukubadilisha kifikra na kivitendo.

πŸ“ŒSiku ya leo nahitaji kusikia ushuhuda wako. Nitumie ujumbe ukielezea jinsi ambayo masomo yangu yamesaidia kubadilisha maisha yako. Unaweza kutuma ujumbe wako kupitia barua pepe fikrazakitajiri@gmail.com au WhatsApp namba +255 786 881 155. Ujumbe wako ni muhimu sana katika kufanikisha uendelevu wa masomo haya. 

Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA

πŸ“ŒKatika makala ya jana tulijifunza siri ya kwanza ya kutengeneza utajiri wa ndoto yako. Tuliona kuwa siri hiyo inahusisha kutenga kati ya asilimia 10 hadi 20 kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba.


πŸ“ŒHata hivyo, niligusia kuwa hauwezi kufanikisha kutenga pesa kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba ikiwa hauna utaratibu maalumu wa kudhibiti mapato yako. Katika hilo, niligusia kuwa njia pekee itakayokuwezesha kudhibiti matumizi yako ni kuhakikisha unakuwa na bajeti ya matumizi inayoandaliwa kulingana na uhalisia wa pato lako.

πŸ“ŒMakala ya leo inalenga kukufungua kuhusu bajeti na gani vitu vya msingi vya kuzingatia wakati unaandaa bajeti yako.

πŸ“ŒJe! Bajeti ni nini? Bajeti ni mpango wa matumizi unaoandaliwa kwa ajili ya kutoa dira ya matumizi ya kila shilingi kwenye pato lako. Bajeti uandaliwa kwa kipindi maalumu kama vile siku, wiki, mwezi au mwaka.

πŸ“ŒMfano, ikiwa pato langu kwa mwezi baada ya kutoa kodi ya pato (pay as you earn) ni Tshs. 500,000.00; bajeti binafsi inatakiwa inipatie mwongozo wa jinsi gani natakiwa kusambaza kiasi hiki katika matumizi mbalimbali kama vile; mahitaji ya chakula, kodi ya nyumba, ada ya wanafunzi, bima ya afya au bima ya kinga ya mali dhidi ya ajali, kulipa madeni kama yapo, na matumizi ya starehe au tunaweza kutumia jina la matumizi yasiyo ya lazima.

πŸ“ŒJe! Ni mbinu ipi niitumie kurahisisha upangaji wa bajeti binafsi? Kabla ya kuandaa bajeti binafsi unatakiwa kufanya jambo hili la msingi.

πŸ“ŒHakikisha unakokotoa pato lako halisi kwenye kila mfereji wako wa mapato katika kipindi maalumu cha bajeti yako. Yaani, hakikisha unafahamu pato lako kwa mwezi au wiki kulingana na urefu wa kipindi unachobajetia. Kama ni kwa mwaka hakikisha unatambua makadirio ya mapato yako kwa mwaka.

πŸ“ŒBaada ya kuwa na makadirio halisi ya pato lako kwa kipindi maalumu cha bajeti unaweza kutumia kanuni iliyopendekezwa na aliyekuwa Senator wa US Elizabeth Warren na binti yake Amelia Warren Tyagi katika kitabu cha kijulikanacho kama "All Your Worth: The Ultimate Lifetime Money Plan.” 

πŸ“ŒKanuni hii inajulikana kama 50/30/20, ikamaanisha kuwa; 50% ya pato pako lako inatakiwa kutengwa kwa ajili mahitaji ya lazima (basic needs).

πŸ“ŒTenga 30% ya pato lako kwa ajili ya mahitaji ya ziada au starehe au mahitaji yasiyo ya lazima. Haya ni mahitaji yote ambayo pindi unapoyakosa hauwezi kushindwa kuendelea kuishi.

πŸ“ŒKisha tenga 20% ya pato lako kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba. Pia, kundi hili la 20% sehemu inaweza kuelekezwa kwenye kulipa madeni ikiwa una madeni na sehemu nyingine itengwe kwa ajili ya kurudisha kwenye jamii (sadaka kwa wahitaji). Mara nyingi inashauriwa 10% ya pato lako (kundi la kumi) ndo itengwe kwa ajili ya kurejesha kwenye jamii.

πŸ“ŒUnaweza kuwa mjanja kwa kuongeza bajeti katika kundi hili kwa kupunguza bajeti katika kundi la pili (punguza kwenye 30%). Yaani unaweza punguza matumizi yasiyo ya lazima na kuongezea kwenye kundi la Uwekezaji na Akiba.

πŸ“ŒNihitimishe kwa kusema; utaratibu wa bajeti binafsi ni njia pekee ambayo itakuwezesha kujua sehemu ambazo zinakwamisha pato lako kuongezeka.

πŸ“ŒKufanikisha hilo ni lazima ujenge tabia ya kudhibiti na kuepuka matumizi ya hovyo. Husinunue vitu ambayo havina tija kwako na epuka kununua kwa hisia.

πŸ“ŒKununua kwa hisia mara nyingi hujumuisha kununua wakati ambao umefurahi, kukasirika au kushawishiwa kupitia mbinu za wauzaji. Anza sasa na kumbuka kunishukuru kwa maarifa haya.

NB. Husisite kuwasiliana nami ikiwa unahitaji mwongozo zaidi juu ya jinsi gani unaweza kudhibiti matumizi yako ikilinganishwa na pato lako halisi. Nitumie ujumbe kupitia WhatsApp +255 786 881 155.

WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI 


Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.

JE UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Kama Jibu Ni Ndiyo Anza Kuiishi Siri Hii.

NENO LA SIKU_FEBRUARI 22/2022: JE UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Kama Jibu Ni Ndiyo Anza Kuiishi Siri Hii.



πŸ“ŒNi siku nyingine tumejaliwa pumzi ya uhai. Ni siku ya kutekeleza majukumu ya msingi hasa yale yanayochangia kwenye ukamilisho wa maisha yenye thamani. Naamini unaendelea vyema na majukumu hayo ili siku yako ipate kutumika kwa manufaa.


Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA


πŸ“ŒKaribu katika makala ya leo ambapo nitakushirikisha siri ya kwanza ambayo matajiri wanaitumia kukuza utajiri wao. Jambo la msingi katika mfululizo wa makala hizi ni kutambua kuwa utajiri unatangenezwa kupitia kanuni maalumu ambazo zimeendelea kuwa siri zinazobadilisha maisha ya watu.


πŸ“ŒLeo siri ya kwanza naifikisha kwenye upeo wako wa fikra, wajibu wako ni kuitafakari na kufanya maamuzi mara moja ili upate kuianza safari yako ya utajiri.  


πŸ“ŒKatika makala ya jana nilikushirikisha mbinu ya awali ya kuishi maisha ya kitajiri. Tuliona kuwa utajiri unaanza kwa kuhakikisha matumizi hayazidi kipato chako.


SOMA: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Fahamu Mbinu Ya Itakayofungua Milango Ya Utajiri


πŸ“ŒNi matarajio yangu kuwa kupitia makala hiyo uliweka mikakati ya kukuwezesha kupunguza matumizi sambamba na kuwa na bajeti inayoendana na pato lako halisi. 


πŸ“Œ Baada ya kudhibiti matumizi yako, Siri ya kwanza itakayobadilisha maisha yako ni "kuhakikisha unatenga angalau kati ya asilimia 10 hadi 20 ya pato lako kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba." 


πŸ“ŒNi kama vile naona jinsi unavyofikiria kichwani kwa kujiuliza nitaweza vipi kutenga asilimia 10 au 20 kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba wakati pato langu lenyewe halitoshi kukidhi mahitaji yangu.


πŸ“ŒNi kuondoe wasiwasi huo kwa kukutaka kwanza ukubaliane na siri hii kuwa inaweza kufanya kazi katika maisha yako kupitia pato lako hilo hilo.


πŸ“ŒKukubaliana na siri hii ni hatua moja muhimu ambayo itakufungua akili na kuweza kuona sehemu zipi katika matumizi yako ambako unaweza kupata asilimia kiasi cha fedha ambayo utaanza kuitenga kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba. 


πŸ“ŒPia, jambo la msingi ambalo unatakiwa kufahamu kuhusu siri hii ni; matajiri kwanza huwa wanatenga kiasi cha pesa kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba kabla ya kufanya matumizi mengine."


πŸ“ŒUnapoanza safari ya kuishi kwa kuitekeleza siri hii unatakiwa kutambua kuwa kiasi cha pesa unachotenga kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba ni deni kwako ambalo linatakiwa kulipwa kabla ya matumizi mengine yote yanayofanikisha mahitaji yako ya lazima.


πŸ“ŒHebu fikiria jinsi ambavyo hujawahi kukosa hela ya kula, kodi ya nyumba, matibabu au ada ya wanafunzi. Vyote hivyo vimepewa nafasi katika akili yako na ndiyo sababu unatumia kila mbinu kuhakikisha vinatekelezwa kwa ufasaha na kwa wakati.


πŸ“ŒKwa nidhamu na mbinu hizo hizo ndivyo unatakiwa kuhakikisha kila mara kiwango ulichopanga kutenga kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba kinapatikana na kutengwa tena kabla ya kuanza matumizi mengine.


πŸ“ŒUnaweza kuanza kwa kutenga hata asilimia 5 ya pato lako kwa siku za mwanzoni ili kujenga tabia ya hiyo na kisha ukaendelea kupandisha kiwango hicho kwa kadri uwezavyo.


πŸ“ŒNihitimishe kwa kusema, kutenga bajeti kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba ni siri ambayo itabadilisha maisha yako ikiwa utachukua hatua sasa. Hakuna siku ambayo utapata pesa ya ziada kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba zaidi hizi unazopata kwa wakati huu.


πŸ“ŒKadri utavyojenga tabia ya kutenga kiasi kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba ndivyo utagundua ulichelewa kuanza kutumia siri hii ambayo itatenda muujiza katika maisha yako.


πŸ“ŒNB. Husisite kuwasiliana nami ikiwa unahitaji mwongozo zaidi juu ya jinsi gani unaweza kudhibiti matumizi yako ikilinganishwa na pato lako halisi. Nitumie ujumbe kupitia WhatsApp +255 786 881 155.



KUJIFUNZA MISINGI YA MAISHA YENYE KUACHA ALAMA; PATA NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI


Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.