ELIMU YA DARASANI? FAHAMU MAMBO AMBAYO HAYAFUNDISHWI DARASANI!.

NENO LA LEO (AGOSTI 23, 2020): ELIMU YA DARASANI? FAHAMU MAMBO AMBAYO HAYAFUNDISHWI DARASANI!.

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya katika siku hii ya jumapili ambayo tunapewa kibali cha kuendeleza thamani kwa jamii inayotuzunguka. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza tabia za mfanikio ambazo hautofundishwa shuleni. Mara nyingi tumezoea kusikia malalamiko ya watu kuhusu mfumo wa elimu kwa jinsi ambavyo unamuandaa mwanafunzi kujitegemea  mara baada ya kuhitimu. Malalamiko haya siyo tu kwa Tanzania maana mfumo wa elimu uliopo ni tatizo la kidunia. Nimesoma vitabu vingi ambavyo vimeandikwa na waandishi kutoka sehemu tofauti na wengi wanaogusia mfumo wa elimu wanaonesha jinsi ambavyo haumuandai mwanafunzi kujitegemea baada ya kuhitimu. Mfano, ukisoma karibia kila kitabu cha Robert Kiyosaki utaona jinsi ambavyo anapingana na mfumo wa elimu uliopo sasa. Karibu tupitie tabia ambazo hautofundishwa kwenye mfumo wa elimu ya darasani:-

✍🏾 Tabia #1: Darasani hautofundishwa jinsi ya kuuza (how to sell) na jinsi ya kukubaliana bei (how to negotiate). Ikiwa wewe ni mwanafunzi wa kozi ya biashara au masoko, utakachofundishwa darasani ni maana ya kuuza. Ukibahatika zaidi utafundishwa tabia za wauzaji bora kulingana na mtaala wa elimu unavyoelekeza. Hapa utafundishwa kinadharia zaidi kwa ajili ya kujibia mtihani. Ukitaka kujua kuwa elimu ya darasani haifundishi mbinu za kuuza tafuta mwanafunzi bora darasani na Machinga, halafu wote wapatie bidhaa ambazo wanatakiwa waziuze kila mmoja kwa mbinu zake. Matokeo yatakushangaza kwa kuwa Machinga yawezekana hajawahi kuingia darasani lakini mbinu za kuuza alizonazo ni zaidi ya mwanafunzi aliyehitimu chuo kwenye kozi ya biashara au masoko.

✍🏾 Tabia #2: Jinsi ya kufikiri. Zunguka kwenye Vyuo vyetu kote ambako maelfu ya wanafunzi wanahitimu kila mwaka lakini hautofanikiwa kuona sehemu ambapo mwanafunzi anafundishwa namna ya kufikiri (how to think). Ndiyo maana jamii imejaa wasome wengi ambao wana fikra finyu. Upeo wa fikra wa wasomi wengi umejikita kwenye vitu alivyosomea na kidogo kwenye maeneo ya majukumu yake ya kazi. 

✍🏾 Tabia #3: Kukabiliana na kushindwa au kuanguka. Mfumo wa elimu uliopo unakandamiza uwezo wa wanafunzi kujifunza kutokana na makosa. Elimu sasa mwanafunzi anayekosea au kushindwa katika mtihani anaonekana hana akili ikilinganishwa na wale wanafaulu mitihani. Katika uhalisia wa maisha watu wanaofanya makosa mengi na kujifunza kutokana na makosa hayo wana nafasi kubwa ya kufanikiwa kimaisha. Wasomi wengi wanaendelea kuishi maisha magumi kwa kuwa mfumo wa elimu umewafundisha kukwepa makosa.

✍🏾 Tabia #4: Jinsi ya kuwekeza (how to invest). Uwekezaji ni sayansi na sanaa ambayo darasani utafundishwa maana ya uwekezaji, utapewa mifano kadhaa na pengine utafundishwa kuhusu ongezeko la thamani kulingana na uwekwzaji tofauti tofauti. Kitu ambacho hautofundishwa darasani ni jinsi gani unaweza kuanza kuwekeza ukiwa na mtaji mdogo. Sehemu zipi uwekeze pesa zako katika udogo huo wa mtaji wako. Mfano, nilisoma miaka 18 lakini sikuwahi kufundishwa kuhusu Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (UTT AMIS). Niliweza kujifunza kuhusu mifuko hiyo kwa kusoma makala moja tu.

✍🏾 Tabia #5: Jinsi ya kugunndua kusudi la maisha yako. Tuna Wasomi wengi ambao hawajui maisha yao ni kwa ajili ya ukamilisho wa kitu gani hapa Duniani. Kutokana na kutokujua jinsi ya kugundua kusudi la maisha yao wanaendelea kuishi maisha ya kuunga unga bila mafanikio. 

✍🏾 Tabia #6: Jinsi ya kuwasiliana (how to communicate well). Tuna wasomi wengi ambao hawawezi kuongea mbele za watu. Tuna wasomi wengi ambao haya kuwasilisha mada kwenye kundi la wanafunzi wenzao ni changamoto. Hali hii inatokana na wanafunzi hao kutokuufundishwa mbinu za kuongea mbele za watu.

✍🏾 Mwisho, neno la tafakari ya leo linatufundisha kuwa zipo tabia nyingi ambazo mfumo wa elimu uliopo hauzifundishi. Tabia hizi ni muhimu kwa mtu yeyote ambaye anahitaji kuishi maisha ya mafanikio. Kutofundishwa darasani si kigezo cha kwamba hauwezi kujifunza tabia hizo. Andaa mkakati wa kujifunza kila siku katika kipindi cha maisha yako. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaona tofauti katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(