Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza pale ulipoishia jana. Kumbuka mafanikio ya kitu chochote katika maisha yanapatikana pale unapokuwa na mwendelezo wa kazi au tukio husika katika maisha yako ya kila siku. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza namna ya kuwa na bahati katika maisha yako. Niliwahi kuandika hapa kuwa hakuna bahati kwa kuwa bahati huwa inawapata wale walijiondaa. Karibu ujifunze namna ya kuandaa bahati yako:-
Hatua #1: Fanya maandalizi (setting the stage). Hatu hii inahusisha kuweka maandalizi yote muhimu dhidi ya kufanikiwa kimaisha. Katika hatua hii unatakiwa kutambua sehemu zipi ambazo unahitaji kupata bahati. Unahitaji kujifunza ujuzi na maarifa mbalimbali, unahitaji kutoka kwa watu waliofanikiwa (wenye bahati ya kutengenezwa) na unahitaji kubadili tabia ili ziendane na tabia za wenye bahati ya kutengenezwa. Ukweli ni kwamba pale unapofanikiwa watu wasiojua jinsi ulivyoangaika kupata mafanikio hayo ndo wanajisemea jamaa ana bahati sana. .
Hatua #2: Badili mtazamo. Ikiwa utaendelea kujiona kuwa hauna bahati moja kwa moja ni kwamba hakuna siku bahati itakuja upande wako. Kumbuka bahati inawapata waliojiandaa kwa kuweka mazingira ambayo yanaivuta bahati husika. Mtazamo ulionao kuhusu bahati maishani mwako una nafasi kubwa ya kufungua au kuminya bahati nyingi maishani mwako. Hakikisha mtazamo wako uwe kila aina ya bahati unayohitaji ni lazima uandae mazingira ya kuifanikisha bahati hiyo.
Hatua #3: Gundua fursa zinazojitokeza. Ikiwa hauwezi kuziona fursa zilizopo mbele yako kamwe hauwezi kuwa na bahati maishani mwako. Kila mara unahitaji kujifunza namnna ya macho yako ya ndani kuona fursa zilizopo kwa ajili yako. Mara nyingi fursa huwa inaingilia mlango wa nyuma na wakati wa kutoka inatumia mlango wa mbele. Kipindi fursa inaingia ni wachache wenye macho yanayoona wanaoigundua na kipindi imeshakuwa siyo fursa ndipo wengi wanaiona na kuanza kuwaona waliochangamkia kuwa walikuwa na bahati.
Hatua #4: Kuwa mtu wa vitendo. Ikiwa unahitaji kupata bahati ni lazima ufahamu ni vitendo vipi sahihi unatakiwa kuchukua dhidi ya fursa zinazojitokeza. Ni lazima ufanye vitendo sahihi, sehemu sahihi na katika muda sahihi. Bahati haipatikani kama wewe una tabia ya kuahirisha au kusogeza mambo mbele. Linalowezekana leo hakikisha unachukua hatua stahiki kulikamilisha.
Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza zipo njia za kuivuta bahati kwenye maisha yako. Bahati huwa inawapata waliojiandaa na siyo wale wanaokaa kuisubiria. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika maisha yako yatabadilika. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI ili upate mafundisho haya kila siku, bofya link hii: https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com