MARA ZOTE FAHAMU KUWA WATU WATAZUNGUMZA KILA AINA YA NENO JUU YAKO

NENO LA LEO (AGOSTI 7, 2020): MARA ZOTE FAHAMU KUWA WATU WATAZUNGUMZA KILA AINA YA NENO JUU YAKO

๐Ÿ‘‰๐ŸพHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya ambayo tunaendelea kualikwa kufanya matendo ambayo yatawesha kuboresha maisha yetu. Ni siku ambayo hatuna budi kusema asante kwa Muumba kutokana na baraka ambazo anazidi kutujalia maishani mwetu. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍๐Ÿพ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza tabia za wanadamu tunaoishi nao. Mwanamziki Jose Chameleon aliwahi kuimba kuwa msaliti wako mara nyingi ni yule unayeishi naye au rafiki yako wa karibu. Jambo la msingi ambalo tunajifunza kutokana na wimbo wake ni kwamba binadamu ni kiumbe ambaye hautakiwi kuweka uaminifu wako kwake. 

✍๐Ÿพ Tunaishi katika jamii ambayo kila utalofanya litakosolewa. Na mbaya zaidi ni kwamba unaweza kufanya jambo jema ukashangaa kila mtu anakukosoa au kukupinga na pale unapofanya jambo baya ukajikuta kuna baadhi ya watu wako upande wako. Jambo la msingi ambalo unatakiwa kulifahamu ni kwamba "maneno hayalipiwikodi". Kwa kuwa hakuna ukomo wa maneno kila mtu yuko tayari kuongea analolijua dhidi yako hata kama hana ushahidi wowote.

✍๐Ÿพ Kupitia neno la tafakari ya leo unatakiwa kufahamu kuwa kila hatua utakayopiga kuelekea kwenye mafanikio unayotamani itaambatana na maneno ya kukatisha tamaa. Husipoteze muda kusikiliza maneno hayo kwa kuwa mara nyingi wanaokukosoa ni wale ambao wako chini yako kwa kuwa hao ndo wenye muda wa kupoteza kujadili maisha ya wengine.

✍๐Ÿพ Pia jambo jingine ambalo unatakiwa kulifahamu ni kwamba siyo kila sifa zinazoelekezwa kwako zinatolewa kwa lengo jema. Sifa ya wanadamu ni kwamba wengi hawapendi kumuongelea mtu ukweli pale wanapokuwa nae. Utapewa kila aina ya sifa hila ukiwapa mgongo wanaanza kuzungumza uhalisia wa kilichopo rohoni mwao. Wapo wanaokusifia hili upoteze dira.

✍๐Ÿพ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza moja ya tabia ya mwanadamu. Tumeona kuwa mwanadamu mara zote ataongea dhidi ya mwanadamu mwenzake hata kama hana uhakika juu ya analoongea. Fanya yanayokuhusu, ziba masikio pale inapopaswa na epuka kuongelea watu wengine mambo ambayo hayana tija kwako. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika maisha yako yatabadilika. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.

๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ 

BOFYA HAPA KUCHAGUA UCHAMBUZI WA KITABU UNACHOHITAJI

๐Ÿ‘๐ŸพNakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(