FAHAMU MBINU ZA USOMAJI VITABU KWA TIJA.

NENO LA LEO (AGOSTI 25, 2020): FAHAMU MBINU ZA USOMAJI VITABU KWA TIJA.

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa asubuhi ambayo tumezawadiwa katika kipindi cha uhai wetu hapa Duniani. Ni asubuhi ambayo tuna kila sababu ya kumshukuru Muumba kwa kutuwezesha kuendelea kupiga hatua katika yale tunayofanya. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza mbinu ambazo unaweza kuzitumia kusoma vitabu mbalimbali kwa tija. Neno hili limeandaliwa kutokana na swali la mwenzetu ambaye aliuza jana kupitia jukwa hili. Mara nyingi huwa nasisitiza kuwa ikiwa unazeeka mwili kutokana na kuongezeka kwa umri, sehemu pekee ambayo hautakiwi kuiruhusu izeeke ni ubongo wako. Ubongo unahitaji chakula sawa na ilivyo sehemu nyingine za mwili. Chakula cha ubongo si kingine bali ni kuhakikisha unapata maarifa sahihi kila mara. Tumia mbinu zifuatazo kufanikisha usomaji wa vitabu:-

✍🏾 Mbinu #1: Chagua vitabu kulingana na hitaji lako kwa wakati mhusika. Unatakiwa kuchagua vitabu kwa kuzingatia malengo uliyojiwekea kwenye kila sekta ya maisha yako. Kila kitabu unachosoma ni lazima kijazie kimaarifa na ujuzi kwenye hitaji ulilonalo katika kujiendeleza kwenye kila sekta ya maisha yako. Ikiwa unahitaji kujiendeleza kwenye misingi ya familia na mahusiano, hakikisha unachagua kitabu chenye maudhui hayo. Vivyo hivyo, kwenye masuala ya ukuaji wa kipato, kiroho, kiafya na kijamii.

✍🏾 Mbinu 2: Weka lengo la idadi ya vitabu unayohitaji kusoma katika kipindi maalumu. Hakikisha usomaji wa vitabu unakuwa ni sehemu ya malengo unayojiwekea. Idadi hiyo ya vitabu unayolenga hakikisha inaendaendana na malengo ambayo umejiwekea katika kipindi hicho.

✍🏾 Mbinu #3: Hakikisha kila siku unasoma angalau kurasa mbili mpaka tano. Kila siku unatakiwa kuuliza ubongo maarifa kutoka kwenye kitabu ambacho kipo kwenye ratiba. Husilazimishe kusoma kurasa nyingi ili umalize kitabu mapema na badala yake hakikisha kila unachokisoma unakitafakari kwa kina kwenye uhalisia wa maisha yako.

✍🏾 Mbinu #4: Andaa ufupisho (summary) kile unachojifunza. Ufupisho huu unaweza kuuandika kwenye kijitabu (notebook) chako au hata kwenye simu janja kwa ajili ya rejea kwa baadae. Lengo la kuandaa ufupisho ni kutopoteza kumbukumbu ya maarifa muhimu unayojifunza kutoka kwenye kitabu husika.

✍🏾 Mbinu #5: Weka mpango kutekeleza kwa vitendo yale unayojifunza. Kama ambavyo tumeona kuwa kila kitabu unachosoma ni kwa ajili ya kukuza maarifa na ujuzi kwenye malengo uliyojiwekea katika kipindi maalumu. Baada ya kusoma kitabu wajibu unaofuata ni kuhakikisha unajenga tabia mpya kulingana na kile ulichojifunza. Kama ni kuboresha afya kupitia mazoezi ya viungo, hakikisha kwenye ratiba yako ya kila siku unakuwa na muda wa mazoezi. Kama ni kukuza kipato hakikisha bajeti yako inaonesha kiwango kinachotengwa kwa ajili ya kukuza pato lako. 

✍🏾 Mwisho, neno la tafakari ya leo linatufundisha unavyoweza kusoma vitabu kwa tija. Tumia mbinu hizo kuboresha usomaji wako wa vitabu kwenye kila sekta ya maisha yako. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaona tofauti katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(