VITU 3 AMBAVYO UNATAKIWA KUFANYA KABLA YA KUFIKIA MIAKA 40

NENO LA LEO (JANUARI 29, 2021): VITU 3 AMBAVYO UNATAKIWA KUFANYA KABLA YA KUFIKIA MIAKA 40

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya ambayo tunaendelea kupewa kibali cha kuwa hai. Ni katika siku hii tunakopeshwa masaa 24 ili ndani ya masaa hayo tupate kufanya kitu cha thamani kwa ajili ya ukamilisho wa kusudi la maisha yetu. Wote tunaalikwa kuitumia siku siku hii kwa faida ili mwisho wa siku tupate furaha ya moyo inayotokana na yale tuliyokamilisha.

 Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA 

Katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha vitu vitatu ambavyo unatakiwa kufanya kabla ya kufikia umri wa miaka 40. Tunafahamu kuwa mwanadamu ambaye amezaliwa na mwanamke siku za uhai wake hapa Duniani ni fupi sana. Kutokana na hilo, maisha ya mwanadamu yamegawanywa katika hatua tatu za ukuaji. Kuna kipindi cha utoto ambacho ni kipindi cha kujifunza na kuweka msingi wa maisha yanayofuata; kipindi cha ujana ambacho ni kipindi cha kuishi kwa vitendo yale uliyojifunza na unayoendelea kujifunza; na kipindi cha uzee ambacho ni maalumu kwa ajili ya kupunguza maangaiko na kubakia na kazi nyepesi. Mara nyingi katika jamii nyingi huwa kipindi cha ujana ni kuanzia miaka 18 hadi 45, na baada ya hapo kipindi cha uzee huwa kinafuatia. Kabla ya kuhitimisha miaka 40 kwa maana miaka 5 kuelekea kwenye kipindi cha uzee inashauriwa uwe umefanya mambo haya matatu ambayo ni msingi wa maisha yako yote:-

Msingi #1: Tafuta fursa ambayo kila mtu ameikosa katika eneo lako. Dunia haijawahi kupungukiwa kwa watu ambao wanajua nini wanataka kufanikisha. Vizazi vinakuwepo na kuondoka lakini kila kizazi hakitakosa fursa kwa ajili ya mwendelezo wa historia ya maendeleo ya mwanadamu. Kipindi cha ujana ni kipindi kwa ajili ya kutafuta fursa kwenye kila sekta au fani. Iwe umesoma na kufikia chuo kikuu au hujasoma ikiwa utashindwa kutumia kipindi cha ujana kupata fursa ya kubadilisha historia ya maisha yako hakika husitegemee miujiza katika kipindi cha uzee. Hivyo, katika kipindi cha ujana hakikisha unatafuta fursa iwe kwenye eneo lako la kazi, eneo unaloishi, chuoni na kuhakikisha unakuwa makini kutambua fursa zinazojitokeza kupitia ukuaji wa teknolojia.

Msingi #2: Jifunze jinsi ya kutengeneza pesa. Unaweza kuwa na fursa nyingi lakini zisikusaidie kuwa na uhuru wa kifedha. Ukuaji wa umri unaambatana na ongezeko la mahitaji ya kipesa. Ikiwa unahitaji kufurahia maisha yako iwe kwenye kipindi cha ujana na hata uzee ni lazima ujifunze namna ya kukuza kipato chako. Kama umeajiriwa unatakiwa kutambua kuwa mshahara unaopata katika kipindi cha ujana ni lazima utumike kukuza kipato chako kwa ajili ya kuwa salama katika kipindi cha uzee. Ikiwa umejiajiri kila shilingi unayoipata unatakiwa kuhakikisha sehemu yake inatumika kuzalisha shilingi zaidi. Kwa ujumla, kabla ya kufikia miaka 40 unatakiwa kuwa umeweka mifereji ya uhakika kwa ajili ya kukuwezesha kuishi maisha yenye uhuru wa kifedha kipindi cha maisha yako yote.

Msingi#3: Jifunze jinsi ya kuongoza watu. Mafanikio ya kila aina yanahusisha watu. Hakuna namna utaweza kufanikiwa bila kuhusisha watu kwa maana iwe ni mafanikio kwenye fani yako au biashara ni lazima uhusishe watu. Kwenye tasinia biashara, ukuaji wa biashara unategemea uwepo wa timu imara yenye mchanganyiko wa taaluma mbalimbali. Kabla ya kufikia umri wa miaka 40 unatakiwa kujifunza misingi ya uongozi kwa maana unatakiwa ujue namna ya kuongoza watu. Hakuna mtu ambaye amezaliwa na kujikuta ni kiongozi kwa kuwa uongozi bora unapatikana kwa kujifunza misingi ya uongozi. Unaweza kuwa kiongozi kupitia kuongoza (unajifunza uongozi kutokana na nafasi uliyonayo); unaweza kuwa kiongozi kwa kusaidia watu (hapa unakuwa na mbinu za uongozi japo wewe siyo kiongozi – a leader with no title); uongozi unahusisha kujifunza mbinu za kuongea (kujua nini uongee, jinsi gani uongee na muda upi wa kuongea); na hakikisha unakuwa wa mfano au kioo kuanzia ndani ya familia yako.   

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo nimekushirikisha misingi mitatu ambayo unatakiwa kuwa nayo kabla ya kufikia umri wa miaka 40. Hata hivyo, hakuna wakati ambao umechelewa kujifunza maarifa ambayo unaona ni ya muhimu katika maisha yako. Ikiwa tayari umevuka umri wa miaka 40 makala hii hailengi kukukatisha tamaa bali iwe chachu kwako kuchangamkia fursa zilizopo kulingana na umri wako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

 ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

MEMA NA MABAYA NI SEHEMU YA MAISHA: KWA NINI UNAPOTEZA MUDA KWA HOFU?

NENO LA LEO (JANUARI 28, 2021): MEMA NA MABAYA NI SEHEMU YA MAISHA: KWA NINI UNAPOTEZA MUDA KWA HOFU?

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni ukurasa mpya katika kitabu cha uhai wetu hapa Duniani. Ni katika ukurasa huu wa wazi ambao wote tunaalikwa kuendeleza yenye thamani ili yapate kuunda kitabu cha maisha yetu hapa Duniani. Kila siku ni wito kwa kila mmoja wetu kuhakikisha anatekeleza majukumu ya msingi ambayo kwa ujumla wake yanakamilisha kusudi kuu la maisha yake hapa Duniani.

 Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA 

Katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakukumbusha umuhimu wa kutambua kuwa kipindi cha mwanadamu hapa Duniani kinapitia katika nyakati za neema na nyakati ngumu. Hakuna ajuaye kuwa kesho yake ana uhakika wa kuepukana na ubaya au nyakati ngumu katika maisha yake. Vivyo hivyo, hakuna mwenye uhakika asilimia mia moja kuwa maisha yake yatakuwa na nyakati bora. Zipo nyakati ngumu katika maisha yetu ambazo tunajisababishia wenyewe kwa kujua au kutokujua na zipo nyakati ambazo zinasababishwa na majanga ya asili.

Ni ukweli kwamba kupitia matendo yetu ya kila siku tunaweza kupunguza uwezekano (chances) wa kupatwa matukio yasiyo rafiki katika maisha yetu lakini hiyo siyo tiketi ya kwamba tuna uwezo wa kudhibiti kabisa nyakati hizo zisitokee kwetu. Mfano, katika ajali hakuna ajuaye kuwa kesho itatokea ajali ya bodaboda, gari, treni, meli au ndege. Pamoja na kutokujua siyo kisingizio kuwa watu wasisafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Pia, hakuna anayejua kuwa kesho atapatwa na majanga ya asili kama athari za upepo mkali, mafuriko, ukame au tetemeko la ardhi. Hata hivyo, hiyo siyo tiketi kwa kila mmoja wetu kutulia na kuacha kujishughulisha kwa kuogopa athari za majanga hayo ya asili kwenye shughuli za uzalishaji, makazi au uhai wa mwanadamu.

Kila mmoja wetu katika maisha yake ya akila siku anafahamu namna ambayo amekuwa akipoteza muda kutokana hofu juu ya matukio ambayo haitabiriki yatatokea lini. Wapo watu ambao wanaogopa kuwekeza kwa kigezo cha kuogopa kupoteza pesa zao. Wapo watu ambao wanashindwa kuishi maisha yao kwa kigezo cha kuogopa kufukuzwa kazi. Wapo watu ambao wanashindwa kufanya uwekezaji wa muda mrefu kwa kigezo tu cha kuwa hawana uhakika wa kuishi kwa kipindi cha miaka kadhaa. Hofu kwa matukio ambayo yapo nje ya uwezo wetu wa kuyadhibiti inatawala maisha yetu kila siku. Matokeo yake tunashindwa kuishi maisha yetu kwa ukamilifu kutokana na hofu.

Kwa ujumla, wasiwasi ni zao la hofu. Wasiwasi juu ya matukio au hali ambazo ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya kwako katika siku za baadae hupelekea kuharibu utekelezaji wa mipango kwa ufasaha. Kuendelea kuwa na wasiwasi kwenye hali au tukio husika inapelekea kupoteza muda kutokana na kukosa maamuzi ya haraka kwenye tukio au hali iliyopo mbele yako. Hivyo, kuwa na wasiwasi juu ya siku zijazo hakukusaidia kupata suluhisho bora la shida iliyopo mbele yako na badala yake inapelekea katika hali ya kupingana kifikra juu ya kipi kifanyike bila kupatwa na mabaya.  Hali hii inapelekea kupoteza mawazo ya busara ambayo yangefaa kukupa maamuzi sahihi kulingana na wakati husika.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI  

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumeona kuwa mema au mabaya ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Hakuna anayeweza kujihakikishia maisha yenye matukio mema pekee kwa kuepuka mabaya. Kubwa tunachotakiwa kufanya ni kuepuka kupoteza muda kutokana na kushindwa kuchukua maamuzi kwa wakati sahihi kutokana na kuogopa kupatwa na mabaya. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

 ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

HUU NDIYO URAHIBU (ADDICTION) UNAOITESA DUNIA YA SASA

NENO LA LEO (JANUARI 27, 2021): HUU NDIYO URAHIBU (ADDICTION) UNAOITESA DUNIA YA SASA

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku kipekee ambayo tunaendelea kutumwa katika Dunia hii kukamilisha kusudi kuu la maisha yetu. Safari bado ni ndefu na katika safari hiyo kila siku tunakumbushwa kuifanya njia hiyo rahisi kupitia matendo yetu. Hivyo, kila siku ni ukurasa mpya unaounda kitabu cha siku za uhai wetu hapa Duniani. Kila mmoja wetu ana wajibu wa kuandika vitu vitakavyovutia watu kusoma kitabu chake katika enzi za uhai wake na hata baada ya ukomo wa maisha haya.

 Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA 

Katika neno la tafakari ya leo tutaangalia urahibu unaoitesa Dunia ya sasa. Neno urahibu au addiction kwa lugha ya kingereza linatumika kumaanisha kilele cha ukomavu wa tabia kwa mhusika. Urahibu ni zao la mwisho katika hatua za kujenga tabia mpya. Katika hatua hii mhusika anajikuta anatekeleza au kufanya tukio pasipo kupitia kwenye mlolongo wa ubongo kufanya maamuzi. Hivyo, mhusika anajikuta katika hali ambayo hawezi kujizuia kutekeleza tabia husika. Katika hali kama hiyo, mhusika anapoteza uwezo wa kung'amua mambo, ubunifu na hata uwezo wa kujitegemea.

Siku za nyuma tulizoea urahibu kama vile matumizi ya bangi, madawa ya kulevya, sigara na matumizi ya vilevi. Urahibu huu tofauti na urahibu wa sasa ulihusisha idadi ndogo ya watu katika jamii na athari zake zilikumba makundi machache ya watu. Mfano, katika jamii tulizoea vijana wanaathirika zaidi na matumizi ya dawa za kulevya au bangi ikilinganishwa na makundi mengi ya watu. Tafsiri yake ni kwamba walioathirika na urahibu katika jamii walikuwa wachache ukilinganishwa na urahibu wa sasa.

Ulimwengu wa sasa unakibiliwa na urahibu wa mitandao ya kijamii (social media addiction) na athari zake ni nyingi ikilinganishwa na athari za urahibu katika historia ya maendeleo ya mwanadamu. Tofauti ya urahibu wa sasa na urahibu uliozoeleka hauchagui kundi la watu. Iwe wasomi au ambayo hawajasomo wote wanaangamia. Iwe vijana, wazee na hata watoto wote wanazama ndani ya kundi hili. Jamii ya sasa inahusudu mitandao ya kijamii (Facebook, Instagram, Twitter na mingineyo) kuliko inavyofanya kwa vitu vya msingi.

Kutokana na ukomavu wa urahibu huu kwa sasa ni kawaida kukuta katikati ya majadiliano ya msingi baadhi ya watu wapo bize na kuperuzi simu zao. Tunashuhudia wanafamilia wanakosa muda wa kuwa karibu na wapendwa wao lakini wanapata muda wa kuperuzi kwenye mitandao. Tunashuhudia kizazi ambacho ubunifu unapungua kutokana na athari za kuwaza kuingia kwenye mitandao ya kijamii. Tunashuhudia kizazi ambacho hakiwezi kusoma kitabu cha maarifa mbalimbali au kushika kitabu cha maandiko matakatifu lakini ndani ya mitandao ya kijamii kila kitu kinawezekana.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI  

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumeona kuwa Dunia ya sasa inakabiliwa na urahibu ambao utaendelea kutesa makundi yote ya watu. Watoto, Vijana, Wazee au akina baba na akina mama wanaendelea kuangamia na urahibu huu ikilinganishwa na rahibu zilizozoeleka siku za nyuma. Ni wakati sahihi wa kupima matumizi ya mitandao ya kijamii katika ratiba yako ya siku. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

 ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

FAHAMU CHANZO HALISI CHA MSONGO WA MAWAZO

NENO LA LEO (JANUARI 26, 2021): FAHAMU CHANZO HALISI CHA MSONGO WA MAWAZO

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambayo tunaalikwa kuendelea kufanya yale yanayoboresha maisha yetu. Kila siku asubuhi tunaalikwa kujiuliza swali hili: ni ipi ajenda yangu ya msingi katika siku hii leo? Majibu ya swali hili yanakupatia majukumu ya kukamilishwa katika siku husika. Hata hivyo, unayofanya kila siku yanatakiwa kuwa na mwendelezo siku hadi siku.

 Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA 

Katika neno la tafakari ya leo tutaangalia chanzo halisi cha msongo wa mawazo katika maisha ya watu wengi. Katika Ulimwengu wa sasa tunashuhudia ongezeko kubwa la watu katika jamii ambao wanaishi kwa msongo mkubwa wa mawazo. Hali hii inaweza kuthibitishwa kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya wanaojiua kwa sumu, kujinyonga au kwa jinginezo. 

Sababu zipo nyingi ambazo zinapelekea msongo wa mawazo kwa idadi kubwa ya watu katika jamii. Moja ya sababu ni kukua kwa teknolojia ya mawasiliano ambayo imepelekea mmonyoko wa maadili katika jamii. Pia, sababu nyingine ni kupanda kwa gharama za maisha katika ulimwengu wa sasa ikilinganishwa siku za nyuma. Vyote hivi kwa pamoja vimepelekea mafarakano ndani ya familia hali inayopelekea ongezeko la msongo wa mawazo kwa wahusika. Je pamoja na hayo ni kipi ambacho unahisi kimekuwa chanzo cha msongo wa mawazo kwako?

Je msongo wa mawazo unatokana na Mkuu wako wa kazi?, Je msongo wa mawazo umekuwa ukisababishiwa na mwenza wako? Je msongo wa mawazo unatokana watoto wako?  He msongo wa mawazo unatokana na changamoto za kiafya? Je msongo wa mawazo umetokana na msongamano wa magari barabarani? Je msongo wa mawazo unatokana na watu wanaokuzunguka? Je msongo wa mawazo unatokana na mahitaji makubwa ya kipesa? Je msongo wa mawazo unatokana na mwenye nyumba yako?

Tunaweza kuorodhesha sababu nyingi kama chanzo cha msongo wa mawazo lakini ukweli utabakia kuwa chanzo halisi cha msongo wa mawazo kipo ndani mwako. Chanzo halisi cha msongo wa mawazo ni fikra. Jinsi unavyoitikia sababu zote hizo zilizoorodheshwa katika mfumo wako wa fikra ndicho kinapelekea uwe na msongo wa mawazo. Unaweza kuamua kuwa na mtazamo chanya au hasi katika kila hali inayokuzunguka. Unavyokuwa na mtazamo hasi kwenye changamoto iliyopo mbele yako inapelekea kuwa na msongo na hatima yake ni kuharibu mfumo mzima wa maisha yako.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumeona kuwa chanzo halisi cha msongo wa mawazo ni fikra. Fikra hasi hupelekea mtazamo hasi na hatima yake ni msongo wa mawazo. Anza sasa kuwa na fikra chanya kwenye kila hali inayokukabili. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

JE UNAYAFAHAMU HAYA KUHUSU MALEZI YA MWANAO?

NENO LA LEO (JANUARI 25, 2021): JE UNAYAFAHAMU HAYA KUHUSU MALEZI YA MWANAO?

Habari ya leo rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku ya kwanza ya juma ambayo ni matarajio yangu kuwa umeianza siku kwa kutekeleza yale ambayo yanakupa muunganiko wa matokeo kila siku. Furaha ya mwanadamu inapatikana pale ambapo anajivunia mafanikio ambayo ni zao la kazi halali kupitia majukumu yake ya kila siku. Hakikisha katika siku hii ya leo umetumia kazi yako kueongeza kilele cha furaha yako katika maisha ya kila siku.

 Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA 

Katika Makala maalumu ya leo nitakushirikisha vitu muhimu unavyotakiwa kuzingatia ikiwa wewe ni mzazi au mlezi au unategemea kuwa na majukumu hayo katika kipindi cha uhai wako hapa Duniani. Kwanza kabisa kama mzazi/mlezi unatakiwa kutambua kuwa tupo kwenye kipindi cha mapinduzi ya teknolojia ya habari. Kipindi hiki kinakutaka mzazi/mlezi uwe macho kuliko vipindi vilivyotangulia kutokana na ukweli kwamba Dunia yote imefunuliwa kwenye macho ya Watoto wako. Ikiwa utashindwa kutimiza wajibu wako, Dunia itawafundisha wanao tabia ambazo zitakusonenesha katika kipindi chote cha uhai wako.

Ni katika kipindi hiki cha mapinduzi ya teknolojia ya habari mzazi/mlezi unatakiwa kufahamu kuwa mtoto anahitaji kufundishwa kujifunza vitu vingi zaidi ya kile alichosomea. Hivyo, ukiwa mzazi/mlezi unatakiwa kufahamu kuwa wewe ni walimu namba moja kwa mwanao. Mzazi/mlezi unapaswa kutambua kuwa elimu inayotolewa haijitoshelezi kwa ajili ya kufanikisha maisha ya mwanao. Hivyo, mtoto anahitaji kufundishwa misingi muhimu ya maisha ya mafanikio ikiwa ni pamoja na elimu ya fedha ambayo haifundishwi kwenye mitaala ya shule zetu.

Je mtoto anapotezea wapi uwezo/akili ya kuzaliwa? Watoto wote wanazaliwa wakiwa tajiri na akili nyingi. Kadri mtoto anavyozidi kukua ndivyo anapoteza uwezo wake na akili ikilinganishwa na enzi za kuzaliwa kwake. Mara Watoto wengi wanapoteza uwezo wao kutokana na mazingira wanayokulia. Mazingira hayo yanahusisha kauli wanazoambaiwa na wazazi/walezi, walimu, ndugu na jamii inayowazunguka.

Je mzazi/mlezi unalinda vipi uwezo wa mwanao katika kufikiri na kununi? Katika ukuaji mtoto anatakiwa afundishwe umuhimu wa kufahamu kuwa katika maisha hakuna jibu sahihi. Jibu la HAPANA au NDIYO yote ni majibu sahihi ikitegemewa na namna muhusika anavyosimama kutetea jibu lake. Hii ni elimu ambayo mtoto ataipata kwa wazazi pekee kwani elimu ya sasa inalenga kwenye kutambua watoto wanaoweza kutoa majibu sahihi na kuwafanya wengine waonekana hawana uwezo.

Mtoto anahitaji kufundishwa kwa vitendo. Elimu ya sasa inajikita zaidi kwenye nadharia kuliko vitendo, elimu hii imepelekea kuzalisha vijana wengi ambao darasani wanafaulu kwa viwango vya hali ya juu japo katika maisha mafanikio yao ni ya kawaida. Hii ni kutokana na ukweli kwamba elimu ya sasa inazalisha watu ambao wanaweza kuelezea kwa kina mbinu mbalimbali kwa nadharia wakati hawajawahi kutumia mbinu husika katika maisha yao. Wajibu wako kama mzazi/mlezi ni kumfandisha mwanao kupitia shughuli unazofanya. Kama unamiliki biashara hakikisha wanao wanajua misingi ya kusimamia na kuendesha biashara husika.

Je mzazi/mlezi unamuandaaje mwanao kwenye elimu isiyokuwa na mwisho? Mtoto anatakiwa kutambua kuwa elimu ya kweli inaanzia pale anapomaliza masomo yake. Mtoto anahitaji kuandaliwa kwa ajili ya kuendelea kujifunza katika kipindi chote cha maisha yake. Hii ni kutokana na ukweli kwamba watoto wengi wanapomaliza masomo yao wanaona kuwa ndo mwisho wa kujifunza. Hali hii imepelekea jamii kuendelea kuwa na watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri na kungamua mambo kwa kuwa nadhari walizosoma shuleni hazi nafasi katika maisha ya kila siku.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa tupo jinsi tulivyo kutokana na athari ya malezi na makuzi tuliyopewa kutoka kwa wazazi/walezi. Hata hivyo, kwa sasa tumekabidhiwa jukumu la kuhakikisha tunawalea Watoto wetu katika misingi ambayo itawafanya wajivunie kuwa na wazazi/walezi bora katika kipindi chote cha uhai wao. Yapo mengi ambayo tumeyakosa kutoka kwa wazazi/walezi wetu hila sasa wajibu wetu ni kuhakikisha Watoto wetu wanapata kile ambacho tulikosa. Zaidi ya yote tuna wajibu wa kuwalinda Watoto wet una makucha ya Dunia. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

 

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

 ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

JE UNAHITAJI KUWA WA KIPEKEE? FAHAMU UFUNGUO UTAKAOKUPA UPEKEE KWENYE KILA UNALOHITAJI

NENO LA LEO (JANUARI 24, 2021): JE UNAHITAJI KUWA WA KIPEKEE? FAHAMU UFUNGUO UTAKAOKUPA UPEKEE KWENYE KILA UNALOHITAJI.

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya ambapo tumejaliwa kuwa na uhai. Wajibu wetu katika siku ya leo ni kuhakikisha tunaendelea kuwa bora katika yale tunayofanya. Yawezekana kuna mambo mengi ambayo tungependa kufanya siku ya leo lakini katika yote nakushauri uchague mambo kadhaa ambayo yanakupa muendelezo kwa pale ulipoishi jana. Kwa kufanya hivyo kila siku, baada ya muda wa miaka kadhaa kila mtu atakushangaa uliwezaje kufanikiwa katika yale utakayokuwa umefanikisha.

Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA 

Ni ukweli ambao unakubalika kwetu sote kuwa kila mtu anatamani kuona anakuwa wa kipekee kwenye kila sekta ya maisha yake. Kila mtu anatamani kuwa na afya bora – hakuna anayebisha kwenye hilo. Kila mtu anatamani kuwa na umbo zuri iwe kwa jinsia ya kike au jinsia ya kiume – hakuna anayebisha juu ya hilo kwa kuwa kila mara tunaona watu wanakesha kwenye mazoezi kwa ajili ya kujenga miili. Hakuna anayebisha kuwa kila mtu anatamani kuwa na maisha yenye uhuru wa kifedha. Hakuna anayebisha kuwa kila mtu anatamani kufanikiwa kuwa na kazi au biashara nzuri na yenye mafanikio. Kwa ujumla tunakubaliana kuwa kila mtu anahitaji kuwa wa kipekee katika kila sekta ya maisha yake.

Jambo moja ambalo litakuwezesha uwe wa kipekee ni VITENDO (ACTIONS) vikiambatana na MAONO (VISION). Huo ndiyo ufunguo wa kufanikisha kila aina ya upekee unahitaji katika maisha yao. Kila siku tunaamka na kuzama kwenye majukumu (vitendo) kwa ajili ya kujipatia mkate wa siku. Hata hivyo, ikiwa kazi tunazofanya haziongozwi na maono tunajikuta tunazunguka huku na kule bila mafanikio. Maana yake ni kwamba vitendo bila maono ni sawa na bure.

Je unahitaji kuwa na mwili wenye afya bora na uliojengeka vizuri?  Kuanzia sasa jipatie muda wa miezi sita ya kufanikisha hitaji lako. Katika kipindi hicho cha miezi sita hakikisha unafanya kile ambacho unatakiwa kufanya kwa ajili ya kuwa na aina ya mwili unaotamani. Hakika baada ya kipindi cha miezi sita utakuwa na mwili uliojengeka kiumbo na afya bora kuliko asilimia 90 ya watu katika eneo lako. Hakuna muujiza bali kinachokubadilisha na kufanya kile ambacho wengine wanafanya kwa ajili ya kujiimairisha kiafya na kimwili.

Je unahitaji kufanikiwa kwenye biashara yako? Hakuna muujiza ambao utakufanya ufanikiwe kibiashara au kwenye kazi yako zaidi ya kujitofautisha na wengine. Kuanzia sasa jipatie muda wa miezi sita na kuendelea kwa ajili ya kufikia kile unachotamani kwenye biashara au fani yako ya kazi. Ikiwa muda mrefu umekuwa unatamani kuanzisha biashara hakikisha katika kipindi hicho cha miezi sita unaanzisha bila kujali ukubwa wa mtaji utakaoanza nao. Unapoanzisha hatua ya kwanza kuna nguvu kubwa ya kubadilisha yasiyowezekana yakawezekana. Hakika katika kipindi cha miezi sita ukiwa na nidhamu ya kufanya kile kinachotakiwa kufanywa katika biashara au kazi yako utakuwa wa kipekee kwa asilimia 90 zaidi ya watu wengi katika kile unachofanya.

Je umekosa mtaji wa kuanzisha biashara kwa muda mrefu? Watu wengi wanatamani kuanzisha biashara lakini wengi wanashindwa kutokana na kutokuwa na mtaji. Hata hivyo, ukiuuliza mtu unahitaji mtaji kiasi gani na mchanganuo wa kiasi anachotaka utashangaa kuona kuwa wengi hawajui kiwango cha mtaji wanachotaka. Pia, matumizi ya kiwango hicho ni kitendawili kwa wale ambao wanajua kiwango cha mtaji wanachohitaji. Kumbe, hali hii inadhihirisha kuwa mtaji upo ndani ya uwezo wetu kutoka kwenye pesa tunazopata kila siku. Ndiyo inawezekana kupata mtaji katika kipindi cha miezi 6. Mbona kila siku unatapa hela ya kifurushi, mbona kila siku unapata hela ya kula, mbona kila siku unapata hela kinywaji na mengine mengi. Yote hayo unayapata kwa kuwa umeyapa kipaumbele. Kuanzia sasa weka mkakati wa kufanikisha mtaji unaohitaji katika kipindi cha kuanzia miezi sita na kuendelea. Hakika baada ya miezi sita utashangaa una asilimia 90 ya mtaji ukilinganisha na watu wengine wanaokuzunguka.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza umuhimu wa vitendo na maono katika kufikia hitaji la maisha yetu. Tunashindwa kufanikiwa siyo kwamba hatuna uwezo wa kufanikiwa bali tunashindwa kuwa tunakosa vitendo ambavyo vinaongozwa na maono. Kwa kutokuwa na maono tunafanya mambo mengi ambayo hayana muunganiko au uhusiano na mwisho wake kila mara tunaangaika kimaisha kwa kuwa vitendo tunavyofanya havitufikishi popote. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

FAHAMU HATUA 3 ZA KUPITIA KATIKA KUFIKIA KILELE CHA MABADILIKO UNAYOTAMANI

NENO LA LEO (JANUARI 22, 2021): FAHAMU HATUA 3 ZA KUPITIA KATIKA KUFIKIA KILELE CHA MABADILIKO UNAYOTAMANI

Habari ya asubuhi mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza pale ulipoishia jana. Ni siku nyingine tunapata nafasi ya kuendelea kutoa thamani kwa ajili ya kuwa bora zaidi katika majukumu yetu.

Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA

Mabadiliko ni jambo ambalo kila mtu anatamani. Pamoja na kwamba wengi wanatamani mabadiliko ukweli unabakia kuwa wanaofikia kwenye kilele cha mabadiliko wanayotamani ni wachache. Huo ndiyo ukweli kwa kuwa mabadiliko yanamtaka mhusika kubadilisha mfumo mzima wa maisha jambo ambalo ni gumu ikiwa mhusika hajadhamiria kubadilika kweli. Katika neno la tafakari ya leo nitakushirikisha hatua tatu ambazo kila mtu anatakiwa kupitia katika kufikia kilele cha mabadiliko anayohitaji.

Hatua #1: Mabadiliko kwenye tabia au changamoto husika Katika hatua hii mhusika anatakiwa awe tayari kutafuta mshauri ambaye atamsaidia kufikia kilele cha mabadiliko anayotamani. Kazi ya mshauri ni kumpa mhusika mwongozo ambao utasaidia kubadilisha tabia/changamoto ambayo imekuwa ikimkwamisha kufikia malengo yake. Mfano, mtu anaweza kutafuta ushauri wa jinsi gani anaweza kukabiliana na changamoto za kikazi, msongo wa mawazo, changamoto za kifedha au jinsi ya kukuza mauzo kwenye biashara. Hii ni hatua muhimu ambayo mhusika anatakiwa kuitumia kwa ajili ya kubadilisha mtazamo, fikra au matendo kuhusiana na changamoto iliyopo mbele yake. Mfano, katika hatua hii mhusika anatakiwa kubadilika kutoka kwenye kuwa na hofu na kuanza kujiamini au kutoka kwenye kutokuchukua hatua na kuanza kuchukua hatua za kivitendo.

Hatua #2: Mabadiliko katika sehemu/sekta maalum ya maisha – Katika hatua hii mhusika tayari ametambua changamoto anayotaka kubadilisha na yupo tayari kukabiliana kwa vitendo na tatizo linalomsumbua katika maisha yake ya kila siku au jamii inayomzunguka. Mfano, mtu anaweza kuwa anahitaji kuboresha maisha yake kwenye sekta ya mahusiano, mauzo, malezi, kujiamini n.k. katika hatua hii muhusika anakuwa na programu ya kubadilisha sehemu ya maisha yake ambapo anaweza kusoma vitabu au makala yanayohusiana na changamoto aliyonayo. Ili kuwa na mabadiliko ya jumla, mhusika anatakiwa kuweka ratiba ambayo anapaswa kuitekeleza katika majukumu yake ya kila siku.

Hatua #3: Mabadiliko ya jumla – Hatua hii inahitimisha mabadiliko ya jumla katika mfumo mzima wa maisha ya mhusika. Katika hatua hii muhusika anabadilika moja kwa moja kutoka kwenye hali yake ya awali na kuingia kwenye ulimwengu mpya kulingana na hitaji la mabadiliko katika maisha yake. Hivyo katika hatua hii mtu anabadilisha mazoea yake yote katika kila nyanja ya maisha. Mfano, mabadiliko ya jinsi mtu anavyojitazama mwenyewe, kujiamini na mtazamo wake kwa watu wanaomzunguka. Hata hivyo, hatua hizi zinategemeana na katika kila hatua lazima mhusika awe tayari kubadilika ndani mwake ili hatimaye mabadiliko hayo yajitokeze katika mfumo wa maisha ya nje.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza hatua tatu za kuzingatia katika kuelekea kwenye kilele cha mabadiliko unayotamani. Hata hivyo, mabadiliko yoyote kwenye maisha ya mtu ili yadumu ni lazima yajengwe kwenye mfumo wa maisha unaolenga kuwa na mafanikio ya muda wote (life time success). Ili kufanikiwa katika mabadiliko ya namna hii ni lazima mfumo mpya wa maisha uambatane na vitendo. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

 ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

NENO LA LEO (JANUARI 19, 2021): JE WAJUA KUWA PESA HAINUNUI FURAHA?

Habari ya asubuhi mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza jitihada zinazolenga kukamilisha ushindi katika siku hii ya leo. Ni siku nyingine tunapata nafasi ya kuwa bora zaidi kuliko ilivyokuwa jana kupitia kwenye thamani tunayotoa katika majukumu yetu ya siku ya leo.

 Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA

Katika jamii tunayoishi, tumeshuhudia asilimia kubwa ya watu ambao mara nyingi huwa wanachanganya uhusiano uliopo kati ya pesa na furaha halisi katika maisha. Katika neno la tafakari ya leo nataka nikukumbushe kuwa kadri unavyoweka malengo ya kuboresha maisha yako hasa katika sekta ya uchumi huna budi kufahamu kuwa kamwe pesa haiwezi kununua furaha.

Wote ni mashahidi kuwa pesa kidogo zinaweza kukufanya uwe na maisha ya huzuni hasa pale mahitaji ya pesa yanapozidi uwezo wako wa kifedha. Kwa tafsiri hii ni wazi kwamba pesa ndogo inaweza kukusababishia uwe na msongo wa mawazo au maisha ya huzuni. Hata hivyo, pamoja na kwamba pesa ndogo inaweza kukusababishia msongo wa mawazo; wote ni mashahidi kuwa wapo matajiri wengi ambao wanaishi maisha ya huzuni pamoja na kwamba wana pesa nyingi kwa ajili ya kukidhi kila hitaji la maisha yao.

Kwa tafsiri hii tunajifunza kuwa unaweza kuwa na pesa nyingi lakini maisha yako yakawa na msongo wa mawazo au huzuni ya moyo kuliko hata masikini. Kumbe, tunachojifunza kwa ujumla wake ni kwamba masikini au tajiri wote wanaweza kuwa na maisha ya furaha au huzuni bila kujali kiwango cha pesa wanachomiliki. Baada ya kugundua uhusiano uliopo kati ya fedha na furaha unatakiwa ufahamu kwamba furaha ya kweli inaanzia ndani mwako pasipo kujali kipato ulichonacho. Hii ni kutokana na ukweli kwamba sio pesa au vitu unavyomiliki vitakufanya uwe na furaha bali furaha unaitengeneza mwenyewe.

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa hatima ya maisha yako ipo mikononi mwako, na ndivyo ilivyo na kwenye maisha yenye furaha. Kila aina ya maisha unayotamani kuwa nayo katika uhai wako ni lazima uyatengeneze ndani mwako (nafsi na roho yako). Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

KWA NINI UNAJICHELEWESHA KWA KIGEZO CHA KUTOKUWA TAYARI?

NENO LA LEO (JANUARI 17, 2021): KWA NINI UNAJICHELEWESHA KWA KIGEZO CHA KUTOKUWA TAYARI?

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni wakati mwingine tumeamka salama tukiwa na nguvu na hamasa kwa ajili ya kuendeleza pale tulipoishia jana. Kila siku katika utangulizi wa neno la siku nimekuwa nikikumbusha umuhimu wa kufanya vitu vyenye muunganiko (Connectivity). Nimekuwa nikifanya hivyo ili kukuepusha kupoteza nguvu na rasilimali pamoja na muda kwa kufanya mambo mengi ambayo hayana uhusiano. Watu wengi wameshindwa kufika mwisho wa safari kutokana na kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja. Katika hali hiyo wanajikuta hakuna hata jambo ambalo linafikia kwenye viwango walivyokusudia na mwisho wake ni kukata tamaa.

Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA 

Katika neno la tafakari ya leo tutaona jinsi gani tumekuwa tunapoteza muda kutokana na kusubiria utayari au ukamilifu wa mahitaji kabla ya kuanza. Watu wengi wamepoteza ndoto zao na wengine kushindwa kupita hatua kutokana na kusubiria utayari au ukamilifu kwa muda mrefu. Katika neno la leo nataka kuanzia sasa uishi kwa kutambua kuwa “wale wote unaowaona kwenye kilele cha mafanikio hakuna hata mmoja ambaye alianzia juu”. Husikubali kudanganywa na mtu yeyote ambaye anasema hakuwahi kuwa kwenye hatua za chini sawa na ilivyo kwako kwa sasa.

Fikiria kwenye kila aina ya mafanikio unayotamani katika maisha yako na jiulize kwa nini unakwama kuanza hadi sasa. Ikiwa ni upande wa mafanikio kwenye siasa – angalia wanasiasa wenye mafanikio makubwa na vuta historia zao. Wengi walianzia kwenye ngazi za chini kabisa kwenye uongozi na utendaji.

Fikiria kuhusu mafanikio kwenye ngazi za utendaji katika taasisi na Serikali au taasisi zisizo za Serikali – Watendaji wa ngazi za juu wote walianzia kwenye ngazi chini. Mfano, Meneja wa Benki alianza kama “Cashier” au Afisa wa kawaida. Wapo watendaji wengi wa ngazi za chini ambao walianzia kwenya nafasi za chini kabisa lakini leo hii imebaki kuwa historia.

Yawezekana mwaka huu umepanga kumiliki nyumba yako lakini bado unasita kuanza kwa vile unaona bado haujajikamilisha. Hakuna linaloshindikana kwa kuwa hata huyo mwenye nyumba yako amepitia kwenye maisha unayoyapitia sasa hila ambacho kimemfikisha kwenye viwango alivyonavyo kwa sasa ni uthubutu wa kuanza.

Yawezekana umekuwa unakusudia kuanzisha biashara lakini unachelea kuanza kutokana na kuona hauna mtaji wa kutosha. Ndugu yangu wale wote waliofanikiwa kibiashara wengi wao walianzia kwenye biashara za kawaida kabisa ambazo kwa mtaji huo ulionao unatosha kabisa kuanza. Mfano, “binafsi nilianzisha ufugaji wa nguruwe kwa nguruwe mmoja na Watoto wake sita lakini kupitia nguruwe huyo hadi sasa nina nguruwe 117 na nimeuza nguruwe 85 ndani ya kipindi cha miaka minne tu”. Wakati naanza nilikuwa na banda la banzi lenye milango mitano tu lakini leo hii ni banda za kisasa zenye milango 18.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa kusubiria utayari au ukamilisho ni chanzo cha ndoto nyingi kuchelewa kutekelezwa au kufa kabisa. Wale ambao tunaona wamefanikiwa katika sekta mbalimbali za maisha kilichowafikisha huko ni kuwa na uthubutu wa kuanza bila kujali hatua wanazoanzia. Anza kidogo bila kupoteza picha pana iliyopo kichwani mwako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

 

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

 ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

SOMO MUHIMU KUHUSU KIPATO NA UHURU WA KIFEDHA

NENO LA LEO (JANUARI 16, 2021): SOMO MUHIMU KUHUSU KIPATO NA UHURU WA KIFEDHA

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambapo tumebahatika kupata kibali cha kuendelea kuwa hai. Ni katika siku hii nakukumbusha kuwa safari bado ni ndefu katika kufikia kilele mafanikio katika maisha. Safari hii imejaa milima na mabonde na vyote hivyo ni kwa ajili ya kutupa changamoto ili tufike salama. Huu siyo wakati wa kukata tamaa kutokana na changamoto zilizopo mbele yako bali wakati huu ni wakati bora kwako kunyanyuka, kuweka mikakati upya na kuanza kutekeleza malengo uliyojiwekea katika sekta ya maisha yako.

Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA

Katika neno la tafakari ya leo tutaona jinsi ambavyo ongezeko la kipato limekuwa upanga wa kuangamiza watu wengi katika jamii. Watu wengi katika jamii yetu huwa wanaamini kuwa ongezeko la kipato ni njia halisi ya kuelekea kwenye uhuru wa kifedha. Ukifanya mahojiano na waajiriwa wengi utagundua kuwa asilimia kubwa kati yao wanaamini kuwa maisha yao yapo jinsi yalivyo kwa kuwa wanapokea mishahara kiduchu. Wengi wanaamini kuwa ongezeko la mshahara litabadilisha maisha yao. Vivyo hivyo, wafanyabiashara nao wanaamini kuwa kuongezeka kwa faida katika biashara zao ni hatua muhimu ya kuelekea kwenye uhuru wa kifedha.

Ni kweli kuwa ongezeko la mshahara au faida ni muhimu katika kuelekea kwenye maisha yenye uhuru wa kifedha. Hata hivyo, kiuhalisia watu wengi katika jamii wameangamizwa na ukuaji wa kipato. Baada ya kuongezeka kwa mshahara au faida, wengi wanajikuta kwenye mfumo ule ule wa upungufu wa fedha katika maisha ya kila siku. Wapo watu wengi katika jamii ambao wanalipwa mishahara mikubwa lakini tunashuhudia wakiangaika kipesa. Vivyo hivyo, wapo wafanyabiashara ambao pamoja na kutengeneza faida kubwa katika biashara lakini bado biashara wanazofanya zimedumaa. Pia katika jamii zetu mifano mingi ambayo inahusisha watu ambao wamepoteza mwelekeo kutokana na ongezeko la kipato cha ghafla katika maisha yao. 

Wote ni mashahidi kuwa katika jamii ni kawaida kukuta Mhudumu wa Ofisi ana maisha mazuri kuliko Maafisa wenye mishahara mikubwa. Hali iko hivyo pia, husishangae kukuta Wafanyabiashara za kawaida (biashara ndogo) kuwa na maisha mazuri ikilinganishwa na baadhi ya Wafanyabiashara wakubwa. Kumbe, somo la kujifunza hapa ni kwamba “uhuru wa kifedha unategemeana na jinsi unavyotumia pesa unazopata”.

Ufunguo wa kuwa na maisha yenye uhuru wa kifedha unahusisha vitu vitatu: Moja, ni lazima uwe tayari kutengeneza pesa – katika kila hali unazimika kufanya kazi kwa bidii na weledi ili upate kuingiza pesa. Mbili, ni lazima utumie pesa zako kutengeneza pesa zaidi – katika hili huwa napenda kutumia msemo kuwa “pesa zinaenda sehemu zinakopendwa zaidi na kuthaminiwa”. Haijalishi ni pesa kiasi gani unaingiza kwa siku au mwezi ikiwa hauthamini pesa hiyo kamwe haiwezi kuongezeka zaidi. Tatu, ni lazima matumizi yako mara zote yasizidi pato lako – ikiwa unaishi maisha ya gharama zaidi ya kipato unachoingiza hakika kipindi cha maisha yako chote utaendelea kuangaika kipesa.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa uhuru wa kifedha unapatikana kwa kuthamini pesa unayopata. Pesa inatengeneza pesa, kwa maana kila pesa unayopata hakikisha kuna kiasi kinachotumika kuzalisha pesa zaidi katika siku za baadae. Hiyo ndiyo siri ambayo watu wote wanaitafuta kwa ajili ya kubadilisha maisha yao. Hata hivyo, wanaofanikiwa kuiishi ni wale wenye maono makubwa na nidhamu katika maisha. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

 ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

SIRI YA KUUFANYA MWEZI JANUARI/JULAI UWE SAWA NA MIEZI MINGINE

NENO LA LEO (JANUARI 15, 2021): SIRI YA KUUFANYA MWEZI JANUARI/JULAI UWE SAWA NA MIEZI MINGINE

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya yenye matumaini na hamasa ya kutosha katika kufikia lengo kuu lililopo mbele yetu. Ni siku ambayo nakukumbusha kuendelea kufanya vitu vya kipekee ambavyo kila siku vinakuimarisha katika hatua za ukuaji kuelekea kwenye mafanikio ya ndoto zako. Pia, nakukumbusha kuwa mwaka 2021 ndo huu tayari unazidi kushika kasi, wakati ni sasa wa kuishi kwa vitendo malengo uliyojiwekea katika kipindi hiki.

Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA

Katika neno la tafakari ya leo tutaona jinsi ambavyo kila mmoja wetu anavyoweza kuufanya mwezi Januari au Julai uwe rafiki kwake sawa na ilivyo miezi mingine. Katika jamii tunayoishi kila ikifika mwezi Januari au Julai huwa tunashuhudia malalamiko ya kila aina huku mengi yakihusisha upungufu wa fedha. Katika neno la tafakari ya jana niligusia kuwa miezi hii huwa inahusisha utokaji wa fedha kwa ajili ya kulipia mahitaji ya shule sambamba na kodi za nyumba. Mahitaji hayo ya lazima huwa yanaacha idadi kubwa ya watu katika jamii wakiwa hawana pesa kwa ajili ya kukidhi mahitaji mengine. Hali hii huwa inapelekea watu wengi kuishi kwa msongo mkubwa unaopelekea wengine kuwa na huzuni zinazoambatana na hasira za mara kwa mara bila sababu za msingi.

Ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye anakuwa hajui kuwa mwezi Januari au Julai anatakiwa kulipia ada za wanafunzi au kulipia pango la nyumba. Chanzo kinachopelekea miezi hii iwe na msongo wa pesa kwa watu wengi ni kwa vile watu hawana mfumo wa bajeti ya mahitaji ya mwaka mzima. Njia rahisi ya kuifanya miezi hii iwe rafiki kwako ni kuwa na bajeti ambayo unaitekeleza kutoka mwanzo hadi mwisho wa mwaka. Ninacho maanisha hapa ni kwamba mahitaji ya ada za wanafunzi au malipo ya kodi yanatakiwa kuanza kuandaliwa toka mwezi Januari unapoanza ili itakapofika muda wake liwe ni suala la kukamilisha malipo.

Katika neno la tafakari ya jana tuliona kuwa badala ya kupunguza matumizi unatakiwa kuongeza mifereji ya pesa. Katika mifereji uliyonayo unatakiwa kutenga kila mwezi asilimia flani kwa ajili ya kufanikisha mahitaji ya ada au malipo ya pango la nyumba katika miezi ambayo fedha hizo zinatakiwa. Kama kuna uwezekano unaweza kuanzisha Mfereji maalum kwa ajili ya kukamilisha kila hitaji la pesa au kuhakikisha kila mtoto anakuwa na mfereji wake wa kukamilisha mahitaji ya masomo. Endapo utatumia mbinu hii kwa nidhamu hakika utashangaa kila ikifika mwezi Januari au Julai unakuwa tayari umejiandaa kukamilisha mahitaji ya pesa kulingana na bajeti yako.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa mwezi Januari au Julai ni miongoni mwa miezi ambayo tunaweza kuishi bila ya kuwa na msongo wa mawazo ikiwa tutakuwa na bajeti na kuhakikisha tunatekeleza bajeti hiyo kila siku. Ukweli ni kwamba hakuna kinachohitaji pesa mwezi Januari au Julai ambacho kilikuwa nje ya ufahamu wako. Hivyo, kuna kila sababu ya kuweka maandalizi kila mwezi kulingana na mahitaji ya pesa yaliyopo kwenye bajeti yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

HII NDIYO NJIA SAHIHI YA KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA MAHITAJI YA PESA

NENO LA LEO (JANUARI 14, 2021): HII NDIYO NJIA SAHIHI YA KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA MAHITAJI YA PESA

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambapo tumepewa kibali cha kuwa hai. Kibali hiki in cha kuwa na uwezo wa kuvuta pumzi ya hewa safi na kutoa hewa chafu na katika kufanya hivyo tunapata nguvu ya kutafuta ridhiki kupitia majukumu yetu ya kila siku. Kila unapovuta hewa safi (Oxyjeni) na kutoa hewa chafu (Carbondiode) unatakiwa kutambua kuwa unazalisha nguvu kupitia mmeng'enyo wa chakula na nguvu hizo zinatakiwa   kutumika kwa faida.

Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA

Mwanadamu ni kiumbe ambacho kinategemea uwepo wa pesa kwa ajili ya kukamilisha mahitaji ya msingi. Toka pesa ilipogunduliwa katika historia ya maendeleo ya Mwanadamu imekuwa ni nyenzo muhimu ya upatikanaji wa mahitaji ya msingi kwa mtu mmoja mmoja, familia na hata taifa. Hata hivyo, katika maendeleo ya Mwanadamu kadri umri kuongezeka ndivyo mahitaji ya pesa yanavyoongezeka. Hali iko hivyo pia kwa familia na hata taifa. Mara zote ukuaji wa mtu, familia au taifa huwa unaambatana na ongezeko la mahitaji ya pesa.

Tutakubaliana kuwa katika kipindi cha utoto mahitaji ya pesa huwa ni kidogo sawa na ilivyo kwa familia changa ya watu wawili. Hila kadri umri unavyozidi kuongezeka au kadri familia inavyozidi kupanuka ndivyo na mahitaji ya pesa yanaongezeka. Katika jamii zetu tumezoea kuona mwezi Januari na Julai katika kila mwaka inakuwa ni miongoni mwa miezi ambayo huwa inahusisha mahitaji makubwa ya pesa kwa mtu mmoja mmoja au familia. Hali hii inatokana na ukweli kwamba miezi hii inahusisha ulipaji ada za wanafunzi pamoja kodi za pango la nyumba. Hata hivyo, mwezi Januari unakuwa na mwezi wenye vilio vikubwa vya upungufu wa pesa kwa kuwa wengi wanakuwa na matumizi makubwa nje ya bajeti katika sherehe za mwisho wa mwaka.

Je ni ipi tiba halisi ya kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya pesa? Katika jamii, watu wengi huwa wanatumia mbinu ya kubana matumizi kama tiba ya kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya pesa. Hata hivyo, mbinu hii huwa haimpi mhusika Uhuru wa kufurahia maisha kutokana na jinsi anavyojibana katika mfumo mpya wa maisha. Matokeo ya mbinu hiyo ni kuongezeka kwa msongo wa mawazo kadri mahitaji ya pesa yanavyoongezeka.

Kumbe, tiba halisi ya kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya pesa siyo kupunguza matumizi bali ni kuongeza mifereji mipya ya mapato. Wengi katika jamii wanaendelea kuteseka kwa kuwa wanaishi kwa kutegemea chanzo kimoja cha pesa bila kugundua kuwa chanzo hicho kinaelemewa kutokana na ongezeko la mahitaji ya pesa. Kama ni mshahara, ukweli ni kwamba kasi ya ongezeko la mahitaji ya pesa haiwezi kuendena na kasi ya ongezeko la mshahara toka kwa mwajiri wako. Hata kwenye biashara, tunashuhudia biashara nyingi zinakufa kutokana na kuzidiwa mahitaji ya pesa yanayowakabili wamiliki wa biashara hizo. Tafsiri yake ni kwamba kasi ya ongezeko la mahitaji ya pesa inakuwa kubwa ikilinganishwa na faida inayotengenezwa kwenye biashara.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza ni kawaida mahitaji ya pesa kuongezeka kadri umri unavyoongezeka. Baada ya kutoka kwenye maisha ya utegemezi wa wazazi, mahitaji ya pesa yanaongezeka kwa kasi sana ikiwa hakuna mkakati wa kuongeza vyanzo vipya vya mapato. Badala ya kupunguza matumizi kwa kujibana kama mbinu ya kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya pesa unatakiwa kuongeza mifereji ya kipato ili kuendana na ukuaji wa mahitaji ya pesa. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

HII NDIYO MIFEREJI YA PESA AMBAYO UNATAKIWA KUIWEKEA MKAZO

NENO LA LEO (JANUARI 12, 2021): HII NDIYO MIFEREJI YA PESA AMBAYO UNATAKIWA KUIWEKEA MKAZO

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa kila mmoja wetu anaendelea vyema na majukumu yake bila kujali changamoto za hapa na pale. Changamoto ni sehemu ya majukumu na changamoto hizo ndizo zinatuimarisha katika yale tunayofanya. Wajibu wetu mkubwa ni kutoruhusu changamoto hizo ziturudishe nyuma au kukubali kuacha yale ambayo tumedhamiria kufanya kwa ajili ya kubadilisha maisha yetu.

Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA

Uhuru wa kifedha ni kilio cha kila mtu ambaye amedhamiria kuisha maisha yenye tija katika kipindi uhai wake. Hata hivyo, fedha haipatikani ikiwa haijawekewa njia ambazo huwa inapitia. Pesa ina njia zake na wale ambao wameweka njia hizo pesa huwa inakilimbilia kwao wakati wale ambao hawana njia hizo pesa inawakimbia. Huo ndiyo ukweli kuhusu upatikanaji wa pesa. Katika neno la tafakari ya leo tutaangalia baadhi ya njia/mifereji ya pesa ambayo unatakiwa kuwa nayo ili kujihakikishia maisha yenye uhuru wa kifedha. Karibu tupitie mifereji hiyo:-

Mfereji #1: Uwekezaji kwenye masoko ya mitaji. Huu ni aina ya mfereji ambao unawezesha pesa yako ikufanyie kazi wakati wewe umelala. Zipo aina mbalimbali za uwekezaji wa mitaji lakini katika mazingira yetu uwekezaji ambao umezoeleka ni:

a)   Uwekezaji kwenye masoko ya hisa – Kama mwekezaji unatakiwa kununua hisa za kampuni ambazo zimeorodheshwa kwenye Soko la Hisa. Kwa Tanzania uwekezaji wa hisa unaratibiwa na Soko la Hisa la Dar es Salaam (Dar es Salaam Stock Exchange). Kupitia uwekezaji huu unaweza kunufaika kupitia kupanda kwa thamani ya hisa ikilinganishwa na kipindi unanunua hisa za kampuni husika au kupitia gawio (divedend) kwa wanahisa ambalo huwa linategemea faida iliyotengenezwa na kampuni husika katika kipindi husika.

b)   Uwekezaji kwenye Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (Mutual Fund Investments) – Huu ni uwekezaji ambao kwa hapa kwetu unafahamika kama uwekezaji kwenye vipande. Uwekezaji huu unaratibiwa na Serikali kupitia Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (UTT) ambayo ipo sita hadi sasa. Kila aina ya Mfuko una taratibu zake za namna muwekezaji anavyofaidika kutokana na uwekezaji wake.

KUJUA KWA UNDANI KUHUSU MIFUKO HII JIUNGE NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

c)   Uwekezaji kwenye Hatifungani/Dhamana za Serikali (Government Bonds) – Huu ni aina ya uwekezaji ambao unahusisha wawekezaji kuikopesha Serikali kwenye vipindi tofauti vya uwekezaji. Hatifungani za serikali ni fursa nzuri ya uwekezaji hasa kwa wale wanaohitaji kuwekeza fedha na kupata faida bila kutumia nguvu nyingi au kuwa na wasiwasi juu ya usalama wa sehemu wanakowekeza pesa zao. Fursa hii inagawanyika katika sehemu mbili ambazo ni: Hatifungani/Dhamana za Muda Mfupi (Treasury Bills) na Hatifungani/Dhamana za Muda Mrefu (Treasury Bonds).

d)   Kuwekeza kwenye akaunti maalum za benki za biashara (fixed benki a/c) – Huu ni uwekezaji wa mtaji ambapo mwekezaji anapata faida kulingana na makubaliano au taratibu zilizowekwa kwenye aina ya akaunti au aina ya benki ambayo amewekeza pesa zake.

Mfereji #2: Kazi au biashara. Huu ni mfereji wa fedha ambao unatumiwa na watu wengi Duniani kote. Katika mfereji huu watu wanatengeneza kipato kupitia kazi walizoajiriwa au kupitia biashara. Biashara inaweza kuhusisha uwekezaji kwenye viwanda, kilimo na ufugaji, duka au mazao. Kwa ujumla mfereji huu unatumiwa na watu wengi kutokana na urahisi au usalama wa upatikanaji wa pesa bila kujali wingi au uchache wa pesa inayopatikana. Pia, kwa asili kila mtu ni mfanyabiashara bila kujali kiwango cha mtaji wake katika biashara anayofanya. Vivyo hivyo, wengi wanatumia mfereji wa kazi kama chanzo cha mapato kutokana na mazoea yaliyojengeka katika jamii. Mwanangu nenda shule soma kwa bidii ili upate kazi yenye malipo mazuri – ni kauli ambayo imezalisha watu wengi ambao wanategemea kazi kama mfereji wa mapato.

Mfereji #3: Uwekezaji kwenye ardhi na majengo (Real Estate Invesments). Huu ni uwekezaji mwingine ambao unahusisha utengenezaji wa faida kutoka kwenye kipande cha ardhi au majengo kupitia kodi za matumizi ya rasilimali hizo. Unaweza kuwa na ardhi ambayo ipo eneo zuri la kimkakati lakini hauna pesa za kujenga japo kuna watu wenye pesa ambao wapo tayari kujenga kwa makubaliano maalum ambayo mtaingia. Pia, kupitia uwekezaji wa nyumba za kupangisha unaweza kutengeneza kipato kupitia kodi za wapangaji.

Mfereji #4: Pato kutokana na maarifa au haki miliki (Intelectual property rights) – Hii ni aina nyingine ya mifereji ya kipato ambao unahusisha kuingiza pesa kutokana na maarifa uliyonayo au hatimiliki zilizotokana na matumizi ya akili yako. Mfano, unaweza kuwa unalipwa kutoka na ujuzi ulionao; mwanasheria nje ya pesa anayolipwa kama mshahara wake anaweza kuingiza pato kupitia ushauri wa kisheria. Vivyo hivyo, kwa fani nyingine ambazo zinahusisha utengenezaji wa kipato nje kazi waliyoajiriwa. Tukiachana na pato kutokana na fani yako, mfereji huu unahusisha pia upatikanaji wa pesa kutoka kwenye mauzo ya rasilimali au vifaa ambavyo unavimiliki. Mfano, unaweza kutengeneza kipato kupitia mauzo ya vitabu ulivyoandika au unaweza kutengeneza kipato kupitia mauzo kanuni ya uzalishaji wa bidhaa ambayo unaimiliki wewe. Mfano mwingine, Coca cola au pepsi wanatengeneza pesa nyingi kutoka kila kona ya Dunia kupitia formula ya utengenezaji wa Soda zenye ladha ya Coca au Pepsi.

Mfereji # 5: Uwekezaji kwenye mitandao. Huu ni mfereji mwingine ambao kwa sasa unashika kasi na matajiri wengi ambao wanaongoza kwa kutengeneza pesa nyingi ni wale ambao wanatumia teknolojia ya ukuaji wa mawasiliano. Fikiria kuhusu mmiliki wa Facebook, Instangram, WhatsApp, Twiter, Google. Fikiria kuhusu uuzaji wa bidhaa au maarifa kupitia mitandao. Jeff Bezos (Tajiri namba 2 Duniani) kupitia Amazon na Jack Ma (Tajiri namba moja nchini China) kupitia Alibaba ni miongoni mwa matajiri wakubwa ambao wamenufaika kupitia ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano. Ni muda muafaka kila unachofanya kufikiria kitakuingiziaje pato zaidi kutokana na ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano. Unaweza kutumia mitandao hii kutoa maarifa, kutangaza bidhaa zako na unaweza kutumia mitandao hii kama Duka sawa na maduka mengine.

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza mifereji mitano ya fedha katika Ulimwengu wa sasa. Katika kipindi hiki cha mwaka 2021 ni wakati muhafaka wa kuongeza mifereji ya kipato zaidi ili kujiweka salama kwenye maisha yenye uhuru wa kifedha. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com