NENO LA LEO (AGOSTI 9, 2020): HIZI NDIZO SIRI 5 ZA KUJIAMINI UNAPOONGEA MBELE ZA WATU.
ππΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni wakati ambao tumeamka tukiwa wazima wa afya na tupo tayari kuianza siku kwa kutekeleza majukumu yaliyopo mbele yetu. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza siri tano za kuongea mbele za watu. Wote kwa pamoja tunakubaliana kuwa sifa mojawapo ya kufanikiwa katika maisha iwe kwenye sekta ya kiroho, kiuchumi, kijamii na kimwili ni lazima ujifunze kuzungumza na watu. Hata hivyo, linapokuja suala la kujieleza mbele za watu, watu wengi wanashindwa kufanya hivyo kutokana na hofu ya kuhisi hawataeleweka. Ni kutokana na hali hii watu wengi wanaweza kujieleza kwa maandishi lakini wengi wao wanashindwa kuongea kile walichoandika.
Karibu tujifunze siri tano mhimu za kuzingatia pale unapoongea mbele za watu:-
✍πΎ Siri #1: Unapoongea mbele za watu jitahidi kuwa wewe. Hii ina maana kuwa usiogope umati unaokuzunguka kwa kuhisi kuwa labda kuna watu wenye uelewa mkubwa zaidi yako. Ni kawaida kuwa na hofu wakati unajiandaa kuwasilisha mada, hivyo, wajibu wako ni kuhakikisha unashinda hofu hiyo kabla ya kusimama mbele za watu. Njia bora ya kuishinda hofu ni kufanya maandalizi ya kutosha ili uwe na uelewa mpana kwenye mada yako.
✍πΎ Siri #2: Hakikisha wazo/mada yako ina mashiko/thamani. Kila mwenye wazo lenye mashiko au thamani anao uwezo wa kushirikisha hilo kwa wengine. Haijalishi kiwango cha kujiamini ulichonacho, uwezo wako wa kuongea kwa haraka au uwezo wa kumudu hadhira yako. Silaha muhimu ambayo unatakiwa kuwa nayo ni wazo lenye thamani au maana kwa wanaokusikiliza.
✍πΎ Siri #3: Yafanye maongezi/wasilisho lako kuwa na sifa ya safari kwa msikilizaji. Mfanye msikilizaji ajione yupo kwenye safari yenye kila aina ya vitu vipya na uzoefu wa kila aina ambao hajawai kuupata katika maisha yake. Maongezi yako yawe sawa na filamu au kitabu cha simulizi ambacho kila mara kinakuhamasisha kusoma ukurasa unaofuata. Hali hii itamfanya msikilizaji ajenge picha katika akili yake na hivyo kuwa na hamasa ya kuendelea kukusikiliza.
✍πΎ Siri #4: Epuka mada yenye mlengo wa kutangaza sifa zako kana kwamba unatangaza bidhaa kwa ajili ya kununuliwa. Watu wengi wanafanya makosa kiasi ambacho pale wanapoongea wanaishia kueleza sifa walizonazo au mafanikio yao. Kumbe wanachotakiwa kufanya ni kuwasilisha wazo au mada kwa ufasaha ili kupitia wasilisho hilo wafanikiwe kujenga heshima au uaminifu a kwa wasikilizaji wao. Mara zote lenga kumpatia msikilizaji kitu kipya badala kufikiria utapata nini kutoka kwake.
✍πΎ Siri #5: Epuka maongezi yasiyo na dira. Hii inajumuisha makosa ambayo mtoa mada anazama kueleza vitu ambavyo vipo nje ya kusudio la mada anayowasilisha. Matokeo yake ni mtoa mada kueleza vitu vingi ambavyo havina uhusiano na mada aliyokusudia kuwasilisha. Hali hii inafanya wasikilizaji wakose hamasa ya kuendelea kukusikiliza. Kumbuka kuwa watu wanakupa dakika chache katika maisha yao kwa ajili ya kusikiliza vitu vya kipekee au vipya wasipovipata wataondoka.
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza siri tano za kujiamini pale unapoongea mbele za watu. Pia, tumeona kuwa maongezi ndio msingi wa mafanikio kwenye kila sekta ya maisha yetu. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaona tofauti katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
https://fikrazakitajiri.blogspot.com/2020/01/orodha-ya-vitabu-nilivyosoma-katika.html?m=1.
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(