FAHAMU MATUMIZI YA LAZIMA KATIKA BAJETI YAKO.


NENO LA LEO (AGOSTI 26, 2020): FAHAMU MATUMIZI YA LAZIMA KATIKA BAJETI YAKO.

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama ikiwa na nguvu za kutosha kuendeleza pale ulipoishia jana. Ni asubuhi ambayo naendelea kukumbushia kuwa husidharau hatua fupi unazopiga kila siku kwa kuwa hatua hizo endapo zitaendelezwa ndizo zitakamilisha mzunguko wa safari yako. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza namna ambavyo unaweza kubana matumizi kwa kuhakikisha unaepuka matumizi yasiyo lazima kwenye bajeti yako. Neno la tafakari ya leo linajibu swali ambalo liliulizwa na mwenzetu katika jukwaa hili. Tumefundishwa sehemu mbalimbali kuwa mahitaji ya msingi kwa binadamu ni Chakula (food), Mavazi (clothes) na Malazi (shelter). Hivyo, tafsiri ya haraka ni kwamba bajeti ni lazima izingatie mahitaji hayo ya msingi kwa kiwango stahiki kabla ya kuongeza mahitaji mengine kulingana na umuhimu wake kwako.

✍🏾  Hata hivyo angalizo ambalo tunatakiwa kuzingatia ni kwamba, mahitaji ya msingi katika bajeti yako yanatakiwa kupangiwa kiwango cha pesa kulingana na uhitaji halisi. Mfano, siyo lazima kila mwezi uweke bajeti ya mavazi. Pia, siyo lazima niweke bajeti ya chakula cha elfu ishirini kwa siku wakati kuna uwezekano wa kutimiza hitaji hilo kwa shilingi elfu kumi. 

✍🏾 Baada ya bajeti yako kuzingatia mahitaji ya msingi kwa kila mwanadamu kinachofuata kuweka mahitaji muhimu ambayo yanabadirika kulingana na vipaumbele vya mhusika. Mfano, kwa ajili ya maendeleo ni lazima bajeti yako izingatie kutenga pesa kwa ajili ya uwekezaji, kujiendeleza kimaarifa au ujuzi, mahitaji ya msingi kwa wategemezi wako, mahitaji ya kiafya, mahitaji ya kijamii pamoja na mahitaji ya kiroho. 

✍🏾 Mahitaji yasiyo ya lazima ambayo yanatumia kiwango kikubwa cha pesa kwa watu wengi kwa kutaja tu baadhi ni pamoja na: ulevi, uvutaji sigara, manunuzi ya vitu visivyo vya lazima kama vile nguo kila mara na kuigiza maisha ya juu ambayo hayaendani na pato lako. 

✍🏾 Mwisho, neno la tafakari ya leo linatufundisha mahitaji ya lazima na yale ambayo siyo ya lazima katika bajeti yetu. Kila mtu ana nafasi ya kuboresha bajeti yake kwa kuhakikisha inakuwa na mahitaji ya lazima kulingana na vipaumbele vyake. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaona tofauti katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(