HOFU HOFU IMEKUWA IMEKUWA ADUI WA MAISHA YA MWANADAMU: JE UNAJUA CHANZO CHAKE?

NENO LA LEO (AGOSTI 5, 2020): HOFU HOFU IMEKUWA IMEKUWA ADUI WA MAISHA YA MWANADAMU: JE UNAJUA CHANZO CHAKE?

๐Ÿ‘‰๐ŸพHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya katika siku za uhai wetu ambayo tunaalikwa kuendelea kutoa thamani kwa jamii inayotuzunguka. Ni matumaini yangu kuwa umeamka ukiwa na nguvu na hamasa ya kutosha kwa ajili ya kuendeleza pale ulipoishia jana. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍๐Ÿพ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza kuhusu hofu na chanzo chake katika maisha ya mwanadamu. Tunaishi katika Ulimwengu ambao umejaa matukio ambayo siyo rafiki kwa uendelevu wa maisha yetu. Pamoja na Ulimwengu kuwa na matukio yasiyo rafiki, maisha yanakuwa na thamani pale tunapokuwa na tumaini kuwa matukio hatarishi hayatatupata na badala kuna mengi mema ambayo yanatusubiria.

✍๐Ÿพ Chanzo kikubwa cha hofu kwa Watu wengi ni mambo mengi kama vile kuhofia wapendwa wao kupatwa na changamoto kama vile magonjwa; ajali; athari zitokanazo na vita/ugaidi; Wanyama wakali; ukosefu wa fedha kwa ajili ya mahitaji muhimu ya maisha; vifo vya wapendwa wao (watoto, wenza, wazazi au ndugu wengine); uoga wa kukataliwa au kusalitiwa; na majanga ya kidunia (mafuriko, ukame, tetemeko la ardhi au wadudu waharibifu). 

✍๐Ÿพ Pia, jambo jingine ambalo linapelekea hofu kwa watu ni kuhusiana na usalama wa kazi au biashara zao. Mara nyingi watu wanatimiza wajibu wao kwa ajili ya kuridhisha waajiri wao lakini hiyo haizuii kuondolewa kazini pale mabadiliko ya lazima kwenye taasisi yanapotokea. Hata hivyo, hofu hii inatufanya tushindwe kufurahia maisha kwa kiwango chake. 

✍๐Ÿพ Athari zinazotokana na hofu ni nyingi kwenye maisha ya mwanadamu. Athari hizi zinajumuisha magonjwa yanayotokana na msongo wa mawazo; uhasama katika jamii; ulevi; urahibu (addiction) wa madawa ya kulevya; na kuongezeka kwa watu wenye matatizo yatokanayo na ulaji wa hovyo (eating disorders). Wajibu wetu namba moja ni kuhakikisha tunajifunza mbinu za kukabiliana na hofu ili tupate furaha halisi ya maisha. Ukweli ni kwamba bila kuishinda hofu hakuna chochote ambacho tutafanikisha katika kipindi cha uhai wetu.

✍๐Ÿพ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuhusu vyanzo vya hofu pamoja na athari ya hofu katika maisha yetu. Yapo mengi ambayo yanatujaza hofu japo uhalisia ni kwamba si yote tunayohofia huwa yanatokea maisha mwetu. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika maisha yako yatabadilika. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ 


๐Ÿ‘๐ŸพNakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(