PAMBANA NA UMASIKINI WA KIPATO LAKINI HUSISAHU KUWA HUU NDIYO UMASIKINI MBAYA ZAIDI

NENO LA LEO (AGOSTI 14, 2020): PAMBANA NA UMASIKINI WA KIPATO LAKINI HUSISAHU KUWA HUU NDIYO UMASIKINI MBAYA ZAIDI.

πŸ‘‰πŸΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi nyingine mpya ambapo tunaendelea kupewa kibali cha uhai. Kibali hiki ni muhimu katika siku za uhai wetu pale ambapo tutakitumia kuendelea kutoa thamani kwa jamii inayotuzunguka. Basi kwa pamoja tuseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza juu ya umasikini mbaya zaidi kuliko umasikini wa kipato. Linapotajwa neno masikini wengi wetu huwa tunakimbilia kutafsiri umasikini wa kipato. Ni kutokana na tafsiri hii wengi ambao wamejidhatiti kuishi maisha yenye uhuru wa kifedha wanapambana kila siku ili kuepuka umasikini wa kipato.

✍🏾 Pamoja na kupambana na umasikini wa kipato, wengi huwa wanasahau kuwa kuna umasikini zaidi ya huo. Ukiondoa umasikini wa kipato, maisha ya mwanadamu yanakabiliwa na umasikini wa kiroho pamoja na umasikini wa afya. Yamkini wengi wetu huwa tunapambana na umasikini wa kipato na kuacha mapambano dhidi ya aina nyingine za umasikini.

✍🏾 Kama ilivyo kwenye umasikini wa kipato, umasikini wa roho na afya huwa unaambatana na matatizo kwa mhusika kama vile: kukataliwa, kutopendwa, kunyanyapaliwa au kutojaliwa na jamii inayokuzunguka. Matatizo yote hayo huwa yanapelekea huzuni ya roho na maumivu ya mwili kwa mhusika. 

✍🏾 Hapa unaweza kugundua kuwa maangaiko dhidi ya kukabiliana na umasikini wa kipato yanaweza pelekea umasikini wa roho na afya. Ukweli ni kwamba watu wengi wapo radhi kukimbizana na pesa na kusahau mahitaji muhimu ya maisha kama vile kutoa upendo kwa wengine ili nao wapendwe. Pesa haiwezi kununua furaha yako kwa kuwa kadri unavyofikia ngazi flani ya kiwango cha pesa ndivyo unatamani kufikia ngazi ya juu zaidi.

✍🏾 Ukweli ni kwamba kadri tunavyoangaika kupambana na umasikini wa kipato ndivyo tunajikuta tunakosa muda wa kujali afya yetu sambamba na kukosa muda wa kuwa karibu na wapendwa wetu. Maisha yenye furaha ni yale ambayo mhusika ameweza kulinganisha (balance) mizania ya nguzo zote za umasikini.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa kuna umasikini mbaya zaidi ya umasikini wa kipato ambao unahusisha kukosa chakula, mavazi na nyumba. Tuna wajibu wa kuhakikisha tunatafuta maisha yenye mlinganyo ili tuwe na furaha katika siku za uhai wetu. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

https://fikrazakitajiri.blogspot.com/2020/01/orodha-ya-vitabu-nilivyosoma-katika.html?m=1.

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(