NENO LA LEO (AGOSTI 2, 2020): UTAWEZAJE KUFANIKIWA KAMA HAUPO TAYARI KUWAJIBIKA?

UTAWEZAJE KUFANIKIWA KAMA HAUPO TAYARI KUWAJIBIKA?

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi ambayo nimeamka salama nikiwa na nguvu na hamasa kwa ajili ya kuendeleza majukumu yangu ya siku ya leo.  Ni asubuhi ambayo hatuna budi kusema asanthe kwa Muumba kwa kutuongezea siku hii ya kipekee katika siku za uhai wetu. Basi kila mmoja wetu aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza umuhimu wa kuishi mzunguko wa uwajibikaji kama msingi namba moja wa kufikia mafanikio ya hitaji la maisha yetu. Watu wenye mafanikio ni wale ambao wanatambua kuwa wao ndiyo wahusika wakuu wa kufanikisha matokeo wanayotamani maishani mwao.

Badala ya kukalia kiti cha abiria katika safari ya maisha yako unatakiwa ukalie kiti cha dereva kwa ajili ya kuhimili usukani. Katika mzunguko wa uwajibikaji ni lazima utambue kuwa vitendo huleta matokeo na matokeo huamua aina ya vitendo vinavyohitajika. Watu wanaowajibika wanatambua kuwa kila tukio jema au baya wao ndiyo wahusika wakuu wa kulifanikisha au kulizuia katika maisha yao.

Unapokubali kuwajibika kwa ajili ya maisha yako utajikuta unafanikisha matokeo ambayo kwa wengine yanaendelea kuwa ni ndoto. Katika uwajibikaji mara zote unatakiwa kujikita kwenye matokeo unayotamani na kuhakikisha matokeo hayo yanajidhihirisha bila kusingizia kiwango cha ujuzi/maarifa, mazingira, hisitoria, mfumo wa Serikali au mahusiano yako kwa wakati huo.

Kila siku tunaalikwa kwa ajili ya machaguzi mawili: Kati ya kuwajibika kwa ajili ya matokeo tunayotamani au kutokuwajibika na kuacha asili ichukue mkondo wake. Kumbuka hauwezi kuwa pande zote mbili kwani ni lazima uchague upande mmoja wa shilingi kukubali kuwajibika au husiwajibike. Uchaguzi wa upande wowote utaleta matokeo sahihi katika maisha yako kulingana na upande umechagua.

Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa uwajibikaji ni msingi wa kufikia hitaji la maisha yako. Hauwezi kufanikiwa kama kila mara unasingizia wazazi, Serikali, mazingira, familia au kuwa na majukumu mengi kama kigezo cha wewe kutofanikiwa. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika maisha yako yatabadilika. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

https://fikrazakitajiri.blogspot.com/2020/01/orodha-ya-vitabu-nilivyosoma-katika.html?m=1. 

Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

 

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com


onclick='window.open(