FAHAMU KUWA THAMANI YA MAISHA NI KWA VILE HAYAKUPATII KILE UNACHOHITAJI KILA MARA

NENO LA LEO (AGOSTI 24, 2020): FAHAMU KUWA THAMANI YA MAISHA NI KWA VILE HAYAKUPATII KILE UNACHOHITAJI KILA MARA.

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya ambayo inatufungulia juma jipya. Ni siku ya kipekee kwetu kwa ajili ya kuendelea kutoa thamani kwa jamii inayotuzunguka. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza kwa nini siyo kila mara maisha yatakupatia hitaji lako. Tunaishi katika Ulimwengu ambao kila mara tunawajibika kuhitaji kupata zaidi kutoka katika Asili inayotuzunguka. Asili haijawahi kupungukiwa kwa kila anayehitaji ikiwa anajua namna ya kutafuta hicho anachotaka. Hata hivyo, Asili mara zote pamoja na kwamba haijawahi kupungukiwa watu wengi huwa wanapewa kinyume au pungufu na hitaji lao.

✍🏾 Maisha yana thamani kwa vile Asili haitabiriki. Fikiria kama ungeweza kutabiri mahitaji yako yote kwa siku zijazo na ikawa hivyo katika kipindi chote cha maisha yako. Hakika kama tungeweza kutabiri mahitaji yetu na Asili ikatuzawadia kulingana na hitaji la kila mmoja maisha yasingekuwa na maana. Fikiria upo katika Ulimwengu ambao unahitaji kuwa na mwenza wa ndoto yako na hakika unampata wa vile vile. Fikiria upo katika Ulimwengu ambao shughuli za utafutaji unafanikiwa kupata mahitaji yako yote ya kiuchumi bila ya changamoto yoyote.

✍🏾 Fikiria upo katika Ulimwengu ambao ungeweza kuwa na afya hisiyo na changamoto yoyote ya maradhi katika kipindi chote cha uhai wako. Fikiria upo katika Ulimwengu ambao hakuna kuondokewa na ndugu wala rafiki yako ambaye ulimpenda zaidi. Fikiria upo katika Ulimwengu ambao hakuna kupoteza mali au chochote unachomiliki na kukipenda zaidi.

✍🏾 Maisha hayako hivyo ili yawe na thamani. Kadiri unavyopewa au kupata kinyume na matarajio kuna somo unajifunza kuhusu maisha. Kadri unavyobahatika kumpata mwenza uliyempenda fahamu kuwa baada ya kumpata kuna changamoto za kutokuelewana humo ndani. Changamoto kadri unavyozitatua ndivyo maisha ya ndoa yenu yanakuwa na thamani inayotokana na kuvumiliana. Kadri unavyompoteza mpendwa au kitu chochote ulichokipenda zaidi ndivyo unapitishwa kwenye nyakati za kilio na huzuni ili kupitia nyakati hizo ujifunze somo muhimu kuhusu maisha.

✍🏾 Maisha hayatabiriki ili uweke jitihada ya kujifunza zaidi na bidii ya kazi. Ikiwa kama tungepata kila kitu kama ilivyokuwa kwa Adam na Eva enzi za bustani ya Eden hakika watu wasingejifunza mbinu za kukabiliana na maisha. Ikiwa hakuna changamoto yoyote katika utafutaji hata matokeo yasingekuwa na maana kwa mhusika.

✍🏾 Mwisho, neno la tafakari ya leo linatufundisha kuwa maisha hayatabiriki kwa kuwa Asili haitabiriki. Hata hivyo, tunafundishwa kuwa kutotabirika huko ndiko kunaleta thamani ya kwa nini tunaishi. Endelea kujifunza namna ya kukabiliana na Asili hisiyotabirika ili upate zaidi kwenye mahitaji yako. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaona tofauti katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(