NENO LA LEO (AGOSTI 13, 2020): SHUKURU KWA KWA KILE ULICHONACHO LAKINI KUMBUKA SIYO DHAMBI KUHITAJI ZAIDI.
ππΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya katika siku za uhai wetu hapa Duniani. Ni siku ambayo naamini wote tumeamka salama na tupo tayari kuendeleza pale tulipoishia. Basi kwa pamoja tuseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii ili nipate yaliyo bora katika maisha.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza umuhimu wa kuwa mtu wa shukrani. Tuna wajibu wa kushukru kwa kila jambo na kwa kila hatua ambayo tumefikia. Nasema ni wajibu kwa kuwa kadri unavyoshukuru hata kwa kitu kidogo ndivyo utaongezewa zaidi. Hata pamoja na kushukuru tunatakiwa kuendeleza ile roho ya kutokuridhika na hatua tuliyopo. Mara nyingi nimekuwa nikisisitiza kuwa maisha ya mwanadamu yanakuwa ya thamani pale ambapo kila hatua inafungua nafasi ya kukua au kuongezeka zaidi. Hivyo kila siku sema asanthe lakini sema sitakufa mpaka niwe nimekamilisha lengo hili katika maisha yangu.
✍πΎ Sema asanthe lakini lenga kuongezeka zaidi kiuchumi. Ni makosa kuridhika na hatua ya kifedha au rasilimali unazomiliki. Kila siku ya uhai tunaojaliwa kuishi hapa Duniani tuna wajibu wa kulenga kuongezeka zaidi kiuchumi kuliko tulivyokuwa jana. Uchumi wako unatakiwa kuongezeka kila mwaka na ili ufanikiwe kwenye hilo ni lazima uwe mtu wa kutoridhika na hatua unayopiga.
✍πΎ Lenga kuongezeka zaidi kiroho. Kila siku lengo linatakiwa kuomba Mungu akuwezeshe ujijue au kujitambua zaidi ili kwa kufanya hivyo uone matendo yake makuu katika maisha yako. Mara zote katika safari ya kiroho tunakumbushwa kuwa katika maisha bado hatujafika mwisho wa safari kwa kuwa sisi so wakamilifu. Ni kutokana na hilo tuna wajibu wa kuongezeka zaidi kiroho katika maisha yetu ya kila siku.
✍πΎ Lenga kuongezeka zaidi kimahusiano. Mahusiano bora ni yale ambayo kila siku wahusika wanakuja na vionjo vipya. Ni kutokana na vionjo hivyo wenza hao watendelea kujiona wapya kwa kuwa kuna ubunifu ndani mwao.
✍πΎ Lenga kuwa bora zaidi kiafya. Afya ni msingi wa mafanikio yako kwa kuwa mwili wenye afya dhaifu hauwezi kufanya kazi. Mara zote unatakiwa kuweka mikakati ya kuboresha afya yako kwa kuhakikisha unakula kwa kuzingatia kanuni za mlo bora, kula kwa wakati, kuepuka vinjwaji visivyo vya lazima, kufanya mazoezi na kupata muda wa kutosha wa kupumzika.
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa tuna wajibu wa kushukuru kwa kila jambo na kila tunaposhukuru tukumbuke kutaka kuongezeka zaidi katika kila sekta ya maisha yetu. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
https://fikrazakitajiri.blogspot.com/2020/01/orodha-ya-vitabu-nilivyosoma-katika.html?m=1.
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(