JIFUNZE HATUA 4 ZA MCHEZO WA PESA

NENO LA LEO (Agosti 1, 2020): JIFUNZE HATUA 4 ZA MCHEZO WA PESA

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa asubuhi hii ya leo ambapo tunaunza mwezi Agosti ikiwa ni miezi mitano tu ambayo tumebakiza kumaliza mwaka 2020. Kila mmoja kwa nafasi yake amshukuru Muumba kwa baraka zake ambazo amemjalia katika kipindi chote cha mwaka huu. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.


JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza hatua nne za mchezo wa kutengeneza pesa. Mwanafanikio na bilionea Robert Kiyosaki anatushirikisha kutengeneza pesa ni sawa na michezo mingine ambayo inapendelewa na watu kuwa mchezo huu unahusisha kanuni na sheria. Katika kanuni hizo na sheria Kiyosaki anatushirikisha hatua nne muhimu za mchezo wa kutengeneza pesa kama ambavyo zimefafanuliwa katika Makala hii hapa chini:-

Hatua #1: Ondoa madeni yote mabaya. Baada ya kumaliza madeni hayo andaa bajeti na hakikisha unaifuata bajeti hiyo. Ni kawaida watu kukopa kila mara pale fursa ya kukopa inapojitokeza na wengi katika kuchukua mikopo hiyo huwa hawajiulizi juu ya usalama wa mkopo husika. Tabia hii inapelekea watu kujidumbukiza kwenye madeni makubwa ambayo yanaathiri mtiririko wa pato lao.

Ikiwa unahitaji kuwa na uhuru wa kifedha hatua ya kwanza unayotakiwa kufuata ni kuepuka mikopo mipya sambamba na kuweka utaratibu wa kumaliza madeni yote. Endapo utahitaji kukopa hakikisha umejiridhisha kuwa mkopo husika utajirejesha wenyewe kutokana na faida inayozalishwa kwenye sehemu ambapo umeuelekeza mkopo huo.

Hatua #2: Toa thamani kupitia kazi au biashara unayopenda kutoka rohoni. Pesa zinatengenezwa kwa kutoa thamani kwa jamii inayokuzunguka. Iwe ni kazi au biashara utazawadiwa kulingana na thamani unayotoa kwa walengwa wako. Ili utoe thamani zaidi ni lazima utambue ni sadaka zipi ambazo upo tayari kujitoa. Sadaka hizi zina husisha: kujinyima kwenye matumizi ya muda – utatakiwa kufanya kazi zaidi ya masaa uliyozoea; rasilimali fedha – utalazimika kuithamini pesa unayopata kwa kuhakikisha inatumika kununua vitu vya msingi; kujitesa – utalazimika kuulazimisha mwili kufanya kazi za ziada; na kijamii/kimahusiano – utajikuta unakimbiwa na marafiki kwa kuwa hawakuoni kwenye ya viwanja mlivyozoea hapo awali au kama ni familia utajikuta kuna mabadiliko ya muda ambao umezoea kuwa karibu nao.

Hatua #3: Kusanya mtaji na punguza matumizi yasiyo ya lazima. Katika hatua ya pili tumeona kuwa unatakiwa kujitoa sadaka kwa ajili ya kuishi maisha mapya ya mchezo wa pesa. Kwenye hatua ya tatu ya mchezo huu unatakiwa kuainisha sehemu ambazo utapunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuhakikisha pesa hiyo inawekezwa sehemu salama kwa ajili ya kukuza mtaji wako. Sehemu ambazo unaweza kupunguza matumizi ni kama vile: kupunguza matumizi ya vinjwaji ulivyoea Mfano, kama kila siku umezoea kunywa kinywaji cha Tshs. 1,000.00 kwa kutokuwanywa kinywaji hicho kwa mwezi utakuwa umeokoa Tshs, 30,000.00; pia unaweza kupunguza bajeti yako ya manunuzi ya nguo; kupunguza kwenye matumizi ya simu (vifurshi); vifurushi vya TV; na mahemezi ya bidhaa zisizo za lazima.

Hatua #4: Wekeza pesa na anzisha biashara. Ili na uhuru wa kifedha ni lazima ifikie hatua ambayo pesa inaingia hata nyakati ambazo haufanyi kazi. Kadri unavyokuwa na vitega uchumi vingi ambavyo viko hai ndivyo unakuwa na uhuru wa kifedha. Hata hivyo ni lazima utambue kuwa vitega uchumi vinatengenezwa kupitia uwekezaji. Unaweza kuwekeza kwenye biashara ya majengo (real estate), unaweza kuwekeza biashara ya mitaji kama vile hisa, hatifungani au mifuko ya uwekezaji wa pamoja (Capital Market Investments) au unaweza kuwekeza kwenye biashara za maduka, vyakula au viwanda bila kusahau uwekezaji kwenye compyuta softwares.

Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza hatua nne za mchezo wa kutengeneza pesa. Hatua hizi zinatumiwa na matajiri wengi kutengeneza utajiri mkubwa na zinaweza kufanya kazi kwako pia endapo utaamini kuwa zinafanya kazi. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika maisha yako yatabadilika. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujifunza zaidi kuhusu uwekezaji wa hisa na dhamana kwa kununua uchambuzi wa vitabu viwili ambavyo: (a) How the Stock Market Work ambacho kimeandikwa na Profesa Ramon P. DeGennaro wa Chuo Kikuu cha Tennessee, Knoxville; na (b) The Warren Buffet Way” kutoka kwa mwandishi Robert G. Hagstrom. Uchambuzi wa Vitabu vyote unapatikana kwa gharama ya OFA ya Tshs. 5,000/= badala ya elfu kumi.

Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

 

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com


onclick='window.open(