NENO LA LEO (AGOSTI 12, 2020): JE UNAHITAJI KUWA TAJIRI? UBEPARI NI NJIA SAHIHI KUKUFIKISHA HUKO.
ππΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza pale ulipoishia jana. Kipekee ni asubuhi ambayo hatuna budi kumshukuru Mungu kutokana na baraka anazotutendea katika maisha yetu ya kila siku. Basi kwa pamoja tuseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii ili nipate yaliyo bora katika maisha.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza umuhimu wa kuwa na tabia za kibepari katika safari yako ya kuwa tajiri. Kwa kifupi “Bepari (Capitalist)” ni mtu ambaye analenga kutengeneza faida kutokana na kuwekeza mtaji (capital investments) au uendeshaji wa biashara binafsi. Mara nyingi Mabepari ni watu ambao hawapendwi katika jamii kwa kuwa misingi ya kipebari huwa inahusisha kutanguliza maslahi binafsi kabla ya ya maslahi ya wengine kama ilivyo kwenye ujamaa. Ndiyo maana matajiri wengi huwa hawapendwi kuwa jamii inawaona kana kwamba ni watu wachoyo, wenye dhuruma na wabinafsi.
✍πΎ Hata hivyo, ukweli ni kwamba iwe tajiri au masikini kila mtu huwa anatanguliza maslahi yake kwanza kabla ya maslahi ya wengine. Ni kutokana na ukweli huu hatuwezi kuzungumzia maendeleo katika historia ya mwanadamu bila kuzungumzia mchango wa mabepari. Ubepari umekuwa ni sehemu ya kuhamasisha ubunifu ambao kila mara umekuwa zawadi kwa jamii na tunu kwa mgunduzi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba unapogundua teknolojia mpya ni lazima ilete huduma/bidhaa mpya kwenye jamii. Bidhaa/huduma hii ni lazima iwe bora ikilinganishwa na zilizopo hivyo jamii itafaidika kwa matumizi ya teknolojia hii huku mgunduzi akiendelea kupata faida.
✍πΎ Moja ya sifa ya bepari (capitalist) ni kuvumbua bidhaa/huduma zenye wigo mpana wa machaguo kwa wateja wake. Mara zote bepari analenga kuwapa wateja kitu ambacho wanapenda kila siku ikilinganishwa na bidhaa/huduma nyingine zilizopo sokoni. Ni kutokana na sifa hii, Mabepari wamekuwa na mchango mkubwa wa kuibadilisha dunia hii kuwa mahala pema pa kuishi kwa viumbe vilivyopo na vijavyo. Mfano, Kampuni ya Google na Apple ni baadhi ya makampuni ambayo yana misingi ya kibepari na mchango wa kampuni hizi kwa ulimwengu wa sasa unajipambanua vizuri kwa kila mtu.
✍πΎ Mabepari wanaamini katika msingi wa kuanza kidogo, kukuza biashara na hatimaye kutanua biashara husika. Ubunifu wa kibepari ni lazima uzingatie misingi ya kuanza na kidogo na hatimaye kuweza kupenya soko kwa hustadi wa hali ya juu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba pindi unaanza ni rahisi kutawala soko dogo ikilinganishwa na soko kubwa. Fikiria mwanzilishi wa Facebook alivyoanzisha mtandao huu akiwa na lengo la kuwakutanisha wanafunzi wenzake. Leo hii Facebook ni mtandao wa kijamii ambao unaoongoza kuwa na watumiaji wengi duniani.
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa ubepari ni hatua muhimu katika safari ya kutengeneza utajiri. Hapa ndipo tunaweza kuona kuwa ubepari ni safari yenye kuhusisha “vitendo na athari zake (cause and effect)”. Kwa kifupi ni kwamba ili uvune ni lazima uwe umepanda mbegu na si vinginevyo na baada ya kupanda kiwango cha mavuno yako kitategemea bidii na uvumilivu wako katika kutunza miche shambani mwako. Huo ndio ubepari halisi. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
https://fikrazakitajiri.blogspot.com/2020/01/orodha-ya-vitabu-nilivyosoma-katika.html?m=1.
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(