ππΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama ukiwa na nguvu na hamasa ya kutosha kuendeleza pale ulipoishia jana. Basi kila mmoja wetu aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza sifa muhimu ambazo kiongozi au mtendaji bora anapaswa kuwa nazo. Kwa ujumla mafanikio ya kiongozi bora yanatokana na ufanisi wake katika kujitawala mwenyewe na hatimaye kupitia matendo yake ndo anafakiwa kuwa mfano bora kwa wale anaowaongoza. Hauwezi kuwa kiongozi/mtendaji bora kama hauwezi kujitawala mwenyewe kwa kudhibiti hisia na matendo yako.
✍πΎ Akili, mawazo na ujuzi ni rasilimali muhimu kwa kiongozi/mtendaji japo ufanisi ni njia pekee inayobadilisha rasilimali hizi kuleta matokeo makubwa kwa muhusika. Hii ni kutokana na ukweli kwamba ufanisi ndio njia pekee ambayo wafanyakazi katika taasisi yoyote wanapaswa kuwa nayo kwa ajili ya kuboresha bidhaa na huduma kwa wateja wao.
✍πΎ Thamani ya kiongozi/mtendaji yeyote ni pale ambapo taasisi/watu wengine watanufaika na mchango wake. Mtendaji/kiongozi ni lazima maarifa na ubunifu wake uwasaidie wale waliopo chini yake na kupitia matendo yake wafuasi wake wapate hamasa na dira ya utendaji kazi kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma wa taasisi/kampuni kwa wateja wao.
✍πΎ Kiongozi/mtendaji anabeba taswira ya taasisi au kampuni anayoongoza. Kwa sifa hii watendaji wanapaswa kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi ili kuleta sifa bora kwa taasisi/kampuni zao. Hapa unapaswa kuwa makini katika kuishi utamaduni wa taasisi/kampuni yako na hatimaye kuhakikisha kila taarifa inayotoka nje inakuwa na ukweli juu ya taasisi/kampuni. Kwa maana nyingine ni kwamba mwonekano wa nje wa taasisi/kampuni unatakiwa kuwa ni zao la kazi inayofanywa na viongozi/watendaji wa kampuni/taasisi husika.
✍πΎ Watendaji/viongozi wanakuwa makini katika maeneo muhimu ya kazi zao kwa ajili ya ajili ya kupata matokeo bora katika maeneo hayo. Ili kufanikiwa ni lazima wajiwekee vipaumbele na kuhakikisha wanaishi kwenye vipaumbele hivyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mambo ya yanafanyika kulingana na umuhimu wa vipaumbele. Pasipo kufanya hivyo sio rahisi kwa watendaji/viongozi kupata ufanisi na matokeo yake ni kufanya vitu nusu nusu.
✍πΎ Watendaji/viongozi ni lazima watenge muda maalumu kwa ajili ya kuwa na vikao na wafanyakazi wao wa chini kwa ajili ya kuthamini mchango wao. Hapa mwandishi anatushirikisha kuwa ni muhimu sana kwa watendaji wa ngazi za juu kuwasikiliza waajiriwa wao ili wapate kufahamu maoni na ushauri wao kwenye sehemu ambazo taasisi au kampuni inaweza kuboresha ili kuongeza thamani ya huduma au bidhaa za taasisi/kampuni husika.
✍πΎ Viongozi/watendaji wanapaswa kuepuka tatizo la kuchanganya mambo yao ya mahusiano na majukumu yao ya kazi. Mwandishi hapa anatushirikisha kuwa kadri wafanyakazi wanavyokaa pamoja kwa kipindi cha muda mrefu ndivyo wanaanza kupoteza muda mwingi kwenye masuala ambayo hayaendani na majukumu ya kazi zao. Muda mwingi unapotezwa kwenye mawasiliano yasiyo ya lazima au kwenye maongezi ambayo hayana tija kwenye utoaji wa huduma kwa wateja.
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza sifa muhimu za kuwa kiongozi au mtendaji mwenye ufanisi katika majukumu yako ya kila siku. Kila mtu ni kiongozi bila kujali ngazi ya uongozi wako, hivyo, sifa hizo ni kwa ajili yako ili uongeze ufanisi kwenye majukumu yako ya kila siku. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
https://fikrazakitajiri.blogspot.com/2020/01/orodha-ya-vitabu-nilivyosoma-katika.html?m=1.
ππΎNakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(