FAHAMU TOFAUTI KATI YA MTU ANAYEWAJIBIKA NA HASIYEJIBIKA KWA AJILI YA MAISHA YAKE.

NENO LA LEO (AGOSTI 3, 2020): FAHAMU TOFAUTI KATI YA MTU ANAYEWAJIBIKA NA HASIYEJIBIKA KWA AJILI YA MAISHA YAKE.

πŸ‘‰πŸΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa asubuhi hii ya leo ambapo ni matumaini yangu kuwa tunalianza juma tukiwa na afya ya kutosha kwa ajili ya kuendelea kuweka thamani katika kipindi cha uhai wetu. Basi kila mmoja wetu aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza sifa za mtu anayewajibika kutimiza hitaji la maisha na yule ambaye anatanguliza visingizio katika kila hali. Katika neno la tafakari ya jana tuliona kuwa uwajibikaji ni msingi wa kufanikisha hila lolote maisha. Pia tuliona kuwa kila siku tunaalikwa kuchagua kuwajibika au kutowajibika na kuacha asili achukue mkondo wake. Kwa kuanzia karibu tujifunze tofauti ya sifa za watu hawa:-

✍🏾 Sifa #1: Mtu anayewajibika yupo tayari kuendelea na wazo lake – Hapa mhusika anafanya maamuzi ya kutimiza jukumu lililoko mbele yake bila kuogopa vikwazo. Wakati huo huo, mtu hasiyewajibika mara zote anatafuta visingizio binafsi (anakubaliana na visingizio vinavyoendana na hali yake – Mfano, mimi siwezi kwa kuwa sina mtaji au sina elimu n.k). Baada ya kukubaliana na visingizio hivyo hatua ya mwisho ni kuamua kusubiria kwa matumaini (hapa mhusika anajipa kauli zote za matumaini kama vile “kama ipo, ipo bwana, ipo siku nitafanikiwa, n.k).

✍🏾 Sifa #2: Mtu anayewajibika yupo tayari kutafuta suluhisho – Mtu anayewajibika mara zote yuko upande wa kutafuta suluhisho juu vikwazo au changamoto zinazomkabili. Sifa hii inahusisha kujiuliza swali la je natakiwa kuchukua hatua gani ili kuondoka na changamoto iliyopo mbele yangu? Wakati huo huo mtu hasiyewajibika huwa na muda wa kuangaika kutafuta suluhisho. Pale anapokumbana na changamoto au kikwazo anatumia changamoto hiyo kama kielelezo cha kuelezea kwa nini alishindwa kusonga mbele.

✍🏾 Sifa #3: Mtu anayewajibika anamiliki suluhisho ambalo amechagua – Baada ya kupata suluhisho ya changamoto au kikwazo kinachomkabili, mtu anayewajibika mara zote kuwa yeye ndo mhusika mkuu wa kufanikisha au kutofanikisha suluhisho husika. Pia anatakiwa kuwa tayari kukubaliana na matokeo yatakayotokea kutokana na suluhisho ambalo amechagua. Kinyume chake ni kwamba mtu ambaye hawajibiki hata pale anapopata suluhisho anatekeleza huku akitafuta sehemu ya kuangushia mzigo pale ambapo matokeo hayatakuwa upande wake.

✍🏾 Sifa #4: Mtu anayewajibika anakubaliana na ukweli – Mtu anayewajibika anatambua kuwa kupingana na ukweli ni kupoteza muda. Kutokana na kutambua ukweli ulioyopo mara zote anawajibika kutafuta ukweli kwa kujiuliza ni mbinu au njia zipi ambazo ni sahihi kufanikisha hitaji lake. Kwa upande wa mtu ambaye hawajibiki mara zote anakataa ukweli (hajisumbui kujiuliza maswali kutokana na changamoto iliyopo mbele yake. Pia anatumia nguvu na rasilimali nyingi kupambana na ukweli ikiwa analenga aonekane njia yake ndo sahihi.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza tofauti zilizopo kati ya mtu anawajibika kufikia hitaji la maisha yake na yule ambaye hawajibiki. Naendelea kukumbusha kuwa uwajibikaji ni msingi wa kufikia hitaji la maisha yako. Si Serikali, Wazazi, familia, elimu, kazi au mazingira unayoishi ambayo yanakukwamisha kufikia hitaji la maisha yako. Ukweli ni kwamba ambaye anakukwamisha ni wewe mwenyewe. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika maisha yako yatabadilika. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 


πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(