👉🏾 Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa asubuhi hii ya leo ambayo ni matumaini yangu kuwa umeamka salama. Ni wakati ambao tuna deni la kusema asante kwa Muumba wetu kutokana na baraka ambazo zimetufikisha siku hii ya leo tukiwa na nguvu na hamasa ya kuendelea kuwa bora zaidi. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza wezi wanne ambao wamekuwa wakikwamisha uzalishaji wetu kwenye sehemu ya kazi au biashara. Tunatambua kuwa mafanikio ni zao la mhusika kuzalisha matokeo yasiyo ya kawaida (extraordinary results) ikilinganishwa na wengine wanaomzunguka. Ili uweze kutoa matokeo yasiyo ya kawaida ni lazima utambue athari ya hawa wezi wanne ambao ninakushirikisha katika makala ya leo:-
✍🏾 Mwizi #1: Kushindwa kusema hapana – Uwezo wa kusema hapana kwenye vitu ambavyo viko nje ya kipaumbele chako ni kipimo cha kuongeza uzalishaji unaotamani. Kila mara utapata vishawishi vinavyokuta uachane na jambo moja ambalo ulikusudia kufanya katika muda maalum ambao umeutenga. Wapo marafiki watahitaji msaada kutoka kwako; wapo watu ambao watahitaji maongezi na wewe; wapo ambao watahitaji ushauri wako; wapo ambao watahitaji mkutane sehemu kwa ajili ya kinjwaji; na wapo ambao watakuhitaji kwa ajili ya mchezo ambao umezoea. Kwa ujumla vishawishi vya kukutoa kwenye kazi ambayo umekusudia kufanya ni vingi kiasi kwamba kama hauwezi kusema HAPANA hautoweza kuendelea na kazi husika. Kadri unavyosema NDIYO kwenye jambo ambalo halikuwa kwenye ratiba yako ni sawa na kusema HAPANA kwenye jambo ambalo ulikusudia kutekeleza katika muda husika. Kumbe, kipaumbele chako kinatakiwa kusema NDIYO kwenye jambo ambalo limeainishwa kutekelezwa katika muda husika na mengine yote husione aibu kusema HAPANA. Mchekeshaji Bill Cosby aliwahi kunukuliwa kuwa: “sijui ufunguo wa mafanikio ni upi lakini ninachojua ufunguo wa kutokufanikiwa ni kujaribu kumridhisha kila mtu”.
✍🏾 Mwizi #2: Uoga wa kero – Unapochagua kuishi kwa ajili ya uzalishaji wenye tija yapo mengi ambayo hayatakuwa sehemu ya maisha ya maisha yako. Tafsiri yake ni kwamba yapo ambayo yataonekana kuwa kero kwa vile hujayafanyia kazi. Hali hii inatokana na ukweli kwamba, kadri unavyowekeza muda wako kwa ajili ya uzalisha yapo matukio mengi kwenye jamii ambayo utaona siyo kipaumbele chako. Hali hii itakufanya matukio hayo yaonekane kuwa kero kwako n ahata jamii inayokuzunguka. Hivyo, uoga wa kero ni mwizi mwingine ambaye anaathiri uzalishaji wako.
✍🏾 Mwizi #3: Tabia mbaya kwa afya yako – Afya bora ina uhusiano mkubwa na uzalishaji wa hali ya juu. Mwili wenye afya njema una uzalishaji mkubwa ikilinganishwa na mwili wenye afya mgogoro. Hivyo tabia ambazo zinadhohofisha afya ni mwizi mkubwa wa uzalishaji katika kutekeleza kusudi la maisha yako. Baadhi ya tabia ambazo zinadhoofisha afya ni pamoja na kukosa muda wa kutosha wa kupumzika; kushindwa kula kwa wakati au kutokula kabisa; kuendekeza vinjwaji vikali; kupenda kula ovyo bila kuzingatia mahitaji ya mwili; uvutaji sigara; pamoja na kutokuwa na muda wa mazoezi.
✍🏾 Mwizi #4: Mazingira Siyo Mazuri kwa ajili ya malengo yangu kuanza – Mazingira yanajumuisha watu wote unaonana nao pamoja na uzoefu wa majukumu yako kila siku. Hivyo, unapotaja mazingira kuhusiana na malengo yako unamaanisha watu wanaokuzunguka kila siku pamoja na sehemu unazokuwa kwenye mzunguko wa siku nzima. Tafsiri yake ni kwamba ili uongeze uzalishaji ni lazima uhakikishe watu wanaokuzunguka pamoja na vitu au sehemu zinazokamilisha mzunguko wako wa siku ziwe upande wa kufanikisha malengo yako. Hapa ni lazima uhakikishe unazungukwa na watu wenye mtazamo chanya sawa na wako vinginevyo ukiruhusu watu wenye mtazamo hasi ni rahisi na wewe kuiga tabia zao. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mtazamo una athari kwenye tabia na hatimaye afya na matokeo yake ni kwenye uzalishaji wa mhusika.
Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza sehemu nne ambazo tunaweza kuzitumia kuongeza uzalishaji katika maisha yetu ya kila siku. Kumbuka pale matokeo yanapokuwa kinyume na matarajio yakow ewe ndo mhusika mkuu wa kujilaumu kwa kuwa umejikwamisha mwenyewe. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika maisha yako yatabadilika. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu
👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾
👐🏾 Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(