NENO LA LEO (JULAI 31, 2020): JIFUNZE UWEKEZAJI WA HISA KAMA MOJA YA UWEKEZAJI WA MTAJI

👉🏾 Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama ukiwa na hamasa na nguvu za kutosha kwa ajili ya kuendeleza pale ulipoishia jana. Nitumie nafasi hii kuwatakia kheri ya siku kuu ya Eid al-Adha wenzetu wa dini Kiislamu. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambao tutajifunza kuhusu uwekezaji wa hisa. Somo limeandaliwa kutokana swali la mwenzetu ambaye aliniuliza kuhusu hisa na namna mtu anavyoweza kuwekeza mtaji wake. Labda kwa kifupi nianze kwa kusema kuwa ukwezaji kwenye hisa ni watu wachache sana hasa kwa vijana ambao wanafahamu. Pia, vijana wengi hawavutiwi na uwekezaji wa hisa kwa vile walio wengi wanataka utajiri wa haraka. Uwekezaji wa hisa unabadirika kila wakati na hivyo ni uwekezaji ambao kabla ya kuwekeza unahitaji kufahamu mabadiliko ya namna hiyo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba soko la hisa linaendeshwa na hisia za wanunuaji pamoja na wauzaji wa hisa.

✍🏾 Kwa ujumla tunakiwa kujifunza kuwa hisa ni mfumo wa uwekezaji unaowezesha wamiliki wa kampuni husika kugawana mali zinazomilikiwa na kampuni au mali zinazozalishwa na kampuni ndani ya kipidi husika. Ugawanaji wa mali hizi unategemea na kiasi ulichowekeza kwenye kampuni husika. Hivyo unavyonunu hisa za kampuni flani na wewe unakuwa ni moja wa wamiliki wa kampuni hiyo kulingana na kiasi cha hisa unazomiliki. Maamuzi kuhusu uendeshaji wa kampuni husika huwa yanafanyika kwa kuzingatia wingi wa hisa ambazo unamiliki. Tafsiri yake ni kwamba mwenye hisa nyingi anakuwa na sauti kuliko mwenye hisa kidogo.

✍🏾 Je soko la hisa ni nini? Kama ambavyo tunafahamu kuwa soko ni sehemu inayounganisha watu zaidi ya mmoja kwa ajili ya kufanya biashara ana kwa ana au kwa kuunganishwa na mtandao wa interneti. Soko la hisa pia lina maana hii kwa kuwa ni mtandao wa kifedha unaowaunganisha watu kwa ajili ya kuuza au kununua umiliki wa hisa. Soko hili linafanya kazi sawa na masoko mengine kwa maana misingi muhimu ya masoko kama vile ushindani kwenye soko. Hii ina maana kwamba kama unauza hisa zako unahitaji wateja makini wa kununua hisa zako na kama unanunua unahitaji wauzaji makini wa kuuza hisa.

✍🏾 Unapoamua kununua au kuuza hisa fanya hivyo kwa dhana ya kuwa bei ya wakati huo ni halisi kwa maana ya kwamba hisa husika haiuzwi kwa bei ya juu/chini kuliko thamani yake. Hata hivyo, unahitaji kukumbuka kuwa hata kama bei ni halisi bado bei hiyo si ya uhakika kwani inaweza kubadilika ndani ya masaa au siku. Na hii ndio itathibitisha kuwa bei husika ilikuwa/haikuwa halisi. Na hivyo uwekezaji wa hisa ni biashara ambayo muhusika ni lazima awe tayari kubeba hatari (risk) kwani hakuna ambaye anajua bei ya hisa za kampuni fulani zikuwa na thamani gani siku zijazo.

✍🏾 Unapowekeza kwenye hisa unategemea kufaidika kupitia ongezeko la thamani ya hisa za kampuni husika pamoja na gawio kwa wanahisa kulingana na idadi ya hisa zako. Hapa unahitaji kujifunza vitu viwili; moja, kama thamani ya hisa za kampuni husika itashuka basi na wewe utegemee kupata hasara kwenye uwekezaji wako (mtaji) na endapo thamani ya hisa ikiongezeka ndivyo na wewe mtaji wako utaogezeka. Mbili, gawio la kila mwaka linakokotolewa kulingana na faida iliyotengenezwa na kampuni katika kipindi husika. Kama kampuni imepata hasara ndani ya kipindi husika tegemea kupata gawio kidogo. Hizi pia ni tofauti nzuri kati ya uwekezaji wa kwenye hisa na dhamana kwani uwekezaji wa kwenye dhamana hautegemei faida iliyotengenezwa au kupanda na kushuka kwa thamani kama ilivyo kwenye hisa.

✍🏾 Gawio linaweza kulipwa kwa mfumo wa hisa au kwa mfumo wa pesa taslimu kulingana na utaratibu wa kampuni husika. Hii ina maana kwamba kama kampuni inalipa gawio kwa mfumo wa hisa wawekezaji wanategemea idadi ya hisa zao kuongezeka kila mwaka kwa kutegemea faida iliyotengenezwa na kampuni husika katika kipindi hicho. Na pale kampuni inapotoa gawio kwa mfumo wa fedha taslimu maana yake ni kwamba idadi ya hisa za wawekezaji inaendelea kuwa ile ile kama hawajanunua hisa zaidi ndani ya kipindi husika na gawio lao hulipwa moja kwa moja kwenye akaunti zao au kwa cheki kila mwaka kulingana na faida iliyotengenezwa.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza juu ya uwekezaji wa his ana soko la hisa jinsi linavyofanya kazi. Kwa hapa Tanzania Soko la Hisa ni Dar es Salaam Stock Exchange ambalo lina jumla ya Kampuni 21 ambazo zimejiorodhesha kuuza sehemu ya umiliki wa kampuni (hisa). Hata hivyo, kwa hapa kwetu siyo rahisi kufaidika na uwekezaji wa hisa kama bado ndo unaanza na mtaji wako ni kidogo. Hii inatokana na thamani ya hisa za kampuni nyingi kutoongezeka kwa kipindi kirefu na wakati mwingine thamani ya hisa huwa inashuka kuliko kupanda. Unaweza kufaidika kupitia gawio ambalo huwa linatolewa kila mwaka kulingana na faida iliyotengenezwa na kampuni kwenye mwaka husika japo pia unatakiwa uwe na kiwango cha juu cha hisa unazomiliki kwa maana uwe na mtaji mkubwa ambao umwekeza. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujifunza zaidi kuhusu uwekezaji wa hisa na dhamana kwa kununua uchambuzi wa vitabu viwili ambavyo: (a) How the Stock Market Work ambacho kimeandikwa na Profesa Ramon P. DeGennaro wa Chuo Kikuu cha Tennessee, Knoxville; na (b) The Warren Buffet Way” kutoka kwa mwandishi Robert G. Hagstrom. Uchambuzi wa Vitabu vyote unapatikana kwa gharama ya OFA ya Tshs. 5,000/= badala ya elfu kumi.
👐🏾 Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI ili upate mafundisho haya kila siku, bofya link hii: https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com




onclick='window.open(