NENO LA LEO (AGOSTI 21, 2020): FAHAMU UHUSIANO ULIOPO KATI YA PESA, ELIMU NA MAISHA.
ππΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya ambayo natumaini tumeamka salama na tupp tayari kuendeleza pale tulipoishia jana. Ni asubuhi ambayo nakukumbusha kuwa husisahu kuwa mafanikio makubwa yanatokana na yale unayoyapa kipaumbele katika ratiba yako ya kila siku. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza uhusiano wa fedha, elimu na maisha. Tunafahamu kuwa pesa na elimu vyote vina mchango mkubwa kwenye mtazamo wa mhusika kuhusu maisha. Kupitia neno hili tutaangalia makundi manne ya watu ambayo ni: mwenye pesa nyingi sana lakini hana elimu, mwenye elimu lakini hana pesa, mwenye pesa pamoja na elimu na hasiye na pesa wala elimu. Ieleweke hapa kuwa elimu inayozungumziwa hapa siyo tu elimu ya darasani bali ni pamoja na upeo was maisha kwa ujumla.
✍πΎ Kundi 1: Mtu mwenye pesa nyingi sana lakini hana elimu. Mara nyingi tumezoea kusikia misemo kama vile: pesa ni sabuni ya roho, mwenye pesa si mwenyenzako au pata pesa tujue tabia zako halisi. Hii ni misemo ambayo inaelelezea jinsi watu wenye pesa wanavyoendesha maisha yao. Yawezekana misemo hii hisiwe na uhalisia kwa watu wote lakini kwa asilimia kubwa inabeba ujumbe kuhusu watu wenye pesa nyingi. Unapokuwa na pesa nyingi sana na wakati huo hauna elimu moja kwa moja pesa zinakufanya hukose mtazamo chanya wa maisha. Unapokosa mtazamo chanya moja kwa moja pesa zako zitapelekea ufanye vitu ambavyo vinakandamiza wengine au kupelekea anguko kwako.
✍πΎ Kundi 2: Watu wenye elimu lakini hawana pesa. Tumezoea kuambiwa kuwa elimu ni ufunguo was maisha. Msemo huu una ukweli kwa nadharia kwamba elimu inakupatia ufunguo kwa ajili ya kuingia kwenye uwanja mpana was maisha. Mafanikio katika uwanja huo yanategemea jinsi gani unatumia elimu yako kupata pesa kwa njia halali. Unapokuwa na elimu pekee bila pesa unakuwa na mtazamo finyu kuhusu maisha. Katika jamii hapa ndipo unakutana na watu ambao wanajiona wanafahamu kila kitu wakati yale wasiyoyajua ni mengi hila elimu imepofusha upeo wao wa kujifunza zaidi kuhusu maisha.
✍πΎ Kundi #3: Watu wenye pesa na elimu. Elimu na pesa kwa pamoja vinakupa maisha yenye mlinganyo. Mtazamo halisi na chanya unapatikana pale ambapo pamoja na kuwa na pesa unalazimika kuendelea kujifunza kila mara. Ndiyo maana tunasisitizwa kujifunza kila mara ili kuwa na uelewa mpana kwenye kila sekta ya maisha yetu.
✍πΎ Kundi #4: Watu wasiyo na elimu wala pesa. Hili kundi ambalo halina mbele wala nyuma kuhusu maisha. Watu katika kundi hili hawana mpango wowote wa kujiendeleza kimaisha. Wengi kila jambo kwao ni sawa kwa kuwa hawajisumbui kutafiti zaidi kuhusu jambo husika. Tafsiri yake ni kwamba unapokosa elimu pamoja na pesa unaishi kwenye maisha ya giza kutokana na kuwa na mtazamo hasi kwenye kila sekta ya maisha yako.
✍πΎ Mwisho, neno la tafakari ya leo linatufundisha kuwa pamoja na kuangaika kutafuta pesa tusisahau umuhimu wa kujifunza kila mara. Elimu na pesa ni vitu ambavyo vinatupatia mtazamo chanya kuhusu maisha. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaona tofauti katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
https://fikrazakitajiri.blogspot.com/2020/01/orodha-ya-vitabu-nilivyosoma-katika.html?m=1.
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(