ππΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi nyingine ambayo naamini kila mmoja wetu ameamka salama na yupo tayari kukamilisha majukumu yake ya leo. Ni siku ambayo naendelea kukumbusha umuhimu wa kuyatoa maisha yako kwa ya jamii inayokuzunguka na vizazi vijavyo. Basi kwa pamoja tuseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii ili nipate yaliyo bora katika maisha.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tujifunza namna ambavyo kila mmoja anaweza kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kujitangaza na hatimaye kupata mafanikio makubwa sana. Kwa sasa tunaishi kwenye ulimwengu wenye kila aina ya kelele za mitandao ya kijamii, wapo ambao wametumia mitandao hii kutengeneza kipato zaidi na wapo ambao wanatumia mitandao hii kwa mambo yasiyo na tija katika maisha yao. Mitandao hii endapo inatumiwa vyema ni “asset” (kitu kinachokuongezea kipato) na pale inapotumia visivyo ni “liability” (kitu kinachochukua fedha zako mfukoni). Ili ufanikiwe kutumia mitandao hii kwa faida zaidi ni lazima ufahamu mbinu muhimu za namna ya kuwasilisha ujumbe wako kwenye mitandao hii na hatimaye ujumbe wako uwafikia watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii.
✍πΎ Je simu janja (smart phone) yako umekuwa unaitumia kufanyia nini? Haijalishi simu yako unaitumia kusoma makala hii kwa sasa, haijalishi unatumia simu yako kuwashirikisha watu picha zako, haijalishi simu yako unaitumia kuchati kwenye Instangram, Facebook au Whatsapp au simu yako unaitumia kwa ajili ya mawasiliano; muhimu kuanzia sasa tambua kuwa unatembea na nyenzo muhimu ya kujitangaza kwa watu wengi zaidi tena nyenzo yenye uwezo wa kuvuka mipaka ya nchi, mabara na bahari kwa muda mfupi sana.
✍πΎ Je unafahamu kuwa mfumo wa maisha umebadilika kutokana na ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano? Ukuaji wa mitandao ya kijamii umebadilisha mfumo mzima wa maisha ya jamii. Kila mtu kuanzia vijana hadi wazee wanatumia mitandao hii. Mitandao ya kijamii imebadilisha utaratibu mzima wa namna ambavyo watu wanaanzisha au kukatisha mahusiano; ukaribu wa wanafamilia; au namna ambavyo watu wanaingia kwenye ajira. Je unafahamu kuwa hiyo ni fursa kwako kutangaza bidhaa au huduma zako?
✍πΎ Je unafahamu kuwa kwa sasa mitandao ya kijamii ndo sehemu pekee yenye ufanisi wa matangazo ya biashara kwa sasa? Njia za matangazo ambazo zimekuwepo toka zamani kama vile mfumo wa kutumia magazeti, mfumo wa kutumia digitali kama vile televisheni vyote kwa pamoja vimetekwa na mfumo wa mitandao ya kijamii. Kwa sasa ni rahisi sana kuwafikia walengwa wa huduma au biashara zako kwa kutumia mitandao ya kijamii kuliko ilivyo kwenye mfumo wowote ule wa matangazo. Mfano, ilichukua zaidi ya miaka 13 kwa watu milioni 50 kutumia redio au television lakini kwa mtandao wa instangram imechukua kipindi cha mwaka mmoja na nusu kufikia idadi hiyo ya watu.
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa simu janja yako ni kitega uchumi ambacho ambacho pengine hukuwahi kukiorodhesha kati ya vitega uchumi ulivyonavyo. Unaweza kuitumia mitandao ya kijamii kujitangaza kibiashara au unaweza kuendelea kutumia mitandao hii kama sehemu ya kujaza picha zako za ukweli na uongo. Zinduka wakati ni sasa wa kutangaza bidhaa au huduma zako kupitia huduma ya matangazo kwenye mitandao ya kijamii. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
https://fikrazakitajiri.blogspot.com/2020/01/orodha-ya-vitabu-nilivyosoma-katika.html?m=1.
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(