WEMA NI MUHIMU LAKINI HAKIKISHA WEMA WAKO HAUZIDI KIPIMO.

NENO LA LEO (AGOSTI 20, 2020): WEMA NI MUHIMU LAKINI HAKIKISHA WEMA WAKO HAUZIDI KIPIMO.

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya ambayo hatuna budi kusema asanthe kwa Muumba wetu kwa baraka ambazo anaendelea kutujalia. Ni Furaha yangu ni kuona kuwa tunaendelea kupata chakula cha ubongo kila asubuhi ambacho ndicho chakula muhimu kuliko vyote. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza umuhimu wa wema katika kuliishi kusudi la maisha yetu. Kila mmoja wetu kama binadamu wengine tunaishi katika jamii ambayo tunazungukwa na watu aina mbalimbali. Makundi haya ya watu yanaanzia kwa watu wa karibu katika familia, ndugu, jamaa na marafiki katika sehemu zetu za kazi. Katika makundi haya yote kinachotuunganisha kuwa wamoja ni matendo ya wema kati yetu.

✍🏾 Tunawajibika kutoa UPENDO kwa wengine kama sehemu ya matendo ya wema. Hata maandiko matakatifu yanasema mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe. Angalizo ninalokupa kupitia neno la tafakari ya leo ni kutoruhusu kupenda jamii inayokuzunguka zaidi ya unavyojipenda wewe. Tafsiri yake ni kwamba tunawajibika kutoa upendo kwa wengine lakini kadri tunavyofanya hivyo ni lazima tutangulize upendo wa nafsi zetu.

✍🏾 Kama sehemu ya wema tunawajibika KUSAIDIA wengine. Msaada wetu unaweza kuwa wa mawazo, vitu, ujuzi na matendo ya faraja kwa wahitaji. Hata hivyo, kadri tunavyotoa msaada kwa wengine neno la tafakari ya leo linatukumbusha kuwa kutoa msaada kulingana na uwezo wetu. Ni ajabu pale ambapo unajilazimisha kutoa msaada kwa wengine wakati wewe mwenyewe mambo yako hayapo sawa. Ishi maisha ambayo yanatokana na misingi unayoisimamia na siyo maisha ya kutaka uonekane mwema kwa wengine wakati ndani mwako unasikitika.

✍🏾 Mwisho, neno la tafakari ya leo linatufundisha kuwa WEMA ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Tunawajibika kutoa au kufanya matendo ya wema kwa wengine katika safari yetu ya kuelekea kwenye mafanikio. Hata hivyo, hatupaswi kutoa wema uliopitiliza zaidi ya uwezo wetu. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaona tofauti katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

https://fikrazakitajiri.blogspot.com/2020/01/orodha-ya-vitabu-nilivyosoma-katika.html?m=1.

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(