HIZI NI SIRI AMBAZO HAZIONEKANI KATIKA MAFANIKIO YA MTU

NENO LA LEO (AGOSTI 22, 2020): HIZI NI SIRI AMBAZO HAZIONEKANI KATIKA MAFANIKIO YA MTU.

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni faraja kwangu kuona tumebahatika kupewa kibali cha siku za uhai wetu hapa duniani. Ni katika asubuhi nafarijika zaidi pale ninapoona nimefanikiwa kuendeleza kazi hii kwa faida ya kizazi hiki na vizazi vijavyo. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza kuhusu siri ambazo zimejificha kwa watu waliofanikiwa. Mara nyingi katika jamii tunayoishi tumezoea kuona watu wanajadili mafanikio ya watu wengine. Katika majadiliano hayo wengi huwa wanaishia kuponda ili mradi watu wenye mafanikio waonekane wamepata mafanikio waliyonayo kwa njia zisizo halali. Hapa ndipo huwa watu wanasahau kuwa wanapojadili mafanikio ya wengine wanachojadili ni kile kinachoonekana kwa macho. Hapa huwa wanasahau kuwa hayo yanayoonekana yanaaumbwa na siri zisizo onekana kwa wengi. Karibu tupitie siri ambazo zimejificha kwa watu wenye mafanikio:-

✍🏾 Siri #1: Mafanikio ni zao la kufanya kazi kwa bidii, weledi na kuwa na uvumilivu. Ni sheria ya asili ya kuwa kila mmoja anavuna kulingana na jitihada anazoweka wakati wa kupanda. Pia mavuno yana uhusiano mkubwa na jinsi mhusika  anavyovumilia katika kipindi cha kupalilia miche ili ifikie hatua za kuzaa matunda. Wanaojadili mafanikio ya watu huwa hawana muda wa kuangalia mhusika aliweka jitihada katika kazi na wala hawana muda wa kujiuliza amevumilia muda kiasi gani hadi kufikia hatua aliyonayo.

✍🏾 Siri #2: Kuchelewa kulala na kuwahi kuamka. Watu wengi waliofanikiwa mara nyingi huwa ni wa mwisho kulala na wa kwanza kuamka. Watu wenye akili nyepesi ambao kazi yao huwa ni kujadili wengine wenyewe huwa wanalala mapema na wanachelewa kuamka. Hapa unaweza kuona kuwa watu wenye mafanikio huwa wanafikia mafanikio hayo wakati wengine wamelala.

✍🏾 Siri #3: Kukataliwa, kukosolewa na kushindwa. Muulize mtu yeyote mwenye mafanikio jinsi alivyofikia  mafanikio yake moja kwa moja atakuambia haikuwa kazi rahisi kufikia hatua hiyo. Wengi wamekataliwa na kukosolewa zaidi kuhusu kile ambacho waliamini ni sahihi. Wengi walionekana kana kwamba wanapoteza muda pamoja na rasilimali na hawawezi kufika mbali. Wengi walianguka kutokana kushindwa mara ngingi hila walisimama na kujifuta vumbi na kusonga mbele. Watu hawa kwa KUJITAMBUA na kuwa na UVUMILIVU walisimamia kile wachoamini ni sahihi hadi kufikia mafanikio yanayoonekana kwa sasa.

✍🏾 Siri #4: Nidhamu pamoja na kutoa sadaka. Hauwezi kufanikiwa kama hauna nidhamu kwenye kanuni na misingi ya mafanikio. Vivyo hivyo, hauwezi kufanikiwa ikiwa haupo tayari kutoa sadaka. Mafanikio yanaambatana na kutoa sadaka ya muda, rasilimali na nguvu. Ni lazima uwe tayari kujinyima baadhi ya vitu au kukosa ukaribu na baadhi ya watu uliozoeana nao.

✍🏾 Siri #5: Hofu inayoambatana na kubeba hatari (risk) katika yale wanayofanya. Muulize mmiliki yeyote wa chombo cha usafirishaji wa mizigo au abiria ndipo utagundua hofu anayokuwa nayo wakati vyombo vyake vinapokuwa kwenye majukumu yake. Mafanikio yanahitaji kuwa na roho ngumu hasa pale unapotakiwa kuwekeza sehemu ambayo haujawahi kuwekeza. Fursa nyingi zinawezaonekana fursa awali lakini baada ya kuingia ndipo unagundua kuwa haikuwa fursa sahihi.

✍🏾 Mwisho, neno la tafakari ya leo linatufundisha kuwa mafanikio yoyote yale katika maisha yanaundwa na tabia ambazo hazionekani kwenye macho ya watu. Watu wanajadili yanayoonekana kwa macho na kusahau kuwa mafanikio hayaji kwa siku moja. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaona tofauti katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(