FAHAMU WAKATI SAHIHI WA KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUTUMIA PESA ZA WATU WENGINE.

NENO LA LEO (AGOSTI 18, 2020): FAHAMU WAKATI SAHIHI WA KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUTUMIA PESA ZA WATU WENGINE.

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza nguvu na hamasa ile ile ili kufikia mafanikio unayotamani au kuliishi kusudi la maisha yako kwa ujumla wake. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza jinsi ya kutumia pesa za watu wengine kukuza biashara yako. Moja ya mbinu ambayo inatumiwa na matajiri wengi kuendelea kuwa tajiri ni uwezo wa kutambua namna ya kutumia pesa za watu wengine kwa faida. Mbinu waandishi wengi wa vitabu vya mafanikio wanaifupisha kwa silabi tatu tu "OPM" ambazo ni kifupisho cha maneno "Other People's Money (pesa za watu wengine)".

✍🏾 Kwa ujumla mbinu ya OPM inahusisha kutumia fedha ambazo siyo zako kukuza au kuanzisha biashara yako kwa njia halali. OPM inahusisha kuchukua fedha ambazo siyo zako kwa njia mikopo kutoka benki au taasisi yoyote ambayo inatoa huduma hiyo huku ukiwekewa utaratibu wa kurejesha kiasi ulichopewa. Jambo la kujifunza hapa ni kwamba unapotumia mbinu ya OPM ni lazima utambue kuwa hiyo siyo pesa yako hivyo ni lazima itumike kwa umakini ili upate kurejesha lakini wakati huo huo ukitengeneza faida kwenye biashara zako.

✍🏾 Je ni lini naweza kutumia mbinu ya OPM? Wakati sahihi wa kutumia mbinu hii ni pale ambapo unahitaji kukuza au kupanua wigo wa biashara yako. Husitumie OPM kama hauna uzoefu wa kutosha kwenye sehemu ambayo unaenda kuwekeza pesa hiyo. Kwa maana nyingine ni kwamba unapoamua kutumia OPM ni lazima utambue kuwa pesa hiyo siyo kwa ajili ya majaribio. Watu wengi wamefilisika kutokana na kutumia mbinu ya OPM kufanya biashara ambazo hawakuwa na uzoefu nazo na matokeo yake wakajikuta wanashindwa kurejesha pesa ya watu. 

✍🏾 Mwisho, neno la tafakari ya leo limetufundisha wakati upi sahihi ambao tunaweza kutumia pesa za watu wengine kukuza biashara zetu. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaona tofauti katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

https://fikrazakitajiri.blogspot.com/2020/01/orodha-ya-vitabu-nilivyosoma-katika.html?m=1.

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(