NENO LA LEO (AGOSTI 10, 2020): FAHAMU NJIA 2 AMBAZO ZINAZALISHA WATU WA TABAKA MASIKI NA TABAKA TAJIRI.
ππΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya katika juma jipya ambapo tumependelewa kwa kupewa kibali cha kuendelea kutengeneza maisha yenye thamani. Ni asubuhi naendelea kukumbusha kuwa husidharau hatua fupi fupi kama endapo hatua hizo zina mwelekeo wa kukufikicha kwenye kilele cha mafanikio unayotamani. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza njia mbili ambazo zinaendelea kutengeneza matabaka mawili ya masikini na matajiri vizazi na vizazi. Tembelea eneo lolote kwenye jamii yoyote ni lazima utakutana na matabaka tofauti ya watu. Kwenye jamii yoyote ni lazima pawepo tabaka la wenye nacho na tabaka la hoehae (wasiyonacho). Swali la kujiuliza ni je matabaka haya huwa yanatengenezwa na nini?
✍πΎ Kuna njia mbili ambazo zinahusika kutengeneza matabaka haya kwenye jamii. Njia hizi zote zinauhusiiano wa moja kwa moja na pato na matumizi ya watu katika jamii husika. Masikini anajitengeneza mwenyewe kupitia fikra, mtazamo, tabia na vitendo vyake kwenye kila shilingi inayoingia mikononi mwake. Vivyo hivyo tajiri anajitengeneza mwenyewe katika kipindi cha maisha yake. Kupitia fikra, mtazamo na matendo dhidi ya pato lake anaweza kujitofautisha na kundi la watu wengine katika jamii yake.
✍πΎ Njia #1: Njia inayozalisha masikini. Njia hii inakimbiliwa na watu wengi kwa kufahamu au bila ufahamu wao. Katika njia hii wahusika huwa wanaishi maisha ya kuigiza ili waonekane wana maisha mazuri kumbe ndani ya mioyo wamejawa na huzuni, hofu na mawazo mengi ambayo huwa yanauhusiano mkubwa na ufinyu wa pesa. Njia hii inahusisha wahusika kununua vikolokolo (liabilities) ambavyo havina thamani kwenye siku za baadae na thamani yake hupungua kadri siku zinavyosogea. Kwa ujumla wahusika katika njia hii huwa wananunua vitu ambavyo vinaendelea kuwagharimu kila mara katika maisha yao.
✍πΎ Njia #2: Njia ya utajiri. Njia hii haina jamu kwa kuwa wanaifuata huwa ni wachache. Ni njia ambayo ina watu wenye mtazamo na fikra huru. Ni njia ambayo wahusika huwa wanatumia hela yao kununua vitu vya thamani (assets) ambavyo kadri siku zinavyosogea thamani ya vitu hivyo inaongezeka. Wahusika katika njia hii kabla ya kununua kitu wanajiuliza thamani ya kitu hiko katika siku za baadae.
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza njia mbili ambazo zinatengeneza matabaka mawili katika jamii. Njia hizo zipo wazi kwa kila mtu. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaona tofauti katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
https://fikrazakitajiri.blogspot.com/2020/01/orodha-ya-vitabu-nilivyosoma-katika.html?m=1.
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(