FAHAMU UGUMU ULIPO WAKATI WA KUANZA UTEKELEZAJI WA MAFANIKIO UNAYOTAMANI

NENO LA LEO (AGOSTI 19, 2020): FAHAMU UGUMU ULIPO WAKATI WA KUANZA UTEKELEZAJI WA MAFANIKIO UNAYOTAMANI.

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya ambayo tumepata kibali tena cha kuendelea kuwa bora katika maisha yetu. Ni siku ambayo naendelea kukumbusha kuwa husiogope ndoto kubwa uliyonayo na badala yake hakikisha kila siku unafanya kitu ambacho kinakusogeza kwenye mafanikio ya ndoto hiyo. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza juu ya hatua ngumu wakati wa kuanza kutekeleza mafanikio unayotamani. Hadi sasa tunafahamu kuwa unapokuwa na hitaji  katika maisha yako husipochukua hatua yoyote ya kulitafsiri hitaji hilo katika vitendo litaendelea kuwa ndoto. Pia tunafahamu kuwa ndoto hisipotekelezwa huwa inapotea katika fikra za mhusika.

✍🏾 Kupitia neno la tafakari hii tunajifunza kuwa unapokuwa na ndoto hatua inayofuata ni kuitafsiri ndoto hiyo katika hatua za utekelezaji. Hata hivyo kati ya hatua zote ambazo utatakiwa kupiga ni lazima ufahamu kuwa hatua ya kwanza huwa ngumu kuliko zote. Hatua ya kwanza mara zote huwa inaogopesha na ndiyo maana watu wengi wanaishia kwenye kutamani tu (ndoto). 

✍🏾 Hatua ya kwanza huwa inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahusisha mhusika kujiona bado hajawa tayari kuanzisha safari. Utayari huu mara nyingi huwa unahusisha mhusika kujiona hana rasilimali, ujuzi, muda na watu sahihi wa kuanzisha safari yake. Ni kutokana na changamoto hii, watu wengi wanakabiliwa na ugonjwa wa kuhairisha ambao una dalili za kusogeza hatua za utekelezaji mbele. 

✍🏾 Hata hivyo, pale ambapo hatua ya kwanza inatekelezwa huwa njia ya kurahisisha hatua nyingine zote zilizopo mbele ya safari. Mfano, wakati unaanzisha biashara hakuna taasisi ya kifedha ambayo itakuwa tayari kukupatia mkopo kama tulivyoona kwenye neno la tafakari ya jana. Cha kushangaza ni kwamba ukishafanikiwa kuanzisha biashara ikasimama, kila taasisi ya fedha itaanza kukushawishi ukachukue mkopo kwao. Ndivyo ilivyo, ni lazima upambane kwenye kukamilisha hatua ya kwanza ili kupitia hatua hiyo hatua nyingine zote zionekane kuwa rahisi.

✍🏾 Mwisho, neno la tafakari ya leo limetufunulia wakati ambao ni mgumu pale tunapohitahiji kuziishi ndoto tulizonazo. Hata hivyo, hatupaswi kuogopa kuchukua hatua ya kwanza kwa kuwa kupitia hatua hiyo hatua nyingine zote huwa zinarahisishwa kutokana na mafanikio ya hatua za awali. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaona tofauti katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(